Dini ni kwa ajili ya "Low minded people", Genius can't be trapped!

Dini ni kwa ajili ya "Low minded people", Genius can't be trapped!

[emoji23]Asa unatakaje mfano..maana una namna yako ya kuelewa biblia unaona ni sahihi...same as everyone else
Ninazo sababu za msingi ...mfano madhehebu je jesu ni mlokole je yesu ni msabato je yesu ni mkatoriki? Je ingetokea yesu karudi leo kufundisha dini angewaambia watu wawe wakatoliki au wasabato au yeye angekwenda kanisa gani?
 
Ndio..coz bila binadamu Mungu hawezi exist..Mungu anamtegemea binadamu kuexist...Mungu angekuwa mkuu kuliko binadamu asingetegemea binadamu ili ajulikane angemtokea kila mtu..
Na angemtokea kila mtu na akafa sababu ya Mungu jinsi anavyoichukia dhambi ungesema Mungu muonevu kwanini asiwatokee watu wachache watakatifu ili sisi wengine tupone. Wakati Mungu anamtokea Mussa kumpa zile mbao mbili hivyo hivyo wafuasi wake waliomba waongee na Mungu direct radi zilizopiga pale sio kawaida mpaka wote wakaogopa wakasema ongea nae we mwenyewe Mussa. Na Mungu angefanya kadri wanadamu mnavotaka huyo asingekuwa Mungu maana angekuwa anaakili sawa na binadamu.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Ninazo sababu za msingi ...mfano madhehebu je jesu ni mlokole je yesu ni msabato je yesu ni mkatoriki? Je ingetokea yesu karudi leo kufundisha dini angewaambia watu wawe wakatoliki au wasabato au yeye angekwenda kanisa gani?
Usiniulize Mimi asa...waulize wakristo
 
Na angemtokea kila mtu na akafa sababu ya Mungu jinsi anavyoichukia dhambi ungesema Mungu muonevu kwanini asiwatokee watu wachache watakatifu ili sisi wengine tupone. Wakati Mungu anamtokea Mussa kumpa zile mbao mbili hivyo hivyo wafuasi wake waliomba waongee na Mungu direct radi zilizopiga pale sio kawaida mpaka wote wakaogopa wakasema ongea nae we mwenyewe Mussa. Na Mungu angefanya kadri wanadamu mnavotaka huyo asingekuwa Mungu maana angekuwa anaakili sawa na binadamu.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
😂Usiniletee mfano ndani ya Novel bana...hao watakatifu tunajuaje kweli wametokewa na sio agenda kututawala...😂we Mungu mmoja ulimwengu wote anatokea watu buku na kuwapa maneno buku tofauti..biblia tu Ina story buku tofauti kuhusu Mambo mbalimbali..bado Kuna Hawa manabii feki..bado Kuna dini nyingine nyingi...hii ni product ya kila mtu kuamka na kusema ametokewa na Mungu kumbe ni kichwa chake tu
 
Hiki ulichokiandika kimeonyesha wazi huijui Historia. Wana w Israili wamepitia katika vipindi vitatu kwa mujibu wa wanahistoria. Cha kwanza ni kipindi cha makadhi, Cha makadhi kipindi hiki kilisimamiwa na Yusha bin Nuun, kikaja kipindi cha Muluki yaani ufalme hapa wakapelekewa mfalme Jaluta kwa Mayahudi wanamuita Shauli, kipindi cha tatu ni Inqisam (Mgawanyiko) ambapo hapa walifanya mtoto wa Suleyman na yule mwingine.

Historia yako ya dini unaisoma wapi ? Nitakuuliza swali kipindi hicho unachosema Cha ufalme nani alikuwa Mfalme katika dola hizo mbili ? Leta ushahidi wako na Mimi nikuwekee ushahidi wangu.


Sahihi kabisa Yahudha alikuwa mtoto wa Yakubu na ni ndugu wa Yusufu Hawa walikuwa kabla ya Musa. Yusufu alipopta uongozi kule Misri akaamua kumuita baba yake na ndugu zake wakatoka Palestina kwenda Misri. Ukoo huu wa Israili (Yakubu) waliishi kwa amani sana pale Misri kipindi Yusufu yupo hai, baada ya kufariki Yusufu, Wana wa Israili waliishi kwa tabu sana na dhiki sana, ndipo akatumwa Musa kuwakomboa na kuwatoa Misri kuwarudisha kwao, kabla ya kuwafikisha Palestina Musa alifariki na Yusha bin Nuun, akalifanikisha lengo lao la kuwarudisha Palestina, kisha akawagawanya katika makundi kumi na kila kundi akaliwekea kadhi yaani mtu wa kuwahukumia majambo yao.

