Sasa kaiweka halafu na yeye ndo yumo ndani ya Hiyo Isolation vaccum na yeye ndo energy...
So contadiction
Mimi hapa JF bado nafundisha the classic problem of evil as a contradiction showing the omnipresent, omniscient and all benevolent God does not exist.
That,
1. Either the universe allows evil and God does not exists.
or
2. That God exists and the universe does not allow evil.
That the two, 1 and 2, are mutually exclusive.
Somo rahisi sana kuelewa kwa mtu anayetumia mantiki.
Lakini watu kibao ama hawaelewi, ama wanakataa kuelewa kwa makusudi.
Do not discount the psychological effect called "cognitive dissonance".
Yani mtu anaweza kuelewa kabisa mantiki, lakini, kisaikolojia ikawa vigumu sana kuikubali.
Kama mtu aliyekaa miaka 50 akiamini kuwa mtu fulani ni baba yake wa kibaiolojia, halafu siku moja anapewa DNA evidence kwamba yule si baba yake wa kiabiolojia. Anafanya tests mara tano zote zinaonesha huyu si baba yake.
Kwa cognitive dissonance anajifariji kuwa, anaelewa the DNA test is virtually conclusive, but somehow it is possible that the DNA tests are wrong.
Watu wengi sana wakipata ushahidi usiopingika unaoonesha kuwa fikra zao ni potofu, badala ya kubadili fikra zao ziendane na ushahidi, wanaukataa ushahidi ili wabaki na fikra zao.
Hiki ndicho kinatokea kwa wengi hapa.
Habari za kuwapo kwa Mungu zimepimwa kwa miaka mingi na kuonekana kuwa tuna ushahidi usiopingika kuonesha huyu Mungu muumba vyote, mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hayupo.
Ila, watu wengi hawapendi kuukubali ukweli huo.
Ukweli huu ni mchungu sana, unamaanisha tuko wenyewe, hatuna wa kumuomba, tunatakiwa kutatua matatizo yetu wenyewe.
Ukweli huu ni ukweli wenye kututia ukiwa mkubwa.
Na watu wengi hawaupendi ukiwa huu.
Wanaona ni bora waamini uongo mtamu kwamba kuna Mungu anayetupa tutakachotaka tukimuomba tu, kuliko kukubali ukweli mchungu kwamba huyu Mungu hayupo na tunapata tunayotaka kwa kufanya kazi wenyewe tu.
Hapo ndipo unapata "cognitive dissonance" watu wanaamini Mungu ambaye kimantiki tunaona kabisa hayupo.
I think that, deep in history and evolutionary psychology, the idea of God united societies so much, and served such a useful purpose in surviving, so much so that even as we are waking up and understanding that this is only a made up narrative, it is very hard to shake it off and reject it.
Nakumbuka muandishi Yuval Noah Harari aliongelea hili sana katika kitabu chake "Sapiens: A Brief History of Mankind". Wangapi wanasoma hivi vitabu hapa?
Old habits die hard.
Ndiyo maana ni vigumu kushindana na hii "cognitive dissonance".
Ila, kadiri jamii zinavyoelimika, teknolojua inavyotawala, uongo unazidi kujulikana na watu wanaondoka kwenye ujinga huu.