Dini ni kwa ajili ya "Low minded people", Genius can't be trapped!

Dini ni kwa ajili ya "Low minded people", Genius can't be trapped!

Ngoja nikufundishe jambo. Uyahudi una maana nne. Katika maana hizo nne ni maana Moja pekee inayo rejea katika kabila.

Uyahudi sio kabila sababu uzao wa mtoto wa Yakubu aloyeitwa Yahudha (Yuda) haipo tena sababu ulisambaratika katika yale mapigano ya dola mbili zilizo anzishwa na mtoto wa Suleyman aliye itwa Yarbiam na mwenzake aliyeitwa Rahbiam. Hawa walikuja kuanzisha dola mbili zama hizo kwa kukusanya dhuria wa nabii Yakubu, na kilikuwa kimepita kitambo kirefu sana.

Maana nyingine ya tamko Yahudi, ni kurudi nyuma kwa kumtaka msamaha Allah kutokana na matendo maovu waliyo yafanya watu, kadhalika katika maana za tamko hilo ni kurudi kwa sauti za kughuna na kupinga Ngoma, haya yalikuwa yakifanywa na viongozi wa kidini wa zama hizo. Maana ya nne, imenitoka. Ila kwa maelezo zaidi ya Historia ya watu Hawa rejea kitabu kolochoandikwa na mwanachioni aitwae Abdulkaadir Shibatulhamd.

Uyahudi ni dini, na itikadi zao ambazo kwazo zinawatofautisha na wengine, na si nasaba au kabila. Mpaka Musa anaondoka hapakuwepo Uyahudi katika ardhi hii, na hii ni kwa makubaliano ya wanachuoni wote wa Historia, na haijulikani lini kwa hakika Uyahudi ulianza.

Kwahiyo hata huyo Yahudha kipindi wanaunganishwa tena dhuria wake yeye hakuwepo, na hili limefanyika hata nabii Suleyman hakuwepo.
Naelewa Historia Yote ya Israel,Judeans Na hata Waebrania walikotoka na ni kina nani..
Kuanzia kipindi cha Eber (Baba wa waebrania na Mjukuu wa Nuhu)..
Naelewa Israel ilipojitenga na kuwa falme mbili...
Naelewa Pia Israel iliporudi tena kuwa pamoja..

Naelewa pia israel kupoteza makabila Mengine 10 na kibaki na makabila 2 ambayo ni Benyamini na Yuda kwenye vita na Wa Ashuru na Baadae kuungana kwa hizi kabila mbili kati ya Benyamini na Yuda..

Sasa swali langu nilikuuliza kuhusu Musa umenijibu kuhusu Suleyman sasa kati ya Musa na Sulemani nani Ancestor wa mwenzake..

Na kingine nikurekebishe

Yarbiam au Yeroboham alikuwa wa kabila la Efraim na yeye hakuwa mtoto wa Suleiman alikuwa mtoto wa Nabati (Nebati)..

Na kuhusu Rehoboam ndiye alikuwa mtoto wa suleiman aliyezaa na Naamah, binti wa Ammizabad..

Na hapa ndo utawala uligawanyika na Yeroboam kupewa Kutawala makabila 10..

Na suleiman kubaki na makabila 2

Narudia tena swali unasemaje Musa hakuwa Myahudi?
 
Yes, dini ni kwa ajili ya watu wasio na ufikiri sahihi. Dini ina vitu ambavyo ni vya watu wa akili za chini sana.

Vitabu vyote vya dini vina michanganyo isiyohitaji hata kutumia nguvu kujua kuwa "hapa tumepigwa na tunaendelea kupigwa"

Sayansi imejibu maswali mengi sana ambayo dini ilishindwa kuyajibu na kuishia kuwaambia wafuasi waamini tu bila kuona!

Sayansi imetibu magonjwa complex ambayo dini haijawahi hata kuyagusa, inaishia kujipenyeza kitapeli tu.