Kipindi cha dhuria wa Yahudha na bin Yamini, si kipindi cha Ufalme kijana ni kipindi cha mgawanyo wa dhuria wa ndugu hao wawili wa Yusufu.

Mimi natumia vyanzo vya wanachuoni wa kiislamu, vyanzo ambayo ni sahihi zaidi kuliko vyanzo vingine, sababu wamzihakiki kwa umakini Historia kuliko watu wengine wote. Hili ukitaka ushahidi pia nakupa.

Tazama hizo Historia za Wakristo zimeandikwa lini na waandishi hizo Historia wametoa wapi Historia zao.

Sasa wewe ndio unatakiwa uihakiki Historia yako unayo iweka hapa.
Kwahiyo hao waislamu wanajua sana historia ya wayahudi kuliko hata wayahudi wenyewe? Maana wayahudi biblia yao inatumia maandiko sawa na agano la kale la biblia takatifu.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
We umeshashikwa relax endelea kushikwa. Umejiuliza kwa nini viongozi wa makanisa ni matajiri walio wengi , it is a business.
Wewe mwafrika umeibiwa na sayansi kuliko dini ila bado unaitetea na kuishobokea hapa. Watu wamaefikaje hapa africa kirahisi(sayansi) wamechimbaje vya kuchimba vyetu( sayansi) wameachaje neo colonialism ( sayansi) wamewezaje kukutamanisha wewe na kizazi chako fantasy world ikiwa na wao wanastruggle( sayansi) . Waliwatandikaje risasi babu zako( sayansi), wakatengenezaje mifumo ya kukutawala kwa misaada na malimbikizo makbwa ya madeni( sayansi). Je, vipi kuhusu kitendo cha kukuulia kizazi chako kwa magonjwa kama ukimwi na kuendelea kukupa madawa yanayoharibu kizazi chako( sayansi) na madudu kibao ni sayansi ila wewe kwako dini ndo inaiba sana.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Wewe mwafrika umeibiwa na sayansi kuliko dini ila bado unaitetea na kuishobokea hapa. Watu wamaefikaje hapa africa kirahisi(sayansi) wamechimbaje vya kuchimba vyetu( sayansi) wameachaje neo colonialism ( sayansi) wamewezaje kukutamanisha wewe na kizazi chako fantasy world ikiwa na wao wanastruggle( sayansi) . Waliwatandikaje risasi babu zako( sayansi), wakatengenezaje mifumo ya kukutawala kwa misaada na malimbikizo makbwa ya madeni( sayansi). Je, vipi kuhusu kitendo cha kukuulia kizazi chako kwa magonjwa kama ukimwi na kuendelea kukupa madawa yanayoharibu kizazi chako( sayansi) na madudu kibao ni sayansi ila wewe kwako dini ndo inaiba sana.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
Sayansi sio dini...elewa ...
 
Dhehebu la nini? yaani kuongeza kilinge kingine cha kulishana ideas za movies za Marvels na za Mazombie??

Ishi kwa upendo, jali watu, saidia wasio jiweza, epuka maovu, imetosha!
😂naelewa mkuu namwambia huyo anajisifia anajua mambo ya kiroho
 
Wewevumedanganywa makanisani ndiyo maana unaona makosa ila injili ya kweli mimi naijua na logic yake naijua
Lwiva namuita na SimbaMpole123 apitie pia hapa
Na kama utahisi kuna Mtu anauwezo wa kujibu Pia unaweza kumualika

Mkuu hizi contradiction kama ukiweza kuzijibu na kuonyesha Logic yake kama ulivyosema bhasi utakuwa Mkristo wa Kwanza Duniani kuzijibu...

na kama utajibu au yeyote atakayejibu nakaribisha hoja zake ziwe yakinifu zisizo na mihemko na matusi na kama ana swali anaweza kueleza pia...

haya nifatilie

Ntadeal na ukoo wa Yesu zipo Contradiction kibao sana naweza kutumia Siku hata Tatu naandika tu...

