Dili gani ulipiga likakutoa kimaisha na sisi wengine tujifunze

Dili gani ulipiga likakutoa kimaisha na sisi wengine tujifunze

Wakuu nimekua nikipambana bila mafanikio. Nimejaribu fursa mbalimbali lakini mambo bado bilabila.

Nimejaribu kufanya kilimo changamoto yake ipo kwenye umwangiliaji na soko, nimejaribu kutoa boda za mkataba lakini bado napigwa ngumi za pua.

Najua JF pana wengi na hapakosi kuwa na mengi ya kujifunza!

Hivi ulifanyaje fanyaje hadi ukatoboa? Ni vipi ulipatata financial freedom, dili gani ulipiga likakutoa kimaisha!
Mimi niliwahi piga dili la Ngwair yani dili moja tu lenye akili nikalala maskini na kuamka tajiri.

Nipeni dili masela, maseeela nikamate mahela🎧
 
Moja ya njia za kupata pesa ni hii
Kama una simu kubwa fanya online business pita sehemu wanazouza vitu vya ndani piga picha post kwenye magroup ya WhatsApp na kwenye status zako huwezi kukosa utakuwa unapata cha huu na udalali kutoka kwa wenye Mali zao. Au pita kwenye sehemu wanazo tengeneza vitu vya ndani furniture's piga picha post kwenye magroup ya WhatsApp kitanda cha laki mbili unaandika 250,000 na usafiri ukimpelekea mteja analipia mwenyewe hapo unakuwa umepata cha huu na commission kutoka kwa fundi. Sio kitanda tu furniture's zote.

Unaweza tangaza Biashara za watu nyingi nyingi tu.
Nguo
Perfume
Viatu
Saa na vitu vya nyumbani kama Radios, TV, vyombo vya jikoni nk
Ni jutihada zakk tu.
Kwani yule Jeff Bezos mwenye Amazon naye si ni dalali tu ?
We unaogopa nini. Yaani unakuwa ni Mobile Duka
 
Mkuu dili ni kutokuwa muoga wa kufanya maamuzi.

Sehemu yoyote uliyopo ukiona mambo hayaendi, badili mfumo wa mambo. Masuala ya uvumilivu waachie wanajeshi. Wewe kuwa kinyonga badilika chapu. Ila muhimu ni ujue unataka nini kwenye haya maisha, na ukipambanie.

Hii ni kwa uzoefu wangu binafsi Mkuu.
 
Kama una mtaji kiasi hamia border ya tunduma au Kasumulu kuanzia mwezi wa 4,kama una passport itakua poa zaidi . Hata kama huna passport utatumia zile travel permits za muda mfupi. Kunakua biashara za mazao kwenda pande tofauti za border zinakupa faida faster. Mwaka jana karanga,kitunguu saumu na kitunguu maji toka Malawi kuja Tanzania viliniinua sana,leo nipo South Africa japo nimepoteza tena mtaji 😎😞. Sasa hivi kuna upepo wa mahindi kwenda Malawi.

Tunduma huwa kuna mishe za kupeleka mazao kasumbalesa kama mchele,viazi vya chips,maharage,dagaa nk..
 
Acha kutamani vitu vikubwa katika level ya uharamu.
[emoji117]Hebu jaribu ku import bangi kutoka morogoro, afu ndo uanze kuji pima level nyingine [emoji855]
Kwani hili la bangi lina ugumu gani wakuuu? Maana naendeshaga gari Dsm hadi Mza, Arusha hadi Dom, naweza njia nzima nisimamishwe na trafik, ikitokea ni mara moja moja pia tena ukiwatangulizia elf 5 mkononi hawahitaj hata kuendelea kuongea na ww.

Je huo muda ukiwa umejaza bangi kwenye boot si unatamba tu au?
 
Huu uzi ndio utakaonifanya nijibu pm yako au niiweke pending....[emoji28][emoji28][emoji28]

Ila ningependa sana nione akina dada nao wakija kutoa mawazo na michango yao humu jinsi walivyofanikiwa kimaisha.
Maana naona uzi wote mmejaa wanaume.
Mambo makubwa haya, yanahutaj hustling madame, sio kutafuta wazee wastaaf na madanga.

Moral if the story wengi wa wanawake wanafanikiwa kwa kubebwa kupitia hivyo nilivyotaja hapo juu, wachache mnooo wana real historia ya kufanikiwa
 
Kama una mtaji kiasi hamia border ya tunduma au Kasumulu kuanzia mwezi wa 4,kama una passport itakua poa zaidi . Hata kama huna passport utatumia zile travel permits za muda mfupi. Kunakua biashara za mazao kwenda pande tofauti za border zinakupa faida faster. Mwaka jana karanga,kitunguu saumu na kitunguu maji toka Malawi kuja Tanzania viliniinua sana,leo nipo South Africa japo nimepoteza tena mtaji [emoji41][emoji20]. Sasa hivi kuna upepo wa mahindi kwenda Malawi.

Tunduma huwa kuna mishe za kupeleka mazao kasumbalesa kama mchele,viazi vya chips,maharage,dagaa nk..
Hii Iko poa, kama uko serious tukutane Tunduma hiyo mwezi wa nne tuanze upya kuutafuta huo mtaji uliopotea.
 
Kama una mtaji kiasi hamia border ya tunduma au Kasumulu kuanzia mwezi wa 4,kama una passport itakua poa zaidi . Hata kama huna passport utatumia zile travel permits za muda mfupi. Kunakua biashara za mazao kwenda pande tofauti za border zinakupa faida faster. Mwaka jana karanga,kitunguu saumu na kitunguu maji toka Malawi kuja Tanzania viliniinua sana,leo nipo South Africa japo nimepoteza tena mtaji [emoji41][emoji20]. Sasa hivi kuna upepo wa mahindi kwenda Malawi.

Tunduma huwa kuna mishe za kupeleka mazao kasumbalesa kama mchele,viazi vya chips,maharage,dagaa nk..
Mtaji wa angalau wa kuanzia iwe shi ngapi?
 
Back
Top Bottom