Umekubali kwamba hoja yako haina mantiki na hujaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Nimejua kuwa hakuna Mungu (mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote) kama vile ninavyojua hakuna mwanamme mwenye miaka 30 leo ambaye mama yake mzazi kibaiolojia ni binti mchanga mwenye umri wa miezi 6 leo, kwa kuangalia "proof by contradiction".
Kama vile ninavyojua kwamba, kwenye hesabu za base ten, square root ya 2 si 10, kwa kuangalia "proof by contradiction".
Kimantiki, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anakuwa contradicted na ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.
Ama ulimwengu ambao mabaya yanawezekana upo, na Mungu hayupo, ama Mungu yupo, na ulimwengu unaoruhusu mabaya haupo.
Mawili haya hayawezi kuwepo kwa pamoja, the two are mutually exclusive.
Tunaona dhahiri ulimwengu unaoruhusu mabaya upo, hivyo, Mungu hayupo.
Kwenye swali lako la kuhusu haya mambo ya maajabu ya complexity, yanayoonekana yamepangiliwa vizuri, yanawezekanaje kuwapo bila Mungu, kwanza kabisa, swali lako limefanya logical fallacy ya logical non sequitur.
Logical fallacy ya logical non sequitur ni kuunganisha mambo ambayo hayana muungano wowote.
Yani, ulichofanya hapo ni kama vile, kuna Waingereza mateka wameokolewa kutoka jela ya Hamas, hatujui nani kawaokoa. Ila, kwa sababu tunajua Waingereza wana jasusi maarufu James Bond 007 kutoka katika filamu zao, basi lazima itakuwa ni James Bond tu kawaokoa. Kama si James Bond nani sasa?
Yani, hujatoa uthibitisho kwamba James Bond yupo kweli, hujatoa ushahidi kwamba James Bond kawaokoa Waingereza mateka wa Hamas, unachukulia ukweli kwamba huna jibu kuwa ndilo jibu kwamba James Bond kaokoa mateka.
Kutokuwa na jibu ni kutokuwa na jibu tu, fanya uchunguzi upate jibu.
Kutokuwa na jibu kwamba maajabu ya dunia yametokeaje na yanaendaje, hakumaanishi jibu ni Mungu. To claim so is a logical non sequitur fallacy.
Zaidi, unaposema kwamba mastaajabu ya dunia na complexity yoyote ni lazima iwe na muumba aliyepangilia mambo, fikra hii, ingawa kwa kutumia akili ndogo inaweza kuonekana kuwa inatetea uwepo wa Mungu, kwamba lazima Mungu awepo na kuumba mambo complex, lakini, ukitumia akili kubwa inayovuka first level thinking, utaona kwamba, hii hoja kwa kweli inaonesha Mungu muumba vyote hayupo na hawezi kuwapo.
Narudia tena, swali lako la imekuwaje vilivyo complex viwepo vyenyewe bila muumba, halioneshi kuwa Mungu yupo, linaonesha kuwa Mungu hayupo na hawezi kuwepo.
Kwa nini?
Kimsingi swali linaonesha kuwa complexity yenye high order haiwezi kutokea yenyewe, ni lazima ipangwe na kuumbwa.
Tukikubali hilo bila exception, hilo litamaanisha hakuna Mungu muumba vyote, kwa sababu Mungu naye atakuwa complex na atahitaji muumba, na muumba wake atahitaji muumba, na muumba wake atahitaji muumba, ad infinitum, ad nauseam.
Hapa ndipo kuna lile swali la watoto lisilojibika. Mungu katoka wapi? Kawepoje?
Hapo unaweza kuwa na mfumo wa mviringo ambao hauna mwanzo wala mwisho, na hivyo hauna muumba wa vyote, lakini huwezi kuwa na mfumo ambao una Mungu muumba wa vyote.
Ukiweka exception yoyote, kwamba inawezekana Mungu ni special case, hapo tayari unakuwa umekwishavunja kanuni ya kwamba kila kilicho complex ni lazima kiwe kimeumbwa, na kwa kuvunja kanuni hiyo, unafungua mlango wa kuwezekana kuwepo ulimwengu wenye vilivyo complex , bila ya Mungu kuwapo.
Hivyo, swali la msingi linakuwa, je, inawezekana ulimwengu ukawa na vitu complex vyenye high order bila kuumbwa kuwa hivyo kwa makusudi maalum?
Ukisema ndiyo, inawezekana, then hapo Mungu hahitajiki kuwepo, kwa sababu complexity kuwapo si lazima Mungu awepo.
Ukisema hapana, haiwezekani complexity kuwapo bila kuumbwa na Mungu, hapo umekataa uwepo wa Mungu, kwa sababu Mungu naye ni complexity, na kama complexity haiwezi kuwapo bila kuumbwa, basi Mungu naye kaumbwa, na kama kaumbwa, basi huyo si Mungu kweli. Si muumba vyote, kwa sababu na yeye kaumbwa.
Vyovyote utakavyolijibu swali hili, linatuonesha Mungu hayupo.