Yani mimi nitegemee kufundishwa na Kiranga jambo pana kama hili na nkamuelewa just simple tu ?
Mnalazimisha tuelewe tu ?? Kama wewe unaweza ukafundishwa na yeye ni sawa upo sahihi.
Mnatumia mazao ya fikra za watu wengine kuwa ndio fikra zenu ( Ninyi ni watumwa wa hizi elimu ) zimewafunga msifikiri nje ya elimu mlizozipata.
Mimi namuamini Mungu, Na nkupe tu siri imenifanya kuwa na uwezo binafsi wa kuchimba mambo mengine mengi zaidi, ambayo mengine napata majibu ya hiki mnachokiita science, kwa maana hiyo kwa kutumia ufikiri wangu binafsi napata majibu ya kuhusu mambo mbali mbali yanayoshahabiana na hao mnaowaamini nyinyi ( science/scientists )...Utofauti Mimi nipo huru kifikra, nyinyi hampo huru.
Kwa kuongezea, Mimi namuamini Mungu kwa namna yangu peke yangu.
Hujakanusha mantiki niliyoiandika.
Kumuamini Mungu unaruhusiwa, hiyo ni haki yako ya kikatiba.
Katiba ya Tanzania ina kipengele cha uhuru wa kuabudu ama kuchagua kutoabudu. Siwezi na sitaki kukuingilia kwenye uhuru huu kama mimi nisivyotaka uniingilie.
Katika Universal Declaration of Human Rights ya UN, una haki ya kuamini Mungu utakavyo. Hili limepitishwa na Umoja wa Mataifa tangu December 10 1948.
Hili hata mimi nisiyeamini Mungu, nitatetea haki yako ya kuamini Mungu utakavyo.
Kuamini Mungu si issue hapa, after all kuamini Mungu ni issue personal wala sielewi kwa nini ifanyiwe mjadala hapa JF.
Jambo linalojadilika JF ni kutafuta facts, ukweli, si imani tu, je, Mungu yupo kweli?
Ukweli ni zaidi ya imani, kwa sababu, kwenye imani, unaweza kuamini hata uongo. Ukweli upo tu, ukiuamini, usipouamini, upo tu.
Naomba tutenganishe habari za imani tu, na habari za facts.
Hizi habari za Mungu kuwapo ni fact Mungu yupo? ni ukweli Mungu yupo? Au ni imani tu?
Mpaka sasa, hakuna aliyethibitisha Mungu yupo.
Hakuna aliyeweza kuiweka habari ya uwepo wa Mungu kwa misingi ya facts, kwa kuiondoa kwenye imani tupu, kwa kutumia mantiki ya kutafuta ukweli.
Na zaidi, ukizichambua habari za kuwepo kwa huyo Mungu, unaona contradictions na inconsistencies zinazoonesha Mungu huyo hayupo, Mungu huyo ni wa hadithi za kiimani tu zilizotungwa na watu.
Ndiyo maana mpaka leo hakuna mtu aliyethibitisha Mungu huyo yupo.
Hayupo, hivyo huwezi kuthibitisha kwamba yupo.
Ukibisha, thibitisha Mungu yupo.