Hoja zako ni nzuri lakini hazijashiba. By the way, kama ni msomaji mzuri utagundua kuwa science ipo katikati, yaani haiwezi kujibu 'before' and 'after ' questions. Kwahiyo science as science ni ukweli mtupu but ina "mzazi" au nguvu iliyojificha beyond science, ambayo baadhi ya scientists wameieleza kama SUPER NATURAL POWER ambayo ndo asili ya vyote ikiwemo na science yenyewe. Hii nguvu imeleta science na maarifa mengine ili tuweze kujitambua na ku survive. Science haiwezi kueleza chanzo cha kiumbe, na hili liko wazi kwani mpaka leo "origin of pre-existing cells or parent cells" ambazo ndio msingi wa maisha ya kiumbe yeyote hai, haijulikani ni nini. Pia science haiwezi kujibu maisha baada ya kifo inakuwaje. Haiwezi kueleza kwanini ulizaliwa, umekuja duniani kufanya nini, kwanini utakufa na utaenda wapi(soul/ufahamu ulionao) baada ya kufa. Kusema tu kwamba utakufa na utaoza hakutengenezi logic yoyote ya kwanini ulizaliwa. Kwamba ulizaliwa ili ufe au?. DUNIA NA MAISHA VINA CHANZO, LAZIMA VINA CHANZO. Hii awareness tuliyonayo sasa lazima kuna namna itaendelea hata baada ya kufa, otherwise binadamu hana thamani yoyote, ni sawa na jiwe tu. Wewe kama msomi sasa ndio unatakiwa kufanya research na kujuwa chanzo cha yote ni nini hasa, maana si lazima kuamini kuwa ni Mungu. Albert Einstein wakati anakaribia kufariki alisema "I want to know the thoughts of GOD", Aliamini kuna namna. Hoja ya Umasikini wetu inatokana na ufinyu wetu wa maarifa, kusingizia dini ni kutafuta excuse tu, kwani hata kukesha kanisani tukiomba utajiri ni moja ya ishara kubwa kuwa tuna changamoto ya maarifa yote ya kidunia (formal) na ki Mungu (spiritual). Kama mnataka mali mtaipata shambani (ie KAZI, si lazima kilimo) na si kanisani. Dini ni hatima(Fate). Mafundisho ya Dini yanafanya maisha yawe na thamani. Kama una waheshimu Baba na Mama na kuwaona kama ni viumbe vya tofauti ni kwasababu ya Mafundisho ya Dini, otherwise wangekuwa kama Maembe dodo au Mafenesi tu, unaweza hata kuwatafuna ukipenda[emoji3] maana science haielezi umuhimu wa wazazi.