Dini ya Uislam iliwezaje kuenea kwa wingi "Sub Saharan Africa" ilhali waarabu hawakuwa na makoloni huko? Ni biashara pekee ama kuna njia nyingine?

Uislamu una sheria zake. Kutamka aya au hadithi au kutamka Allahu Akbar au kuvaa mavazi ambayo waislam wanayavaa kulingana na imani yao, au kuyafanya yote kwa pamoja haina maana wewe ni muislam.

Kuwa muislam ni kukubali taratibu zote na miongozo yote aliyokuja nayo Mtume. Uislam unasema jishikize kwenye dini kwa miguu yote miwili. Si mguu mmoja ndani na mguu mwengine nje.

Uislam kwa kila kitendo au hali au mazingira mtu awepo uislam una marejeleo ya nini cha kufanya. Ikiwa akitokea mtu hata kama ni muislam akafanya mambo yaliyo nje na marejeleo ya uislam huyo mtu alichokifanya ni utaratibu wake na si utratibu wa uislam na ndivyo vinavyofanywa na hivi vikundi vya kigaidi.

Na hii hali ni ngumu kuitambua iwe kwa waislam na kwa wasio waislam. Mtu pekee anayeweza kung'amua hii hali ni yule aliyekuwa na elimu ya dini ya kiislam. Uislam haulazimishi mtu kusilimu. Bali uislam unalazimisha kuusiana mema na kukatazana mabaya.

Vita ndani ya Uislam zimegawanywa katika makundi mawili. (1) Vita kubwa na (2) vita ndogo. Vita kubwa ni jihadi ya nafsi. Jihadi ya mtu kupambana na matamanio yake, kuushinda moyo wake na hisia zake dhidi ya maovu na kupambana na wasiwasi na viamsho vyote shetani anavichochea kupitia kwenye moyo, hisia na akili ya mtu. Hii vita mwisho wake ni pale mtu anapokufa.

Vita ndogo ndiyo vita ambayo wengi wao katika watu imma kwa makusudi au kwa kutojuwa huwa wananasibisha kuwa ndiyo uhakika wa Uislam. Utakubaliana nami ikiwa utasoma historia ya uislam kipindi cha Mtume Muhammad (s.a.w). Waislam walikuwa wanaishi kwenye nchi yao ya Makka. Ikapitishwa amri na mabwana wakubwa wa Makka kuwa ni kosa kubwa mtu kuwa Muislam na ni kosa kubwa kufanya yanayofanywa na Uislam. Gharama ya hili kosa ni kuuliwa. Waislam wakawa wanajificha.

Waislam wakahama wakaenda kuomba hifadhi kwa Mfalme wa Ethiopia ambae ni Mkristo. Bado wakafuatwa Ethiopia ili kuharibiwa diplomasia yao na huyo Mfalme. Wakafukuzwa kwenye nchi yao ya Makka na kufilisiwa mali zao zote. Eneo walilofikia ikatangazwa amri hakuna yeyote kufanya na miamala ya aina yoyote. Vyakula vikazuiwa kuingia kwao wengi walikufa kwa njaa. Watu wa kutoka nchi ya Madina wakaamua kuwanusuru na kuwakaribisha madina. Mabwana wakubwa wa Makka kusikia hayo wakaenda Madina kuwaletea tena shida na wakatangaziwa vita.

Kwa mazingira ya namna hayo unafikiri nini kifanyike? Ndipo zikashuka aya za Qur'an zinasema wameruhusiwa kupigana kwa wale wanaodhulumiwa. Aya za vita ndipo ziliposhuka hapo! Lakini zilishuka kwa masharti ya kuwa; Wasiharibu vyanzo vya maji na mazingira, wasiue wasiyohusika, wasiue watoto n.k na wasichupe mipaka bali wapigane kwa ile hali ambayo ya kutetea uhuru wao wa dini yao, nchi yao na kulinda damu yao isimwagwe hovyo!

Huo ndiyo munasaba wa aya za kivita ulivyoshuka. Sasa fananisha madai ya hivyo vikundi vya kigaidi kusimamisha vita na sababu ambayo Mtume na Maswahaba iliyopelekea kupigana vita. Na kama haujui vikundi vya kigaidi mfano nchini Syria vimeua wana wazuoni wengi sana wa kiislam na wamelipua na kujitoa muhanga kimabomu mpaka misikitini na kuwaua Masheikh wa kisunni wal Jamaa wengi na wengine wamewachinja.