Mf katika mgogoro wa leo wa Gaza, dunia imegawanyika. Watu wasio na uelewa wanaishia kuchagua upande wa dini A na dini B. Wale wanaoiunga mkono Israel kwa kisa cha dini ya ukristo wajue kuwa % kubwa ya waisrael hawaamini ktk dini na Marekani 86% hawana dini. Pale kinachogombewa ni Maslahi tu!

Dini zetu tungeachana nazo tungekuwa na maendeleo makubwa. Mf China na Nchi za Ulimwengu wa kwanza, nyingi zimeachana na mambo ya dini na zinaendelea sana.

Watu wanavumbua issues za drones, AI na mirobotic machines kibao we unakesha kanisani eti uwe millionea, sijui upate mtoto real?

Unalala na vichupa vya maji sijui chumvi na mafuta ya upako upate gari, are u serious?

Nilikua namsikiliza Shehe/Maalim mmoja anasema wale kunguni wa Ufaransa ni jeshi la Allah limekuja kuwaangamiza kisa wana madhambi...are we real serious?

Dini zina mfumo ambao Unatufanya "tuwe limited" kwenye ufikiri na uvumbuzi.

Live your live, Death is the Ending game! Dini ni ulaji wao!

Atheists make sense than who are not
Mkuu...

Usipomuabudu Mungu ni lazima utamuabudu shetani.

Unafikiri Hao watu wenye ushawishi duniani hawana wanachokiabudu kisa wamekuambia hawana dini?

Na Kwa akili Yako ukawaamini kabisa...

Sasa nikuambie Kila jamii Ina Miungu Yao.

Hao wajapani wachina bado wanafanya matambiko Hadi sasa.

Ukiskia mtu anahamasisha wanaume waoane ujue maagizo ya dini yake...

Alafu nikueleze, Kwa mfano, sio Kila nyimbo msanii au watu wa Injili wanazitunga, nyingine wanapewa ndotoni, NA NANI?

Hata vumbuzi usifikiri eti yote ni akili ya kibinadamu, kuna usaidizi...

Dini...

Iweje uamini kuna Plasmodium ukatae kuna Mungu?

Haya umba hata Jani la nyasi liote liwe hai tujue uwezo wako...
 
Mbona nimekujibu ...nimekuambia ilikujua ni yeye au la ..unatakiwa kumcha kwanza ndipo atakujulisha kama ni yeye au la
This is circular logic. A logical fallacy.

Ili kujua kuwa mimi ni Elon Musk bilionea wa kwanza wa dunia unatakiwa kunikubalia kwanza kama mimi ni Elon Musk.

Mimi ni Elon Musk. Kubali.

Umekubali?

Kama umekubali.

Umejua kuwa mimi ni Elon Musk?
 
This is circular logic. A logical fallacy.

Ili kujua kuwa mimi ni Elon Musk unatakiwa kunikubalia kwanza kama mimi ni Elon Musk.
Inabidi umtafute huyo elon musk hadi umpate ni njia nzuri na sahihi zaidi ....ukisoma kwenya agano la kale kuna mtu alimcha mungu alilalamika kwa mungu akisema .....zipo wapi zile sifa na nguvu na maajabu ya mungu ambayo babu zetu walituadithia ndipo mungu akamtuma malaika na kumwambia cha kufanya
 
Kwahiyo Kwa upande wako Google ndiyo ina universal definitions ya vitu vyote duniani? Google haijakuachia room ya kutumia kichwa chako?

Kichwa chako unatumia kufanyia nini sasa?

Hatuwezi kukubaliana kwenye hilo,...Baki na mtazamo wako mzee
Mkuu
Hata wewe na yeye hamjatofautiana maana ulijaribu kumuonyesha maana ya DINI kutoka kwenye a siku ya neno ambalo ni kiarabu, lakini yeye amesema haikubali hiyo maana sababu zipo maana nyingine zaidi ya uliyomtajia wewe.

