Wewevumedanganywa makanisani ndiyo maana unaona makosa ila injili ya kweli mimi naijua na logic yake naijua
Lwiva namuita na
SimbaMpole123 apitie pia hapa
Na kama utahisi kuna Mtu anauwezo wa kujibu Pia unaweza kumualika
Mkuu hizi contradiction kama ukiweza kuzijibu na kuonyesha Logic yake kama ulivyosema bhasi utakuwa Mkristo wa Kwanza Duniani kuzijibu...
na kama utajibu au yeyote atakayejibu nakaribisha hoja zake ziwe yakinifu zisizo na mihemko na matusi na kama ana swali anaweza kueleza pia...
haya nifatilie
Ntadeal na ukoo wa Yesu zipo Contradiction kibao sana naweza kutumia Siku hata Tatu naandika tu...
Sasa tuanze na Ukoo wa Yesu na hapa zipo nyingi ila ntadeal na chache
Ukoo wa Yesu umeandikwa katika Vitabu viwili vikubwa vya Injili cha kwanza Mathayo 1:1-16 na luka 3:23-38
sasa hapo nitakuomba ukavisome Maana hapa nitaelezea contradiction zake tu..
Sitaki kuingia kwenye zile contra mnazojibu jibu moja kuhusu Father lineage na Mother lineage leo niko Tofauti sana
Ok nitafanya kwa mtindo huu ntakuwa nauliza kwa mtindo wa swali halafu nakuonyesha Agano jipya lilivyosema halfu nakuonyesha uhalisia wake...
- Nani ni alikuwa Baba wa Sheatieli?
- ukisoma kwenye Mathayo inamtaja (Yekonia)(mathayo 1:12)
"Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli;"
- Ukisoma katika Luka Baba wa Sheatieli wanataja ni Neri badala ya Yekonia (Luka 3:27)
wa Yoana, wa Resa, wa Zerubabeli, wa Shealtieli, wa Neri,
Which was the son of Joanna, which was the son of Rhesa, which was the son of Zorobabel, which was the son of Salathiel, which was the son of Neri,
Sasa hapo ndo utagundua kwamba Luka Alisema uongo na kama Luka kaweza kusema uongo katka mambo kadhaa je unaamini katika Injili yake yote ,Je ile dhana ya kuongozwa na Roho, Je roho alimdanganya Luka...?
Sasa Nani alikuwa Baba wa Sheatieli (Halisi)..
1 Mambo ya Nyakati 3:17-18
"Na wana wa Yekonia, huyo aliyechukuliwa mateka; wanawe Shealtieli, na Malkiramu, na Pedaya, na Shenazari, na Yekamia, na Hoshama, na Nedabia. "
Nafikiri umeona Hapo....
- Mtoto Yupi wa zerubabel Ambaye Ukoo wa Yesu unafuata Kutoka kwake?
- Mathayo (Kwenye mathayo 1:13) alimtaja Abihudi
"Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori"
- ila luka akasema hata sio yeye akatutajia Resa.. (Luka 3:27)
wa Yoana, wa Resa, wa Zerubabeli, wa Shealtieli, wa Neri,
Which was the son of Joanna, which was the son of Rhesa, which was the son of Zorobabel, which was the son of Salathiel, which was the son of Neri,
Sasa Hapa Ndo kuna kituko mkuu Kwani si Abihudi wala Resa wanaotambulika katika Historia ya Uyahudi wala historia ya Israel kuwepo! ni watu hewa hawa hawajulikani kokote na biblia haiwatambui kama Watoto wa Zerubabeli...
Soma
1 Mambo ya Nyakati 3:19-20
"Na wana wa Pedaya; Zerubabeli, na Shimei; na wana wa Zerubabeli; Meshulamu na Hanania; na Shelomithi alikuwa umbu lao na Hashuba, na Oheli, na Berekia, na Hasadia, na Yushab-Hesedi, watu watano.
