Ndugu yangu, kwanza kabisa, pole sana kwa msiba na kwa maumivu makubwa unayopitia. Ulichogundua ni jambo zito sana, na ni kawaida kabisa kuhisi hasira, usaliti, kuchanganyikiwa na hata kutokuwa na uwezo wa kumtazama mke wako kwa mtazamo uleule tena.
Lakini kuna jambo moja muhimu sana unatakiwa kulitenganisha: usaliti wa mama yake si kosa la mtoto.
Huyo mtoto wa miaka 7 hakuchagua baba yake wa kibaolojia, hakujua siri hiyo, hakumsaliti mtu yeyote, na hana uwezo wa kuelewa mzigo wote wa siri uliowekwa juu yake. Kwa miaka saba amekujua wewe kama baba yake, amekupenda kama baba yake na amekujenga ndani ya moyo wake kama baba yake.
Usimwadhibu mtoto kwa kosa ambalo hakulifanya.
Pia, kuwa baba si suala la DNA pekee. DNA inaweza kueleza mtoto alitoka kwa nani kibaolojia, lakini ubaba pia ni uwepo, malezi, ulinzi, upendo, kujitoa na kumlea mtoto tangu akiwa mdogo. Kwa hiyo, hata kama si mtoto wako wa damu, nafasi yako kwake bado ni kubwa sana.
Kwa sasa usifanye uamuzi mkubwa ukiwa ndani ya hasira. Usimwambie mtoto kwamba "mimi si baba yako" kwa sababu tu umeumia. Ukweli huo, ukihitaji kusemwa siku moja, unahitaji kuamuliwa kwa umakini sana, kwa kuzingatia umri wake na ustawi wake wa kihisia, vinginevyo inaweza kuwa sababu ya kupoteza kabisa future ya mtoto. Mtoto wa miaka saba anaweza kuumia sana akiaminishwa ghafla kwamba mtu aliyemjua kama baba yake si baba yake.
Na jambo lingine muhimu: acha pombe isiwe sehemu ya suluhisho. Pombe inaweza kupunguza maumivu kwa muda mfupi, lakini inaweza kuongeza hasira, huzuni, maamuzi ya haraka na kuharibu zaidi uhusiano wako na mtoto. Kila unapohisi hasira unapomtazama mtoto, ondoka kwa muda, pumua, jipe muda usifanye maamuzi ukiwa umelewa.
Mtoto huyu anahitaji baba sasa kuliko wakati mwingine wowote. Wazazi wake wote wa kibaolojia hawapo tena, na mtu anayemjua na kumtambua kama baba yake kwa miaka yote ni wewe.
Usimlazimishe mtoto kubeba madhara ya makosa ya watu wazima.
Mpe muda, mpe upendo, endelea kumlea, inawezekana kabisa utafika mudatukamwangalia huyo mtoto bila kumuona kama kumbukumbu ya usaliti, bali utamwona kama mtoto asiye na hatia ambaye amebaki chini ya uangalizi wako.
Mungu akuongoze vema, kwa jina la Yesu. Amen.