Kila mtu Hujaribiwa na Tama yake mwenyewe..
Soma Yakobo..
Na kingine mkuu inawezaje uchuje Mbu na Umeze Ngamia (Yesu pia aliwahi kuwambia hili)
Yaani uchukue baadhi ya mafundisho useme haya yako sawa (Kama hapo umetaja Kujaribiwa kwa yesu ambapo papo kwenye Vitabu hivyo vilivyopotolewa)
Kuna wakati inahitaji kujitoa akili ili kutetea...
Soma biblia Yeremia 8:8
"Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo."
soma biblia Mathayo 23:24
[24]Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia...
Yesu kujaribiwa...nafikiri soma Refference hapa.chini
Yesu alijaribiwa na Tamaa yake mwenyewe baada ya kushinda siku 40 Bila kula skaona njaaa hiyo njaa ndo iliyomjaribu..
Mathayo 4:2-3
Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.
Ukisoma katika Yakobo utaunganisha Dot mwenyewe
Yakobo 1:13-16
Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike.
Sasa malizia na Hii
1 Yohana 2:16
Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.