Unakubali kwamba, hata pale ambapo hujui jibu, inawezekana ukajua kwamba jibu fulani si sahihi?
Yani, jibu hujui. Lakini, hata kama hujui jibu, ukipewa jibu fulani, unaweza kujua kwamba, hata kama sijui jibu ni lipi, lakini najua jibu hili nililopewa si sahihi.
Unakubali hilo?
Yani, inawezekana mtu mwanamme wa miaka 30 leo, Juma, ambaye hamjui mama yake mzazi, akaletewa binti mchanga wa miezi 6 leo, Suzy, halafu akaambiwa kuwa, huyo binti mchanga wa miezi 6 leo ndiye mama yake mzazi Juma, mwanamme wa miaka 30 leo.
Je, Juma mwenye miaka 30 leo anaweza kujua kwamba huyu binti mchanga Suzy wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama yake mzazi, hata kama Juma hamjui mama yake mzazi ni nani?
SimbaMpole123 anakwambia kwamba, kutojua jibu si sababu ya kukubali jibu lolote.
Juma, mwenye miaka 30, hata kama hamjui mama yake mzazi, akiletewa binti wa miezi 6, akaambiwa huyo binti mchanga ndiye mama yake mzazi, anaweza kujua hili jambo si kweli, bila hata ya Juma kumjua mama yake mzazi ni nani.
Kwa sababu Juma anajua kwamba mama yake mzazi ni lazima awe mkubwa kuliko yeye Juma kwa miaka ya kutosha kumzaa, na huyo binti wa miezi 6 hajafikisha sharti hilo.
So, kutokujua jibu sahihi hakukulazimishi ukubali jibu lolote unalopewa, unaweza kuwa hujui jibu sahihi, lakini una principle ya kukuonesha jibu fulani si sahihi na kukuongoza kwenda kwenye jibu sahihi kwa elimination method.