Huoni Kama mkuu hapo mpo sawa? Yeye kagugo ya kingereza wewe ya kiarabu
 
Inabidi umtafute huyo elon musk hadi umpate ni njia nzuri na sahihi zaidi ....ukisoma kwenya agano la kale kuna mtu alimcha mungu alilalamika kwa mungu akisema .....zipo wapi zile sifa na nguvu na maajabu ya mungu ambayo babu zetu walituadithia ndipo mungu akamtuma malaika na kumwambia cha kufanya
Mpaka sasa unapiga hadithi tu, tena za kusimuliwa.

Hujathibitisha Mungu yupo.

Umejua mimi ni Elon Musk?

Ukipinga mimi ni Elon Musk ni sawa na umepinga uwepo wa Mungu.

Kwa sababu kanuni uliyoitaja ya kukubali uwepo wa Mungu, ndiyo hiyo hiyo niliyoitumia kukuambia mimi ni Elon Musk, bilionea wa dunia.

Umekubali mimi ni Elon Musk?
 
Na wewe tuambie umejuaje kua hakuna mungu ? Je vitu vyote vimejipanga na kujiumba kwa mpangilio mkuu wenye akili sana pasipo aliye vipangilia au useme hakuna kilicho na akili kubwa kilicho pangilia mambo haya yenye akili kubwa mfano biology ya binadamu tu ...ukicheki mpangilio wake ni wenye akili kubwa sana je ulijitengeneza wenyewe ....tumia akili ni mpumbavu tu asemaye hakuna mungu
 
😂So Mungu muweza wa yote alishindwa kuwatokea hao mpaka atumie wamisheni...😂ameweza kutokea kwenye ka jangwa huko middle east...huyu Mungu mbona kama ametungwa na kusambazwa Kama novel
Mkuu ngoja nikuitie huyu mtu hapa
DR Mambo AMP atuambie kuna historical evidence yoyote Kama Israel washawahi kuwa utumwani misri? Kwa uchache mkuu
 
Mungu yupi?swali gani hilo la kijinga MUNGU ni mmoja tu duniani kote aliyeumba dunia na vitu vyote vilivyomo iwe china,india,korea,nk.

Ujinga wa waafrikana ni kuamini kuwa kuna MUNGU wa wazungu aliye wa kweli na siyo wa WAAFRIKA

Shit holes
Pole sana wa jazba na matusi mkuu.

nmeuliza hivyo Coz kila dini inaamini Mungu wanaemuabudu ni wa kwel zaidi ya dini nyingne.

Dini zote duniani kila mmoja anaona mwenzake kapotoka yeye ndio yupo sahihi zaidi ya mwingine.

Sasa wewe naona kabisa umekurupuka kwa hasira na kupinga swali langu , bila kuwa na hoja ya msingi kwa utetezi wa jibu lako , zaidi ya kulalamika tu na matusi.
 
Mkuu ngoja nikuitie huyu mtu hapa
DR Mambo AMP atuambie kuna historical evidence yoyote Kama Israel washawahi kuwa utumwani misri? Kwa uchache mkuu
Hakuna physical Exodus Wala Kutoka utumwani Kama watu wanavyojiaminisha mkuu..😅😅

hakuna Evidence inayosuggest Kuwa Misri kulikuwa na Watumwa wa kabila lolote la waisrael..Hakuna hata mchoro mmoja wa Waisrael misri...

Atakayekuambia kulikuwa na physical exodus mwambie akuonyeshe Evidence then Nitag mkuu..

NB: Nakuacha na Tafakuri Nduguze na Yusuph walitoka kanaani kwenda Misri zaidi ya Mara tatu kwa wiki chache kwenda na kurudi...
soma Mwanzo 42- mwanzo 44...
jiulize kama walikuwa wakiena na kurudi kwa wiki kadhaa na Kilomita ni zile zile njia ni ile ile walishindwaje kutumia MUDA WA WIKI AU HATA BASI MIEZI AU MWAKA WALIPOKUWA WANARUDI KANAANI baada ya Utumwa..
😅😅
 
Mungu yupi?swali gani hilo la kijinga MUNGU ni mmoja tu duniani kote aliyeumba dunia na vitu vyote vilivyomo iwe china,india,korea,nk.