Sasa tuanze na Ukoo wa Yesu na hapa zipo nyingi ila ntadeal na chache

Ukoo wa Yesu umeandikwa katika Vitabu viwili vikubwa vya Injili cha kwanza Mathayo 1:1-16 na luka 3:23-38

sasa hapo nitakuomba ukavisome Maana hapa nitaelezea contradiction zake tu..
Sitaki kuingia kwenye zile contra mnazojibu jibu moja kuhusu Father lineage na Mother lineage leo niko Tofauti sana

Ok nitafanya kwa mtindo huu ntakuwa nauliza kwa mtindo wa swali halafu nakuonyesha Agano jipya lilivyosema halfu nakuonyesha uhalisia wake...

  • Nani ni alikuwa Baba wa Sheatieli?
    • ukisoma kwenye Mathayo inamtaja (Yekonia)(mathayo 1:12)
"Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli;"
  • Ukisoma katika Luka Baba wa Sheatieli wanataja ni Neri badala ya Yekonia (Luka 3:27)
wa Yoana, wa Resa, wa Zerubabeli, wa Shealtieli, wa Neri,
Which was the son of Joanna, which was the son of Rhesa, which was the son of Zorobabel, which was the son of Salathiel, which was the son of Neri,

Sasa hapo ndo utagundua kwamba Luka Alisema uongo na kama Luka kaweza kusema uongo katka mambo kadhaa je unaamini katika Injili yake yote ,Je ile dhana ya kuongozwa na Roho, Je roho alimdanganya Luka...?

Sasa Nani alikuwa Baba wa Sheatieli (Halisi)..

1 Mambo ya Nyakati 3:17-18


"Na wana wa Yekonia, huyo aliyechukuliwa mateka; wanawe Shealtieli, na Malkiramu, na Pedaya, na Shenazari, na Yekamia, na Hoshama, na Nedabia. "​

Nafikiri umeona Hapo....

  • Mtoto Yupi wa zerubabel Ambaye Ukoo wa Yesu unafuata Kutoka kwake?

  • Mathayo (Kwenye mathayo 1:13) alimtaja Abihudi
"Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori"

  • ila luka akasema hata sio yeye akatutajia Resa.. (Luka 3:27)
wa Yoana, wa Resa, wa Zerubabeli, wa Shealtieli, wa Neri,

Which was the son of Joanna, which was the son of Rhesa, which was the son of Zorobabel, which was the son of Salathiel, which was the son of Neri,​

Sasa Hapa Ndo kuna kituko mkuu Kwani si Abihudi wala Resa wanaotambulika katika Historia ya Uyahudi wala historia ya Israel kuwepo! ni watu hewa hawa hawajulikani kokote na biblia haiwatambui kama Watoto wa Zerubabeli...
Soma

1 Mambo ya Nyakati 3:19-20

"Na wana wa Pedaya; Zerubabeli, na Shimei; na wana wa Zerubabeli; Meshulamu na Hanania; na Shelomithi alikuwa umbu lao na Hashuba, na Oheli, na Berekia, na Hasadia, na Yushab-Hesedi, watu watano.

And the sons of Pedaiah were, Zerubbabel, and Shimei: and the sons of Zerubbabel; Meshullam, and Hananiah, and Shelomith their sister:

And Hashubah, and Ohel, and Berechiah, and Hasadiah, Jushabhesed, five."


Sasa kama ulivyoona hapo Zerubabel ana watoto watano il si Abihudi wala Resa walio miongoni mwa watoto wake Je Roho mtakatifu aliwadanganya Luka na Mathayo?


  • Nani alikuwa Baba wa Uzzia katika Ukoo wa Yesu?
    • Mathayo alisema Yoram (Mathayo 1:8)
Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia;

Je ni kweli Yoram? kwenye ukoo original agana la kale linapinga kuwa baba wa uzia sio Yoram bali baba yake aliitwa Amaziah..

2 Mambo ya Nyakati 26:1

Na watu wote wa Yuda wakamtwaa Uzia, naye alikuwa mwenye miaka kumi na sita, wakamfanya awe mfalme mahali pa Amazia babaye.
Then all the people of Judah took Uzziah, who was sixteen years old, and made him king in the room of his father Amaziah.


