Upo sahihi lakini suala la uvumbuzi ni suala mtambuka sana,..
Mfano kuna uwezekano nguvu za kiuchumi,kisiasa na kadhalika Kwa baadhi ya nchi ndiyo kunachochoea uvumbuzi na sio ishu ya kuwa theist au atheist.
Mfano Ulaya ambapo tunaamini ndyo kuna atheists wengi,..mbona nchi za Ulaya zisizo na nguvu kubwa kama Lithuania, Luxembourg,Poland, Croatia na kadhalika hazina uvumbuzi wowote remarkable ambao Dunia tunautambua,ukilinganisha na zile nchi zenye nguvu?
Huoni kwamba nchi hizo za Ulaya nilizotaja hapo tunakisia kwamba kuna atheists wengi lakini hakuna uvumbuzi wowote,...so Kwa mantiki hiyo possibility kubwa ni kwamba influence ya atheism kwenye uvumbuzi ni ndogo sana.