Mfano Sheikh buuti ameuliwa akiwa msikitini anatoa mawaidha. Sheikh bouti aliwaambia wazi wanachokifanya si uislam. Akauliwa yeye na mjuu wake na wengineo msikitini kwa shambulio la mtu kujitoa mhanga kwa kujilipua kwa bomu. Na aliyefanya hayo mauaji ni ISIS.

Kingine, kwenye Qur an Mkiristo hakuitwa Kafir. Bali ameitwa Mnaswara na sehemu nyengine ametajwa kwa jina la ahlul kitab! Ikiwa na maana watu waliyopewa vitabu vya Mungu huko nyuma. Si mkristo pekee na Myahudi pia ameitwa hivyo! Kwa hiyo ni uelewa mbaya wa maandiko kwa baadhi ya watu au wanasababu zao ambazo wanatumia mgongo wa dini ili kufanya purukishani zao.

Wanayofanya ISIS, BOKO HARAM, AL QAEDA, AL SHABBAB na wengineo si mambo yanayoruhusiwa kwenye Uislam. Wamelipua mpaka makaburi ya Mitume ya zama ya nyuma kwa mabomu. Mfano kaburi la Nabii Yunus A.S wamelilipua majamaa!
 
Umefafanua sana mkuu. Hakika unajua
 
Hakuna hata chembe ya udini mkuu lakini watu wanaleta udini (mambo ya Yesu na mtume Mohamad)
Udini upo,Mkuu
Haiwezekani Nchi yenye takriban nusu Waislam nusu Wakristo lakini Baraza la Mawaziri ni Wakristo Watupu..

Je raisi akiwa Muislam nae afanye hivyo hivyo,Wakristo watasemaje?

Busara ni kitu kizuri katika kuuondoa mashaka katika nyoyo za Unaowaongoza..

Hivi tuseme, Waislam hawajasoma,Wavivu,au wako kidogo nchini?

Lakini hata iwe hivyo raisi alitakiwa atumie Busara kidogo,alitakiwa afanye baraza la Mawaziri lenye uwiano wa Wakristo na dini Nyengine..

Tafakari
 
Unaongelea nchi gani mkuu?...
 
Ni kweli
kuna yale ma caravan routes and trades.

Hata mtume Muhammad alikuwa trader wa Caravan kabla hajawa mtume..Although alipokuwa mtume na kupata wafuasi alianza kuvizia hawa traders na kuwapokonya mali.
ushaidi upi? miaka hio caravan routes lazima maama uasafiri ulikuwa wa wanyama ngamia wanakatiza jangwa kwa jangwa.wewe umesoma historia kuwa prophet alikua anafanya beshara ni kweli na njia ni hio hio ilikuwa misafara hakuna njia nyingine.mpka alivofika basra ilipo iraki akakutana na padri aliyeona dalil na alama zote za mtume yuleee wa mwisho aliyekuwa akisubiriwa na walokuwa wakijua jambo hili na jewish.padri yule kwa kujua roho za wahayuhd akamfadhilisha sana mjonba wake amrudishe huyu kijana maana ilikua maaajbu tu wingu linaenda sambamba na kichwa chake jua halimpati in short miujiza sana.
kuhusu kuvamia misafara mkuu ni kweli historia ipo ila nadhan umeilewa vibaya .
waliteka msafara mmoja in specific kulipiza kisas cha wao pia kutekwa na wala wakawa hawakuupata msafara wenyewe ila vikafumuka vita eneo la badr askar 300 kwa jesh zaid ya maelfu na waislam walishinda.usipindishe pundishe haina haja huwez kufaulu leo,jana wlaa kesho ila iseme kama ilivyo sawa.
 
Umeanza kama unanipinga halafu maelezo yako yanakubaliana namimi...zingine zote ni ngonjera.
wewe unaita kulipiza kisasi mimi naita wizi mwingine ataita kulipiza kisasi kwa njia ya wizi poteto potato

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Islam is a religion of peace; if you dont accept I kill you.
 
Walitumia biashara ya utumwa.na pembe za ndovu kueneza uislam ukiwa muislam hukamatwi utumwa. Afterall ukoloni siyo njia pekee ya kueneza dini ya mtu. Waarabu ndiyo wakoloni na mabeberu wa muda mrefu Afrika kuliko wazungu, hapo Zanzibar kabla ya mapinduzi kiongozi wa visiwa alikuwa mbantu au mwarabu? Mwarabu masultani toka Oman wakoloni tu kama wazungu. Wajamaica hawakuwa na makoloni Africa lakini dini ya urastafari imeenea toka Mwakaleli Mbeya hadi Kibosho Moshi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…