Ujinga wa waafrikana ni kuamini kuwa kuna MUNGU wa wazungu aliye wa kweli na siyo wa WAAFRIKA

Shit holes
India wana Mungu wao Tangu Miaka 5000 BC Iliyopita kabla ya kuingia Maswala yenu ya Uyahudi wala UKRISTO..
Wachina wana Mungu wao Na dini yao ina umri mrefu kuliko Wayahudi na Wakristo..

Wasamaria Tena huku mpaka kuna Baadhi ya Visa biblia imekopi kutoka kwao na wana Miungu yao Na ambayo Ina umri mrefu zaidi ya Mungu wa Yakobo..na Ibrahimu..

Aliyeletwa na Musa..
Wewe uliyezaliwa katika Ukristo unaamini Ukristo,,Na mchina aliyezaliwa katika Uchina anaamini yake ...
Na kila mtu katika sehemu alipokulia na Mazingira yake..

Ukiwa katika Jukwaa la Intelligence unatakiwa uwe Na wewe Intellectual ....

Bishana au Jibu kwa Hoja matusi kejeli nafikir sio shemu ya intellgint mind...Mihemko huenda kwa wajinga tu....

Na Hata biblia Yako inasema "Hasira hukaa kifuani mwa Mpumbavu"
 
Yes, dini ni kwa ajili ya watu wasio na ufikiri sahihi. Dini ina vitu ambavyo ni vya watu wa akili za chini sana.

Vitabu vyote vya dini vina michanganyo isiyohitaji hata kutumia nguvu kujua kuwa "hapa tumepigwa na tunaendelea kupigwa"

Sayansi imejibu maswali mengi sana ambayo dini ilishindwa kuyajibu na kuishia kuwaambia wafuasi waamini tu bila kuona!

Sayansi imetibu magonjwa complex ambayo dini haijawahi hata kuyagusa, inaishia kujipenyeza kitapeli tu.

Mf katika mgogoro wa leo wa Gaza, dunia imegawanyika. Watu wasio na uelewa wanaishia kuchagua upande wa dini A na dini B. Wale wanaoiunga mkono Israel kwa kisa cha dini ya ukristo wajue kuwa % kubwa ya waisrael hawaamini ktk dini na Marekani 86% hawana dini. Pale kinachogombewa ni Maslahi tu!

Dini zetu tungeachana nazo tungekuwa na maendeleo makubwa. Mf China na Nchi za Ulimwengu wa kwanza, nyingi zimeachana na mambo ya dini na zinaendelea sana.

Watu wanavumbua issues za drones, AI na mirobotic machines kibao we unakesha kanisani eti uwe millionea, sijui upate mtoto real?

Unalala na vichupa vya maji sijui chumvi na mafuta ya upako upate gari, are u serious?

Nilikua namsikiliza Shehe/Maalim mmoja anasema wale kunguni wa Ufaransa ni jeshi la Allah limekuja kuwaangamiza kisa wana madhambi...are we real serious?

Dini zina mfumo ambao Unatufanya "tuwe limited" kwenye ufikiri na uvumbuzi.

Live your live, Death is the Ending game! Dini ni ulaji wao!

Atheists make sense than who are not
Umeandika kitu sahihi. Dini zinatutafuna hadi wenye akili na kujua wanaogopa kusema mbele ya wajinga. Wajanja waovu wanawala wajinga sana kupitia dini.
 
Although born into an Anglican family, and a devout but heterodox Christian, by his thirties Sir Isaac Newton held a Christian faith that, had it been made public, would not have been considered orthodox by mainstream Christians.

Albert Einstein famously wrote: “Science without religion is lame, religion without science is blind.”
 
Mkuu
Hata wewe na yeye hamjatofautiana maana ulijaribu kumuonyesha maana ya DINI kutoka kwenye a siku ya neno ambalo ni kiarabu, lakini yeye amesema haikubali hiyo maana sababu zipo maana nyingine zaidi ya uliyomtajia wewe.

