Dini ni Chanzo cha watu kunyanyasika kwenye ndoa

Dini ni Chanzo cha watu kunyanyasika kwenye ndoa

Macbook pro

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2020
Posts
722
Reaction score
1,030
Habari za wakati huu mwana jamii. Polee kwa majukumu ya kila siku ya kutafuta mkate kwa ajili ya familia yako. Matumaini yangu kuwa wewe unayesoma umzima wa Afya. Niende kwenye mada.

Katina ulimwengu huu tuishio, yapo mpokeo ambayo yamekuwepo toka enzi na enzi. Mapokeo haya yanaweza kuwa ya kiimani, kielimu n. K. Katika moja ya mapokeo yetu ambayo tumekua tukiyapokea ni pamoja na dini au Imani. Ni wazi kwamba mapokeo ya kiimani yanekua na mchango mkubwa wa haya tuliyonayo katika maisha yetu ya kila siku.

Mathalani; Kwenye familia zetu mapokeo moja ya kiimani ambayo tumeyapokea kutoka kwa wakoloni hasa wamagharibi, kuna mambo mengi tu yaliyopo kwenye familia zetu ni matokeo ya dini ambazo hawa watu weupe wamefanikiwa kutushawishi na tumepokea. Katika mapokeo yaliyopo kwenye dini ni pamoja na Hakuna kutengana mpaka kifo.

Hii kauli ni ya kidini sana hasa wakristo, watu wengi wamekuwa wakiteseka, kunyanyasika na wengine hata kupoteza maisha kwa sababu ya huu ujinga huu ujinga wa "Till death do us apart". Mila zetu hazikulazimisha watu kukaa pamoja hata kama hawaelewani au mambo yao hayaendi sawa.

Kuna watu wako kwenye ndoa ambazo wao ni mateka na watumwa wa hizo ndoa ila dini imemlazimisha kuwa hatakiwi kuachana na huyo alienaye hata pale kifo kitakapomuijia. Upuuzi huu ni wakukataa na kupingwa.

Tumepoteza kaka, dada, mama na Baba zetu wengine wakichomwa vifu, wengine wakipigwa risasi, wengine wakipewa ulemavu wa macho na wengine wakichomwa hata majivu kwa mkaa. Tunayo mifano mingi tu na nyinyi ni mashahidi. Dini ya kikristo imetuletea shida na janga kubwa.

Mila zetu zinaturuhusu kuachana endapo mambo hayaendi sawa lakini sio mpaka mmoja afe. Na ni ushamba kulazimisha kuendelea kuishi na mtu ambay huna hisia naye kwani mtu huyu utamtesa kiakili na hata kiroho.

Niwaombe sana ndugu zabgu, tuachane na huu upuuzi wa till death do us apart kwani hutakuja kupewa medali au taji kwa kuvumilia unyanyasaji wa kwenye ndoa hata siku moja na hata hivyo tunaishi mara moja.

Jipe nafasi ya kwanza katika maisha yako, chochote kitakachokua kinataka kukuondoa pale kwenye nafasi ya kwanza kwenye vipaumbele vyako kikatae. Wakristo amkeni na wale ambao mnafurahia ndoa zenu mtu akitaka kuachana na mtu usianze kumwambia mara hivi au vile, hujui ni mangapi ameyavumilia na sasa umefika wakati wa ushindi.

Kataa kukaa kwenye ndoa kama huoni faida au hakuna furaha tena.

FB_IMG_1686490518361.jpg
 
Kwa ushauri wako watu wakiamua kuufuata ndoa zote zinavunjika...
Sababu hakuna maisha yenye amani 100% hata kama ni wewe na mtoto wako lazima ugomvi uwepo
 
Kwa ushauri wako watu wakiamua kuufuata ndoa zote zinavunjika...
Sababu hakuna maisha yenye amani 100% hata kama ni wewe ni mtoto wako lazima ugomvi
Kwahiyo ndoa ni sehemi ya kukaa roho juu juu na kuvurugana. Watu wakiwa wanajeruhiana waendelee kubaki tu kwenye ndoa ili kumfurahisha nani? Wangapi wachapa watu panga na wengine risasi kwa sababu ya kusema hawawezi kuachana hata kifo.??
 
