Dini ni kwa ajili ya "Low minded people", Genius can't be trapped!

In God We Trust, Ni neno ambalo lipo kwenye pesa ya Taifa la marekani ( Dollar ), je huwa wanamaanisha nini kwa unavyoelewa ?

Kama hauelewi, Jibu tu kuwa hauelewi na kama unaelewa nasubiri majibu yako.
Marekani ni nchi iliyoanzishwa na ma Freemasons, sharti kubwa la ma Freemason ni kuamini katika Mungu, huwezi kujiunga na ma Freemasons kama huamini Mungu. Mtu kama mimi nisiyeamini Mungu siruhusiwi kujiunga na Freemasons, ila Mkristo, Muislamu au yeyote anayeamini Mungu anaruhusiwa kujiunga na Freemasons.

Hiyo US dollar si tu ina maneno hayo ya "In God We Trust" bali pia ina alama za Freemasons. Most of US presidents were Freemasons.

Hapo pote hakuna linalothibitisha Mungu yupo. Kuna linalothibitishabkuwa walioanzisha taifa la Marekani walikuwa na imani za ki Freemason mpaka kufanya hela yao iwe na alama za ki Freemason.
 
In God We Trust, Ni neno ambalo lipo kwenye pesa ya Taifa la marekani ( Dollar ), je huwa wanamaanisha nini kwa unavyoelewa ?

Kama hauelewi, Jibu tu kuwa hauelewi na kama unaelewa nasubiri majibu yako.
Marekani ni nchi iliyoanzishwa na ma Freemasons, sharti kubwa la ma Freemason ni kuamini katika Mungu, huwezi kujiunga na ma Freemasons kama huamini Mungu. Mtu kqma mimi nisiyeamini Mungu siruhusiwi kujiunga na Freemasons, ila Mkristo, Muislamu au yeyote anayeamini Mungu anaruhusiwa kujiunga na Freemasons.

Hiyo US dollar si tu ina maneno hayo ya "In God We Trust" bali pia ina alama za Freemasons. Most of US presidents were Freemasons. Most of the founders and signers of The Declaration of Independence were Freemasons.

Hapo pote hakuna linalothibitisha Mungu yupo. Kuna linalothibitisha kuwa walioanzisha taifa la Marekani walikuwa na imani za ki Freemason mpaka kufanya hela yao iwe na alama za ki Freemason. Na ma Freemason wanaamini Mungu.
 
Twende kisomi zaidi, usiseme makundi yalikuwa mawili tu pasi na kufafanua kielimu.

Hakuna aliyesema makundi yalikuwa zaidi ya mawili, nimesema huyu Rahbiam bin Suleyman na Yarbiam, walizikusanya au waliyakusanya makabila yanayotokana na uzao au Koo za Yaghudha na Bin Yamini, Hawa wote ni ndugu wa Yusufu, na hizi ni dhuria zao baada ya kupita kitambo kirefu.

Ndio maana nikasema huko mwanzo dola Moja ya Rahbiam ilikuwa kusini mwa Palestina na mji mkuu wake ulikuwa ni Baytul Maqdis na Yarbiam akaanzisha dola iitwayo Israili upande wa kulia wa Palestina. Dola ya Israili ilienda kwa miaka ya 244. Ndio ikadondosha na hao Ashuuriyuun zama za Sarjuni mwaka 722 kabla ya Kristo.

Upande wa Rahbiam kwenye Koo za Yaghudha ilidumu kwa miaka 362. Nchi hii iliangushwa na Mafarao wa Misri. Yaani walirudi tena Palestina (Filistini), na Hawa walikuwa na kisasi na Wana wa Israili.
 
Nimesema atakayekuja kusema walikuwa Watumwa aje na Evidence sio maneno matupu hata Evidence moja tu ntaipokea au any resonable answer..

So Jibu la Ndiyo walikuwa watumwa ambalo halina logic
Ngoja twende kwa maswali, tuambie ni sababu gani ziliwafanya Wana wa Israili watoke Misri na ilikuwaje dola ya Yaghudha ikaanguka na iliangushwa na nani ?
 
Ukija kwa kubishana lazima utashindwa njoo na hoja na ubainifu. Hapo mwanzo nilikwambia Uyahudi una maana zaidi ya Moja yaani ziko nne. Yahudi halikuwa kabila, bali ilikuwa dini, na ukiongelea dini ni itikadi na mfumo wa maisha.
 