Huoni Kama mkuu hapo mpo sawa? Yeye kagugo ya kingereza wewe ya kiarabu
Sijasema tafsiri niliyotoa Mimi ndiyo sahihi, au yake ndiyo sahihi,.. Bali yeye alikua analazimisha kwamba definition aliyoitoa Google ndiyo sahihi,.. Ndiyo maana nikamuuliza Google ndiyo ina Universal accepted definitions?
 
Katika kufanya vitu kisayansi na kuthibitisha fanya ujaribu kitu kimoja. 'Uexperiment'

Amua kutumia data zinazofikika na wewe binafsi, kutetea au kupinga dhana fulani fulani. Ntafafanua.

Mfano kwenye vya kuonekana achana na vya darubini; mambo ya anga za mbali, nebula na sayari. Chukua unavyoona kwa macho, kwa miwani na hata ukifika kwa hadubini ya mwanga kama seli na tishu. Lakini achana na vilivyo tata zaidi kama vya electron microscope. Tafuta ushahidi humo.

Maana unajuaje kama hakuna uwezekano elimu fulani ikawa imebuniwabuniwa tu (kama moon landing labda ingekuwa ni uongo kweli) yakaundwa ma modeli halafu yakawa hata ni sio au hayajakamilika kwa hiyo yakakupa tafsiri mbovu ya uhalisia?

Unaweza kukuta hawaioni cause ya effect kwa sababu kuna cause ambayo bado haipimiki au haijagundulika inayoviweka katika mwendo. Sayansi inakua kila siku.

Mathayo 11:25-26​

Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.
 
Msiomwamini MUNGU tuonyesheni solution na sio mnakuwa na maneno MENGI.Kwamba marekani hawana dini na Israel hawana dini ila vita inayoendelea pale ni ya maslahi [Nonsense} Kwa wapalestina kuna maslahi gani? Gaza kuna nini zaidi ya boti za uvuvi....Badala ya kupiga kelele hapa kwamba MUNGU hayupo andikeni solution za mgogoro wa mashariki ya kati,,solution ya umaskini wa Afrika na solution ya elimu duni ya Afrika...Ninyi atheist mliozaliwa mchafukoge mkasoma bunge na chuo kikuu cha mlimani bado elimu yenu ni duni tu.
 
Na wewe tuambie umejuaje kua hakuna mungu ? Je vitu vyote vimejipanga na kujiumba kwa mpangilio mkuu wenye akili sana pasipo aliye vipangilia au useme hakuna kilicho na akili kubwa kilicho pangilia mambo haya yenye akili kubwa mfano biology ya binadamu tu ...ukicheki mpangilio wake ni wenye akili kubwa sana je ulijitengeneza wenyewe ....tumia akili ni mpumbavu tu asemaye hakuna mungu
Umekubali kwamba hoja yako haina mantiki na hujaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Nimejua kuwa hakuna Mungu (mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote) kama vile ninavyojua hakuna mwanamme mwenye miaka 30 leo ambaye mama yake mzazi kibaiolojia ni binti mchanga mwenye umri wa miezi 6 leo, kwa kuangalia "proof by contradiction".

Kama vile ninavyojua kwamba, kwenye hesabu za base ten, square root ya 2 si 10, kwa kuangalia "proof by contradiction".

Kimantiki, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anakuwa contradicted na ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.

Ama ulimwengu ambao mabaya yanawezekana upo, na Mungu hayupo, ama Mungu yupo, na ulimwengu unaoruhusu mabaya haupo.

Mawili haya hayawezi kuwepo kwa pamoja, the two are mutually exclusive.

Tunaona dhahiri ulimwengu unaoruhusu mabaya upo, hivyo, Mungu hayupo.

Kwenye swali lako la kuhusu haya mambo ya maajabu ya complexity, yanayoonekana yamepangiliwa vizuri, yanawezekanaje kuwapo bila Mungu, kwanza kabisa, swali lako limefanya logical fallacy ya logical non sequitur.

