HAKI KWA WOTE
JF-Expert Member
- Nov 30, 2022
- 1,108
- 1,132
Wewe unaamini yesu aliletwa na wakoloni kwaajili ya waafrikana wajinga au ulimwengu wote?Maswali yako yote ni ya kitoto sana ila nitakujibu hivyo hivyo na utoto wako
1. Mshahara wa dhambi ni mauti, lakini ukimwamini Yesu hakuna mauti, utapata neema na rehema.
Dhambi zipo ili kulinda ustawi wa jamii
2. Ndiyo Yesu alifuta dhambi zote pale msalabani, ndiyo maana hatuna kafara tena za wanyama zaidi ya damu na Jina la Yesu
Vita, maradhi, umaskini, na ujinga ni mambo ya kibinadamu na Mungu amempa UWEZO binadamu wa kushughulika na haya yote.
3. MATABAKA yapo ili maisha yawezekane, bila MATABAKA hakuna maisha. Imagine kila mtu awe Tajiri nani atakubali kuajiriwa? Hakuna boss anaweza kufanya kazi zake mwenyewe. Hata vidole vya mikono yako mwenyewe havifanani ukubwa wake
4. Binadamu siyo dhaifu, udhaifu ni matokeo ya binadamu kutotumia akili yake sawa sawa.
5. Shetani hajamzidi nguvu binadamu, Shetani ni dhaifu sana mbele ya binadamu, tatizo binadamu hajuwi jinsi alivyo na nguvu nyingi
Kama ni ulimwengu wote kwanini kwingine asipelekwe kwa nguvu iwe Afrika tu?