Unaporusharusha hilo neno sayansi, unamaanisha nini? Jibu swali. Mimi ndiye nimeanza kukuuliza wewe.
Ikiwa.
1. Kitu kinaweza kuonekana kipo, na kikawa hakipo - Mirage jangwani.
2. Kitu kinaweza kuonekana kipo, na kikawa kipo - unavyojiona kwenye kioo.
3. Kitu kinaweza kuwa hakionekani, lakini kipo - Mimi hunioni, lakini nipo.
4. Kitu kinaweza kuwa hakionekani, na hakipo - Pembetatu ambayo ni duara katika Euclidean geometry.
Kwa nini habari nzima ya kuonekana iwe muhimu?
Kwa nini habari ya kuonekana iwe muhimu ikiwa kuonekana au kutoonekana haku prove lolote kwenye swali la kitu kipo au hakipo?