Macbook pro
JF-Expert Member
- Jul 15, 2020
- 722
- 1,030
Habari za wakati huu mwana jamii. Polee kwa majukumu ya kila siku ya kutafuta mkate kwa ajili ya familia yako. Matumaini yangu kuwa wewe unayesoma umzima wa Afya. Niende kwenye mada.
Katina ulimwengu huu tuishio, yapo mpokeo ambayo yamekuwepo toka enzi na enzi. Mapokeo haya yanaweza kuwa ya kiimani, kielimu n. K. Katika moja ya mapokeo yetu ambayo tumekua tukiyapokea ni pamoja na dini au Imani. Ni wazi kwamba mapokeo ya kiimani yanekua na mchango mkubwa wa haya tuliyonayo katika maisha yetu ya kila siku.
Mathalani; Kwenye familia zetu mapokeo moja ya kiimani ambayo tumeyapokea kutoka kwa wakoloni hasa wamagharibi, kuna mambo mengi tu yaliyopo kwenye familia zetu ni matokeo ya dini ambazo hawa watu weupe wamefanikiwa kutushawishi na tumepokea. Katika mapokeo yaliyopo kwenye dini ni pamoja na Hakuna kutengana mpaka kifo.
Hii kauli ni ya kidini sana hasa wakristo, watu wengi wamekuwa wakiteseka, kunyanyasika na wengine hata kupoteza maisha kwa sababu ya huu ujinga huu ujinga wa "Till death do us apart". Mila zetu hazikulazimisha watu kukaa pamoja hata kama hawaelewani au mambo yao hayaendi sawa.
Kuna watu wako kwenye ndoa ambazo wao ni mateka na watumwa wa hizo ndoa ila dini imemlazimisha kuwa hatakiwi kuachana na huyo alienaye hata pale kifo kitakapomuijia. Upuuzi huu ni wakukataa na kupingwa.
Tumepoteza kaka, dada, mama na Baba zetu wengine wakichomwa vifu, wengine wakipigwa risasi, wengine wakipewa ulemavu wa macho na wengine wakichomwa hata majivu kwa mkaa. Tunayo mifano mingi tu na nyinyi ni mashahidi. Dini ya kikristo imetuletea shida na janga kubwa.
Mila zetu zinaturuhusu kuachana endapo mambo hayaendi sawa lakini sio mpaka mmoja afe. Na ni ushamba kulazimisha kuendelea kuishi na mtu ambay huna hisia naye kwani mtu huyu utamtesa kiakili na hata kiroho.
Niwaombe sana ndugu zabgu, tuachane na huu upuuzi wa till death do us apart kwani hutakuja kupewa medali au taji kwa kuvumilia unyanyasaji wa kwenye ndoa hata siku moja na hata hivyo tunaishi mara moja.
Jipe nafasi ya kwanza katika maisha yako, chochote kitakachokua kinataka kukuondoa pale kwenye nafasi ya kwanza kwenye vipaumbele vyako kikatae. Wakristo amkeni na wale ambao mnafurahia ndoa zenu mtu akitaka kuachana na mtu usianze kumwambia mara hivi au vile, hujui ni mangapi ameyavumilia na sasa umefika wakati wa ushindi.
Kataa kukaa kwenye ndoa kama huoni faida au hakuna furaha tena.