And the sons of Pedaiah were, Zerubbabel, and Shimei: and the sons of Zerubbabel; Meshullam, and Hananiah, and Shelomith their sister:
And Hashubah, and Ohel, and Berechiah, and Hasadiah, Jushabhesed, five."
Sasa kama ulivyoona hapo Zerubabel ana watoto watano il
si Abihudi wala Resa walio miongoni mwa watoto wake Je Roho mtakatifu aliwadanganya Luka na Mathayo?
- Nani alikuwa Baba wa Uzzia katika Ukoo wa Yesu?
- Mathayo alisema Yoram (Mathayo 1:8)
Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia;
Je ni kweli Yoram? kwenye ukoo original agana la kale
linapinga kuwa baba wa uzia sio Yoram bali baba yake aliitwa Amaziah..
2 Mambo ya Nyakati 26:1
Na watu wote wa Yuda wakamtwaa Uzia, naye alikuwa mwenye miaka kumi na sita, wakamfanya awe mfalme mahali pa Amazia babaye.
Then all the people of Judah took Uzziah, who was sixteen years old, and made him king in the room of his father Amaziah.
- Nani alikuwa Baba wa Yekonia (Na hapa ndo kuna Siri kubwa sana mwenye masikio na Asikie)
- mathayo anasema kuwa alikuwa anaitwa Yosia /Josia
Mathayo 1:11
Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.
Sasa ukienda kwenye Ukoo Halisi Agano la kale huyo Josia/Yosia sio baba wa Yekonia ila baba wa Yekonia ni Yohoyakim...
1 Mambo ya Nyakati 3:16
Na wana wa Yehoyakimu ni hawa; mwanawe Yekonia, na mwanawe Sedekia.
And the sons of Jehoiakim: Jeconiah his son, Zedekiah his son.
unafikiri kwa nini walikwepa kuandika Baba halisi wa Yekonia Nitakupa Jibu na kama wangemuandika Basi ingemdisqualify Yesu kuwa Kiongozi wa wayahudi...(Tuendelee ili upate kunielewa zaidi)
Sasa kwanini hawakumuandika baba Halisi wa Yekonia na wakaweka baba Fake ambaye hayupo kabisa...
Kama wangeandika Baba wa Yekonia halisi Yehoyakim (Ambaye kiuhalisia Ndiye baba wa yesu halisi)
basi moja kwa hii Ingemdisqualify yesu Kuwa
Mfalme,Mwalimu wala mtawala ndani ya wayahudi wala Taifa lolote la Mungu!
kwanini
kwasababu Mungu alimlaani Yehoyakim Katika uzao (Ukoo) wa Daudi wote na kulaani kizazi chake kuwa hakuna kiongozi atakayetoka katika uzao wake...
Yeremia 36:30-31
Basi, BWANA aseme hivi, katika habari za Yehoyakimu, mfalme wa Yuda; Hatakuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Daudi; na mzoga wake utatupwa nje wakati wa mchana upigwe kwa hari, na wakati wa usiku upigwe kwa baridi. Nami nitamwadhibu yeye, na wazao wake, na watumishi wake, kwa sababu ya uovu wao, nami nitaleta juu yao, na juu ya wenyeji wa Yerusalemu, na juu ya watu wa Yuda, mabaya yote niliyoyatamka juu yao, lakini hawakukubali kusikiliza.
Therefore thus saith the LORD of Jehoiakim king of Judah; He shall have none to sit upon the throne of David: and his dead body shall be cast out in the day to the heat, and in the night to the frost.
And I will punish him and his seed and his servants for their iniquity; and I will bring upon them, and upon the inhabitants of Jerusalem, and upon the men of Judah, all the evil that I have pronounced against them; but they hearkened not.
Sasa nakaribisha kama utawza zijibu hizi hoja chache kati ya nyingi...
Na kwa kufikiria kwa Haraka tu kwamba kitabu chebye Contradiction kama hizi hlafu utaje kwamba kina ngubu mnayoita Roho mtakatifu Its A joke Right ?