Dini si imani, Mimi mkristo nimekubali kuoa ndoa ya kiislamu, ndoa ya kikristo inampa kiburi mwanamke na ni ngumu kusuluhisha matatizo

We nae unadeka sana. Sasa mwanamke anakusumbua vipi kichwa chako hadi unakosa direction kiasi hiki?

Haya ndio matokeo ya kuwajaza watoto wa kiume ujinga vichwani halafu wanakutana na vitu tofauti.

Unakuta mzazi especially akina mama,anamwambia mtoto wake wa kiume, "Mwanamke hapigwi" "usije ukamfokea mtoto wa watu ongea nae kwa upole","mpende mkeo kuliko chochote kama unavyonipenda","mwanamke anapewa pesa usije ukamnyima pesa" na upuuzi mwengineo.

Hii inawajenga vijana wa kiume na mentality ya upunda au ukondoo kiasi kwamba wanashindwa muwajibisha mwanamke kwa uovu wake pale anapofanya.

Mwanamke anatoka nje ya ndoa ukija uliza eti sababu ulikuwa hautengi muda wa kukaa na mimi nikawa mpweke sana. Hapo mtu alikuwa nje kupambana na maisha ili kuleta pesa ndani ya familia.

So ni kaina fulani ka uzembe wa kifikra kakujitakia. Unajifunga kwa fikra zako mwenyewe. Kwa Kila mwanamke anaeondoka kuna wanawake 1000 zaidi wa kuja kuwa nao katika ngazi ya kata unayoishi hapo hatujaenda ngazi ya wilaya, mkoa, na taifa na Dunia.

Why sasa ukae ukisumbuana na mtu ambaye ukiuliza anakupa kiasi gani kwa mwezi zaidi ya bills unakuta ni zero. Mimi ninakuwa na mawazo sana gari yangu ikiwa inahitajika kufanyiwa service kuliko mwanamke akiwa analazimisha kupewa pesa kwa kauli zao zile "nataka unihudumie" kama mgonjwa au mzee asiyejiweza. Ufala tu.

Acha kupoteza muda na kujiweka tegemezi na mwanamke m'moja, mradi wewe hauna changamoto basi, tafuta mwingine life isonge.
 
Pole sana kijana kwanza umri wako bado, hata hivyo ndoa Haina dini, iwe ya kikristo, kiislam, kimila, kihindu n. k bado tu itakuwa na changamoto kwa sababu wanadamu ni walewale ni nani akiyekudanganya kuwa ndoa za kiisalam hazina changamoto?
 
Aliyesema mahakama Ni mambo ya kijeni, napinga, Ni yetu wanachi na tumeiunda wenyewe, je Bible ulishirikishwa? Uliletewa na kukariri tu! Ukizingatia sana hizo Imani za kizungu utakufa masikini na Bible yako mikononi. Aliyefanikiwa na Bible mikononi Ni maujanja tu!!!
 
Umebadili dini na kuwa muislamu au wewe bado ni mkristu ila umefunga ndoa ya kislamu?
 
Eti nimeoa kiislam ila mimi kiimani ni mkristo.

Acha kuifariji jamii mkuu, mimi nitaoa kikristo na dini haitanifunga kuachana kama akisaliti na mali zangu nilizotolea jasho zitabaki kua zangu daima.
 
Umri wako 28 bado unasitasita kuoa kutokana na urasimu (bureaucracy) huko uliko.
Fanya maamuzi kiume , oa huyo mke wa dini nyingine au wa dini yako ndoa ya kiserikali. Hakuna urasimu, gharama ndogo, hakuna unyanyapaa. Mengine utashauriwa jinsi ya kutengeneza. Wangapi wameamua hivyo na kuondokana na kuteswa na msongo wa mawazo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…