  • Nani alikuwa Baba wa Yekonia (Na hapa ndo kuna Siri kubwa sana mwenye masikio na Asikie)
    • mathayo anasema kuwa alikuwa anaitwa Yosia /Josia
Mathayo 1:11

Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.

Sasa ukienda kwenye Ukoo Halisi Agano la kale huyo Josia/Yosia sio baba wa Yekonia ila baba wa Yekonia ni Yohoyakim...

1 Mambo ya Nyakati 3:16

Na wana wa Yehoyakimu ni hawa; mwanawe Yekonia, na mwanawe Sedekia.
And the sons of Jehoiakim: Jeconiah his son, Zedekiah his son.​

unafikiri kwa nini walikwepa kuandika Baba halisi wa Yekonia Nitakupa Jibu na kama wangemuandika Basi ingemdisqualify Yesu kuwa Kiongozi wa wayahudi...(Tuendelee ili upate kunielewa zaidi)


Sasa kwanini hawakumuandika baba Halisi wa Yekonia na wakaweka baba Fake ambaye hayupo kabisa...


Kama wangeandika Baba wa Yekonia halisi Yehoyakim (Ambaye kiuhalisia Ndiye baba wa yesu halisi)

basi moja kwa hii Ingemdisqualify yesu Kuwa
Mfalme,Mwalimu wala mtawala ndani ya wayahudi wala Taifa lolote la Mungu!


kwanini

kwasababu Mungu alimlaani Yehoyakim Katika uzao (Ukoo) wa Daudi wote na kulaani kizazi chake kuwa hakuna kiongozi atakayetoka katika uzao wake...

Yeremia 36:30-31

Basi, BWANA aseme hivi, katika habari za Yehoyakimu, mfalme wa Yuda; Hatakuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Daudi; na mzoga wake utatupwa nje wakati wa mchana upigwe kwa hari, na wakati wa usiku upigwe kwa baridi. Nami nitamwadhibu yeye, na wazao wake, na watumishi wake, kwa sababu ya uovu wao, nami nitaleta juu yao, na juu ya wenyeji wa Yerusalemu, na juu ya watu wa Yuda, mabaya yote niliyoyatamka juu yao, lakini hawakukubali kusikiliza.

Therefore thus saith the LORD of Jehoiakim king of Judah; He shall have none to sit upon the throne of David: and his dead body shall be cast out in the day to the heat, and in the night to the frost.
And I will punish him and his seed and his servants for their iniquity; and I will bring upon them, and upon the inhabitants of Jerusalem, and upon the men of Judah, all the evil that I have pronounced against them; but they hearkened not.


Sasa nakaribisha kama utawza zijibu hizi hoja chache kati ya nyingi...
Na kwa kufikiria kwa Haraka tu kwamba kitabu chebye Contradiction kama hizi hlafu utaje kwamba kina ngubu mnayoita Roho mtakatifu Its A joke Right ?
 
Dhehebu la nini? yaani kuongeza kilinge kingine cha kulishana ideas za movies za Marvels na za Mazombie??

Ishi kwa upendo, jali watu, saidia wasio jiweza, epuka maovu, imetosha!
Hlafu ndo dini walioambiwa kwenye Biblia nashangaa wanataja Ukristo...

Yakobo 1:27
[27]Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.

Pure religion and undefiled before God and the Father is this, To visit the fatherless and widows in their affliction, and to keep himself unspotted from the world.
 
Why Mungu muweza yoooote, Allah aliyeumba kila kitu ashindwe kuwafanya watu tu waamini in Shia au Sunni na sio kuvurugana mpk kutoana macho? Je, hawa wote c wanakumia Kuran mnayoamini ni kitabu bora na kikishushwa na Allah?

Huko ndani ndani ndo hakufai kbs
Unaelewa historia ya Ireland? Kule wakatoliki na Anglikana walitoana macho. Si sawa na Shia na Suni? Kuna tofauti gani?
 
KILA MTU AENDELEE NA ANACHOAMINI

MIMI NAAMINI MUNGU YUPO NA ANAISHI

KAMA WEWE HUAMINI ENDELEA NA KUTOAMINI KWAKO MHIMU USISEME SISI TUNAOMWAMINI MUNGU NI WAJINGA
 
Back
Top Bottom