Watu wakiishi kwa kufuata misingi ya dini hakuna majuto Wala maumivu dini imeeleza watu waishije.
 
Wewe ndo mwenyekiti wa like kundi la 'kataa ndoa, ndoa ni mateso'.
Na kwa taarifa yako hautafanikiwa.
 
Kwahiyo ndoa ni sehemi ya kukaa roho juu juu na kuvurugana. Watu wakiwa wanajeruhiana waendelee kubaki tu kwenye ndoa ili kumfurahisha nani? Wangapi wachapa watu panga na wengine risasi kwa sababu ya kusema hawawezi kuachana hata kifo.??
Ni kujitakia tu....kuzini kumekatazwa lakini bado watu huvunja amri Kwa kuwapelekea moto mpaka kuku....sasa kuvunja ndoa isiyo na afya unashindwia Nini? Unakuwa umejitakia tu
 
Ni kujitakia tu....kuzini kumekatazwa lakini bado watu huvunja amri Kwa kuwapelekea moto mpaka kuku....sasa kuvunja ndoa isiyo na afya unashindwia Nini? Unakuwa umejitakia tu
Best, sijui kama ni kweli wanajitakia. Hebu waza huyu mtu familia yao ji ya kidini sana yaani alfu akutane na unyanyasaji unahisi anaweza kuondoka hapo. Dini zinatesa watu sana. Tena ukiwa die hard fan wa dini mmmh utaishi kwa shida sana na umasikini unakukalia hadi kifo.
 
Hili nalo ni swali mkuu?
Hivi wewe kupigwa na mwenza wako ovyo wakati mwingine kusimangwa hii ni kwa sababu wewe ndio umekosea?? Najua wengi kwa sababu ya dini imezifunga bongo zenu kuelewa mambo katika upana wake.
 
Wewe ndo mwenyekiti wa like kundi la 'kataa ndoa, ndoa ni mateso'.
Na kwa taarifa yako hautafanikiwa.
Utajua hujui. Watu waoane tu na kama furaha ipo basi waishi hadi kifo ila ikitokea huna furaha tena kwenye ndoa yako ondoka achana na mambo ya kukaa hadi kifo kikukute.
 
Hivi wewe kupigwa na mwenza wako ovyo wakati mwingine kusimangwa hii ni kwa sababu wewe ndio umekosea?? Najua wengi kwa sababu ya dini imezifunga bongo zenu kuelewa mambo katika upana wake.
Ndio wewe pengine hujakosea, haya tuchukulie yeye(mnyanyasaji) ndio amekosea, huoni ametoka nje ya malekezo??

NOTE : umetumia neno Waliishi.
 
Dini zote zimeeleza mwanamke anatakiwa aweje na majukumu yake kwenye ndoa na mwanaume pia kaelezwa majukumu yake shidayetu ni kutokufuata misingi ya dini na maarimsho yake hatusomi dini na waliosona hawaifuati tunaishi tunavotaka dini haimfungi mtu ila ni matokeo ya matendo yetu ya ovyo

Before marriage tufuate viongoz was dini watupe mafundisho huenda ikatusaidia
 
Best, sijui kama ni kweli wanajitakia. Hebu waza huyu mtu familia yao ji ya kidini sana yaani alfu akutane na unyanyasaji unahisi anaweza kuondoka hapo. Dini zinatesa watu sana. Tena ukiwa die hard fan wa dini mmmh utaishi kwa shida sana na umasikini unakukalia hadi kifo.
Sitaki ujinga huo mie
 
Fafanua boss
Dini inataka mwanamke amtii mmewe,mume ampende mkewe.mume ni kichwa Cha familia,aliye asisi ndoa aliweka misingi isipofatwa ni lazima migogoro itokee.
Hapo kosa Sio dini bali wanadini kutofata miongozo.
 
Back
Top Bottom