Dilemma: Mke alikiri mtoto wa mwisho si wa mume na kisha akafariki. Mshaurini mume afanyaje baada ya huu usaliti

Ndugu yangu, kwanza kabisa, pole sana kwa msiba na kwa maumivu makubwa unayopitia. Ulichogundua ni jambo zito sana, na ni kawaida kabisa kuhisi hasira, usaliti, kuchanganyikiwa na hata kutokuwa na uwezo wa kumtazama mke wako kwa mtazamo uleule tena.

Lakini kuna jambo moja muhimu sana unatakiwa kulitenganisha: usaliti wa mama yake si kosa la mtoto.

Huyo mtoto wa miaka 7 hakuchagua baba yake wa kibaolojia, hakujua siri hiyo, hakumsaliti mtu yeyote, na hana uwezo wa kuelewa mzigo wote wa siri uliowekwa juu yake. Kwa miaka saba amekujua wewe kama baba yake, amekupenda kama baba yake na amekujenga ndani ya moyo wake kama baba yake.

Usimwadhibu mtoto kwa kosa ambalo hakulifanya.

Pia, kuwa baba si suala la DNA pekee. DNA inaweza kueleza mtoto alitoka kwa nani kibaolojia, lakini ubaba pia ni uwepo, malezi, ulinzi, upendo, kujitoa na kumlea mtoto tangu akiwa mdogo. Kwa hiyo, hata kama si mtoto wako wa damu, nafasi yako kwake bado ni kubwa sana.

Kwa sasa usifanye uamuzi mkubwa ukiwa ndani ya hasira. Usimwambie mtoto kwamba "mimi si baba yako" kwa sababu tu umeumia. Ukweli huo, ukihitaji kusemwa siku moja, unahitaji kuamuliwa kwa umakini sana, kwa kuzingatia umri wake na ustawi wake wa kihisia, vinginevyo inaweza kuwa sababu ya kupoteza kabisa future ya mtoto. Mtoto wa miaka saba anaweza kuumia sana akiaminishwa ghafla kwamba mtu aliyemjua kama baba yake si baba yake.

Na jambo lingine muhimu: acha pombe isiwe sehemu ya suluhisho. Pombe inaweza kupunguza maumivu kwa muda mfupi, lakini inaweza kuongeza hasira, huzuni, maamuzi ya haraka na kuharibu zaidi uhusiano wako na mtoto. Kila unapohisi hasira unapomtazama mtoto, ondoka kwa muda, pumua, jipe muda usifanye maamuzi ukiwa umelewa.

Mtoto huyu anahitaji baba sasa kuliko wakati mwingine wowote. Wazazi wake wote wa kibaolojia hawapo tena, na mtu anayemjua na kumtambua kama baba yake kwa miaka yote ni wewe.

Usimlazimishe mtoto kubeba madhara ya makosa ya watu wazima.

Mpe muda, mpe upendo, endelea kumlea, inawezekana kabisa utafika mudatukamwangalia huyo mtoto bila kumuona kama kumbukumbu ya usaliti, bali utamwona kama mtoto asiye na hatia ambaye amebaki chini ya uangalizi wako.

Mungu akuongoze vema, kwa jina la Yesu. Amen.
 
Marehemu alikosea kuna siri huwa tunakufa nazo
 
Sisi Wanaume tunapitia mengi, ingawa mwamba alichepuka kwanza nadhani shida ilianzia hapo
 
Chai.

Kwamba mnapoishi mmekosa ushauri akakutuma uje JF uombe ushauri halafu u screenshot umtumie.

Huu ni uongo mwepesi.
 
Wa kike huyo amsogeze sogeze taratibu badae anaweka ndani huyo mkewe.
Inakua ngoma droo.
 
Mpaka ameitoa siri ili atubu lazima ilikua imemuelemea, kifo nacho ni fumbo.
 
Mkuu huamini kwenye karma?
Tenda usiyotaka kutendewa.
"usiyotaka"??
 
Asante kwa ushauri mzuri 🙏 , utamfikia.
 
Mkumbushe kuna hatari ya upendo wa watoto wake kwake kuingia doa iwapo watashuhudia mdogo wao akinyanyasika.

Mwambie hana cha kupoteza kumjali huyo mtoto sababu hana baba mwingine anayemfahamu zaidi yake.
Nitamfikishia, shukrani sana.
 
Jamaa ana bahati sana huyo . Sema sijui kama ana itambua hiyo bahati.
 
Aachilie tu hasira kifuani pake, afanye tu kumlea na kutenda wema tu, achukulie kama tu amemu adopt, unajua kosa si lake kosa limeshafanywa na watu ambao tayari wameshatangulia mbele za haki so asamehe tu, najua ni ngumu lakini ajaribu tu, asishushe hasira yake juu ya mtoto huyo
 
ampokee, amleee.......maadui wote weshakufa.... ila ahakikishe anawataarifu ndugu zake...binti hana baya kabisa, aendeleze upendo uliokuwepo. Hasira lazima ziwepo, na inauma kweli, sikia kwa jirani tuu. Mwambie akomae kiume, kinyago amekichonga mwenyewe, kisimtishe.
 
Hao wote ni wapumbavu, hasa mwanamke ndiyo mpumbavu zaidi nini ilikuwa nia yake ilhali babake kashafariki, km ni kwl huyo marehemu ni mwanamke mpumbavu asiye na mfano. Sasa huyo lofa anakuwa mlevi kisa mtoto ni wa ndugu yake? Hao wapumbavu ni kabila gani? Hao wote ni hasara
 
Wewe mwenyewe mkuu ni mtaalamu wa mambo hayo, iweje leo uruke kihunzi kutafuta msaada wa ushauri kwa wadau?

Issue ni ndogo sana kama punje ya haradali hiyo na inasalvika kwa njia ya kuinyamazia bila ya kupiga kelele kwenye publick.

Ingawa mwizi huumia sana akiibiwa, jamaa anatakiwa kujitafakari na kusamehe ili aendelea kumlea kama kawaida huyo mwanaye bila kinyongo wala husda.

Wangapi wanalea watoto wasio wao kwa kujua au kutokujua?

Wangapi wanaasili watoto kwa upendo na kuishi nao maisha yao yote kwa furaha?

Wangapi wanaiba watoto wa wengine ili kukidhi furaha ya kuishi na watoto?

Nimuulize swali: kati ya mtoto wako wa Dna na mtoto wako wa kusingiziwa/kuasili,wana utofauti gani katika future yako?

Ajue kuwa malezi yake mema bila ubaguzi kwa watoto ndiyo hutengeneza mustakabali wao mwema na na kuweka thamani ya mzazi wao rohoni mwao milele-hapo haijalishi ni wake wa Dna au wa kuasili.

Huyo bwana mzee, auvae uvumilivu kisha asamehe na kuendelea kumlea huyo 'mwanaye', maana hajui huko mbele nani 'atayemzika'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…