Logical fallacy ya logical non sequitur ni kuunganisha mambo ambayo hayana muungano wowote.

Yani, ulichofanya hapo ni kama vile, kuna Waingereza mateka wameokolewa kutoka jela ya Hamas, hatujui nani kawaokoa. Ila, kwa sababu tunajua Waingereza wana jasusi maarufu James Bond 007 kutoka katika filamu zao, basi lazima itakuwa ni James Bond tu kawaokoa. Kama si James Bond nani sasa?

Yani, hujatoa uthibitisho kwamba James Bond yupo kweli, hujatoa ushahidi kwamba James Bond kawaokoa Waingereza mateka wa Hamas, unachukulia ukweli kwamba huna jibu kuwa ndilo jibu kwamba James Bond kaokoa mateka.

Kutokuwa na jibu ni kutokuwa na jibu tu, fanya uchunguzi upate jibu.

Kutokuwa na jibu kwamba maajabu ya dunia yametokeaje na yanaendaje, hakumaanishi jibu ni Mungu. To claim so is a logical non sequitur fallacy.

Zaidi, unaposema kwamba mastaajabu ya dunia na complexity yoyote ni lazima iwe na muumba aliyepangilia mambo, fikra hii, ingawa kwa kutumia akili ndogo inaweza kuonekana kuwa inatetea uwepo wa Mungu, kwamba lazima Mungu awepo na kuumba mambo complex, lakini, ukitumia akili kubwa inayovuka first level thinking, utaona kwamba, hii hoja kwa kweli inaonesha Mungu muumba vyote hayupo na hawezi kuwapo.

Narudia tena, swali lako la imekuwaje vilivyo complex viwepo vyenyewe bila muumba, halioneshi kuwa Mungu yupo, linaonesha kuwa Mungu hayupo na hawezi kuwepo.

Kwa nini?

Kimsingi swali linaonesha kuwa complexity yenye high order haiwezi kutokea yenyewe, ni lazima ipangwe na kuumbwa.

Tukikubali hilo bila exception, hilo litamaanisha hakuna Mungu muumba vyote, kwa sababu Mungu naye atakuwa complex na atahitaji muumba, na muumba wake atahitaji muumba, na muumba wake atahitaji muumba, ad infinitum, ad nauseam.

Hapa ndipo kuna lile swali la watoto lisilojibika. Mungu katoka wapi? Kawepoje?

Hapo unaweza kuwa na mfumo wa mviringo ambao hauna mwanzo wala mwisho, na hivyo hauna muumba wa vyote, lakini huwezi kuwa na mfumo ambao una Mungu muumba wa vyote.

Ukiweka exception yoyote, kwamba inawezekana Mungu ni special case, hapo tayari unakuwa umekwishavunja kanuni ya kwamba kila kilicho complex ni lazima kiwe kimeumbwa, na kwa kuvunja kanuni hiyo, unafungua mlango wa kuwezekana kuwepo ulimwengu wenye vilivyo complex , bila ya Mungu kuwapo.

Hivyo, swali la msingi linakuwa, je, inawezekana ulimwengu ukawa na vitu complex vyenye high order bila kuumbwa kuwa hivyo kwa makusudi maalum?

Ukisema ndiyo, inawezekana, then hapo Mungu hahitajiki kuwepo, kwa sababu complexity kuwapo si lazima Mungu awepo.

Ukisema hapana, haiwezekani complexity kuwapo bila kuumbwa na Mungu, hapo umekataa uwepo wa Mungu, kwa sababu Mungu naye ni complexity, na kama complexity haiwezi kuwapo bila kuumbwa, basi Mungu naye kaumbwa, na kama kaumbwa, basi huyo si Mungu kweli. Si muumba vyote, kwa sababu na yeye kaumbwa.

Vyovyote utakavyolijibu swali hili, linatuonesha Mungu hayupo.
 
Back
Top Bottom