Njoo uonyeshe uongo uliopo katika Uislamu na uonyeshe ukweli uliopo katika Ukristo. Sababu najua Wakristo si watu wa kutunza Historia Sasa ndio maana nataka uniambie machimbo ya Historia ya Ukristo kuhusu Uyahudi mmeitoa wapi ? Zaidi ya kwenye vitabu vya Mayahudi na Waislamu ?
 
Sasa naomba twende polepole nikueleweshe...

Kitu ambacho sikulaumu ni kitu Kimoja Umesoma Tarekhe lakini bado hukupata Kusoma Iliyo sahihi ama hukupata mtu aliyekuelekeza Ambaye anajua ama wewe ndo hukujua...

Narudia tena Mimi ni Msomi wa Theology na pia niliwahi kuwa Muslim so najua upande unaoutetea lakini kwakuwa historia ya wana wa israel is not credible kwa upande wa Uislamu ntatumia biblia kama sources ya refference nikueleweshe..

Unakumbuka mwanzoni kabisa nilikuambia kuwa huwezi kupata Historia ya Uisrael uarabuni....
Sasa nifatiliee..

Wana wa israel wamepitia Vipindi Vinne na sio vitatu kama unavyosema...
  • Uongozi wa kiongozi mmoja {na yeye kuteua wasaidizi wake katika kila kabila}(Ama huu uongozi uliitwa Uongozi wa Kikuhani,Kitume,Au unaweza ukaita unavyoweza kuita)
    • Hapa utakuta Viongozi wakiwa kama kina Musa na jopo la Viongozi aliowateua wakiwemo wale wazee 70 kumsaidia kila kabila...
    • Na baada ya kufa Musa alishika kijiti Yoshua bin Nun (au Mnavoita Yusha bin Nun)
  • Uongozi Wa waamuzi (Judges)..
    • Baada ya kifo cha Yoshua Bin Nuni, wana wa Israeli walianza kuishi katika Kanaani (Walipoahidiwa) Waliishi katika makabila kumi na mawili, kila kabila likiwa na kiongozi wake. (kama musa livyopanga)
    • Mungu aliweka waamuzi kati yao ambao ndo walikuwa waamuzi wa maswala yote kato yao.... Wakati wa matatizo, wana wa Israeli walimwita mwamuzi ili awaongoze na kuwasaidia. Waamuzi hao walikuwa watu wa kawaida sana..
    • Mfano wa Waamuzi hao kawatafute uwasome Ehudi (Hudi),shamgari ,Debora,Baraka, Gideoni ,Samson Etc..
  • Uongozi wa kifalme
    • Wakati wa Samweli, wana wa Israeli walianza kutamani kuongozwa na mfalme kama mataifa mengine. Wakamwita Samweli na Jamaa samweli aliwaonya kwamba kuwa na mfalme kutawaletea matatizo, . Kwa hiyo, Samweli alimtia mafuta Sauli kuwa mfalme wa kwanza wa Israeli. Baadae Daudi na kuendelea wengine mpaka kwa kina Nebukandreza huko..
  • Kipindi cha maombolezo
    • Nadhani hata wewe unaamini kuwa ufalme wa Israeli uligawanyika katika falme mbili,
    • ufalme wa Israeli kaskazini (Ambayo ndo iliitwa Israel) na ufalme wa Yuda kusini.
    • Ufalme wa Israeli uliharibiwa na Ashuru mwaka 722 BCE, na ufalme wa Yuda uliharibiwa na Babeli mwaka 586 BCE. Baada ya uharibifu huo, wana wa Israeli waliishi kama watu waliotekwa kwa miaka mingi. Wakati huo, waliongozwa na wazee na manabii.
    • Kipindi hiki wao wanakiita kipindi cha MANABII WADOGO au kipindi cha maombolezo utakuta manabii kama kina Amosi,Hosea,Habakuki ,Sefania,OBADIA ,YONA ,YOELI..etc
Historia yako ya dini unaisoma wapi ? Nitakuuliza swali kipindi hicho unachosema Cha ufalme nani alikuwa Mfalme katika dola hizo mbili ? Leta ushahidi wako na Mimi nikuwekee ushahidi wangu.
Mkuu Mimi Nilikuwa Mtaalamu w Theolojia na pia ni Mwislamu Mstaafu...kwa nachokuambia kiko relible na kimeandikwa sio tu kwwnye vitabu hata kwenye biblia za Kitahudi TANAKH na biblia za kikisto ....

Sasa tuachane na hayo maswali lets hits the topics..
Umesema kipindi cha ufalme ukiwa upande mbili nani alitawala hizo pande mbili...

