Dilemma: Mke alikiri mtoto wa mwisho si wa mume na kisha akafariki. Mshaurini mume afanyaje baada ya huu usaliti

Dilemma: Mke alikiri mtoto wa mwisho si wa mume na kisha akafariki. Mshaurini mume afanyaje baada ya huu usaliti

Amlee tu, kuna ushahidi upi watakaoutumia wale wa upande wa shemeji kumdai mtoto?
Kwa sasa, hakuna anayejua kwamba yule si mtoto wake zaidi ya yeye, sisi ndugu zake wa karibu na mkewe ambaye ndiyo amefariki.
Kitamaduni watoto atakaozaa mwanamke ni wangu kama nitakuwa nimemtolea mahari ikiwa nitaridhia. Pia mtoto mwenye changamoto ni wa kike, atakuwa na kuolewa ataenda kwake. Tatizo lingekuwa kubwa endapo angekuwa wa kiume
Umenena vyema.
 
Alisema ndugu wa rafiki yake na familia ya mkewe wote ni maisha duni, akimpeleka mtoto huko vijijii atateseka sana, na anapata ugumu maana huyo mtoto anampenda sana baba yake na baada ya mama yake kufariki amebaki naye kama mzazi pekee.
Mambo ni 2 tu hapo Apige kavu au atumie condom.
Either ampeleke Kwa ndugu zake hata kama Wana hali duni ya kimaisha au abaki nae ili aje ashikwe Kwa kosa la jinai.
Kuhusu upendo Huwa unaisha kama yeye upendo wake ulivyoisha Kwa huyo mtoto.
Lakini kama anaweza kujizuia kufanya makosa au kumfanyia vitendo vichafu huyo mtoto basi amlee tu kama Binti yake.
 
Kuna machoko kama Top Gun washampenda marehemu alomvalisha shemej yake na muda huu yupo hivi
 
Attachments

  • 1789795289226.jpg
    1789795289226.jpg
    52.5 KB · Views: 7
binti kiziwi huyu anahitaji kwanza kutenganisha makosa ya wazazi na mtoto. Mtoto hana kosa lolote, wala hakuchagua kuzaliwa hivyo. Miaka 7 amemjua huyo mtu kama baba yake, hivyo kumkataa ghafla kunaweza kumuacha na jeraha kubwa la maisha.

Kwa sasa asifanye uamuzi wa hasira wala kutumia pombe kama njia ya kukabiliana na maumivu. Aongee na mshauri wa familia/saikolojia na ndugu anayemuamini, hasa kabla hajamwambia mtoto kuhusu DNA.

Kumsamehe marehemu si lazima iwe leo; uponyaji unachukua muda. Lakini mtoto huyu anahitaji baba yake sasa kuliko wakati mwingine wowote.
We acha ujinga.. Gambe anywe mpaka adondoke kwenye mtaro ndio uchungu utaisha

Inabidi anywe mpaka ajute kuwa malaya

Kila kitu kina gharama yeye aliwezaje kuzalisha mapacha kwa mfano.! Bao lake lilikuwa sio la kawaida. 🤭

Hapaswi kujuta kila ntu apambane na vita yake🤗
 
😂😂 Hapo umemaliza kabisa. Kila mtu ana vita yake, ila kunywa mpaka kuanguka mtaroni si suluhisho. Afanye maamuzi yake akiwa na akili timamu, maana kila uamuzi una gharama zake.
 
binti kiziwi huyu anahitaji kwanza kutenganisha makosa ya wazazi na mtoto. Mtoto hana kosa lolote, wala hakuchagua kuzaliwa hivyo. Miaka 7 amemjua huyo mtu kama baba yake, hivyo kumkataa ghafla kunaweza kumuacha na jeraha kubwa la maisha.

Kwa sasa asifanye uamuzi wa hasira wala kutumia pombe kama njia ya kukabiliana na maumivu. Aongee na mshauri wa familia/saikolojia na ndugu anayemuamini, hasa kabla hajamwambia mtoto kuhusu DNA.

Kumsamehe marehemu si lazima iwe leo; uponyaji unachukua muda. Lakini mtoto huyu anahitaji baba yake sasa kuliko wakati mwingine wowote.
Umenena kwa busara sana, huu ushauri utamfikia.
 
Hapo aone kama analea yatima tu, afanye kamq kamuadopt kumfanya wa kwake.
Ushauri mzuri
Kinachouma ni kwamba walisaliti ikiw aliwapenda na kuwaamini. Historia ambayo haiwez kurekebishika
Kweli, anaumia kwa sababu amesalitiwa na watu wake wawili wa karibu zaidi na hana hata uwezo wa kuwauliza kwanini waliamua kufanya vile.
 
Anapaswa kushukuru kwa kufahamu ukweli mapema, mshauri alee watoto wote ni wake tena huyo wa kike anaweza kumfaa kuliko wanae anaomini kuwa ni wake.

Nilijifunza jambo moja kwa Wakurya na Wamasai wao wamewafundisha watoto wao wa kiume sio watoto wote watazaliwa ndoani kwake ni wake, ukipata na ukawa unaamini mmoja au wawili kati ya hao ni wako ni jambo la kushukuru maana hata wanaume wana watoto wengine nje ya ndoa zao. Lea wote ni wako
Asante kwa ushauri mzuri, utafika kama ulivyo kwa mhusika.
 
Umenena kwa busara sana, huu ushauri utamfikia.
Kama ni wewe umeamua kuuliza kwa njia ya mtu mwingine, naomba ujue kuwa si jambo jema hasa kwa mwanamke kutoka nje ya ndoa. Inahitaji mwanaume mwenye kifua kipana na mwenye hofu ya M/Mungu kuweza kumlea huyo mtoto la sivyo, huyo baba anaweza kumfanyia vitendo vya ukatili ili kulipiza yale aliyofanyiwa
 
Hakika binafsi nasema inahitaji uwezo wa akili wa hali ya juu unless otherwise mtu anaweza kumfanyia Binti kitu mbaya
 
Back
Top Bottom