Swali la kitoto sana ila Nitakujibu japo hata mtoto wa miaka mitano ambaye bado yupo katika ukristo au Aliyesoma Tarekhe atakujibu hili swali..ila kwa faida ya wengi nitakujibu tena kwa Refference...

Mfalme katika Makabila kumi au mfalme wa Israel alikuwa Yeroboamu mwana wa Nebati.
Na Mfalme kwa makabila ya Yuda na Benyamini au Judea Au Yuda alikuwa Rehoboamu Mwana wa suleiman (Kasome Habari hii yote ya falme hizo kugawanyika kwenye 1 Wafalme 11 Mpaka 1 Wafalme 14)
Mimi natumia vyanzo vya wanachuoni wa kiislamu, vyanzo ambayo ni sahihi zaidi kuliko vyanzo vingine, sababu wamzihakiki kwa umakini ..
Huwezi kusema vyanzo wa Wanazuoni wa Kiislamu ni sahihi kuliko vingine hili nalikataaa 😅😅

Ngoja nitakupa mfano mmoja..
Ukiona Sudan wana claim kuwa na historia sahihi ya Tanzania kuliko Tanzania Yenyewe Lazma upate mashaka kwanini wanaclaim hivyo wakati Tanznia wapo na wanahistoria yao...

Kwakuwa nimekujibu upande wako naomba sasa unithibitishie Kuhusu EXODUS
 
Kuna vitu huwa ni muhali sana kwa Wakristo na Mayahudi, yaani vitu vya kihistoria. Nilitaka hili nilishangae.

Nashangaa unasema ulikuwa Muislamu na kweli hukuwahi kuujua Uislamu, ungekuwa umeusoma walau hata kidogo, Wana wa Israili wameongelewa katika Qur'an kadhalika Mayahudi.

Unasahau ya kuwa hata Wapelestina ni katika Waarabu.
Hili unalosema wewe huenda hujajikita katika suala hili la kihistoria. Kusa alikuwa nabii na Mtume wa Allah. Sababu hata katika uongozi wa Rahbiam na Yarbiam ulikuwa ni uongozi wa mmoja mmoja.
Kwa mujibu wa Wanahistoria kipindi cha Jaluti (Shauli) hiki ndio kipindi cha kifalme kwa mujibu wa wanahistoria wote.
 
Tazama hizo Historia za Wakristo zimeandikwa lini na waandishi hizo Historia wametoa wapi Historia zao.

Sasa wewe ndio unatakiwa uihakiki Historia yako unayo iweka hapa.
Japokuwa Woye kwa sasa nawaona hamko sahihi.ila napenda kusema ukweli... Sijakusudia taklit

Historia ya Kikristo yaani Biblia (agano la kale) inakadiriwa kuandikwa miaka 3500 Iliyopita Yaani kipindi cha Babilon exile mwaka 1500 B.C.E

Cha ajabu ni kwamba Historia nyingi za Kiislam ziliandikwa kipindi Cha ijtihad na Taqlid
Kwa maimam kama kipindi cha 109 -116 AH kipindi cha An-Naafi‘, mpaka miaka ya 130-150 AH Kipindi cha Abuu Haneefa,, Au kipinid cha maliki 150-179 AH ...
Na wengine wengine ambayo ukiiweka katika Hisabu ni Miaka ya 800 au 900 na kuendelea
 
Bado hujaonyesha ya kuwa Rahbiam alikuwa Mfalme. Umesema swali la kitoto lakini umeshindwa kuthibitisha ya kuwa hao walikuwa ni Wafalme.
 
We ntakujibu kesho mapema sana
 
Ndio maana nikasema hivi bado mchanga sana katika hii kadhia. Kwanini hujibu maswali ninayo kuuliza ?

Usiniandikie eti imeandikwa miaka 3500, swali ni nani aliandikachiyo Historia na ilikuwa lini ?
 
Wewe toa ushahidi Historia ya Ukristo imeandikwa na nani ? Hiyo Biblia yenyewe unayo isema haikuwepo hata kipindi cha Mtume.

Hivi ushawahi kufanya utafiti wa haya mambo au inasoma kwenye vitabu kisha unafunika tu ?
 
Ngoja twende kwa maswali, tuambie ni sababu gani ziliwafanya Wana wa Israili watoke Misri na ilikuwaje dola ya Yaghudha ikaanguka na iliangushwa na nani ?
Swali ls kitoto turudi kweny Mada tuliyoanza nayo..maswali.mengine hta mwanafunzi wa maddrasa anajibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…