Msae-Marangu
Member
- May 28, 2023
- 70
- 109
Sasa si bora wewe Mkatoliki uliambiwa utoe hiyo 25,000/=Salaam!
Mimi nafikirishwa sana na hizi dini za leo za kizungu, binafsi mimi ni mkatoliki lakini naona uchafu uchafu tu.
Hawa wakristo tuwape muda tu hii karne ya 21 ikipita najua hatuta kuwepo wengi humu ila ukristo utakuja kuwa kituko cha karne (22) kutokana na yale tunayo yaamini viongozi wetu wanatuletea mapicha picha ya kutufanya sisi ni misukule yao.
Nimejiuliza swali moja tu mimi kama baba mlezi mtoto alifika hatua ya kipaimara, nikaambiwa eti nitoe shilingi elfu 25,000 ili mtoto akae pamoja na askofu. Yaani yeye askofu anakuja kukaa na watoto hiyo siku ya kipaimara wanakula pale sahani ya wali na soda na stori mbili tatu afu imeisha hiyo. Mimi kipaimara changu hakikuwa hivi sasa hii elfu 25 ni ya nini? Mamichango ya zaka ni lundo.
Kidogo nisahau kuuliza hili swali?
Hivi wakuu na huko kwenye uislamu ni hivi hivi?
Mimi Mlutheri (KKKT), niliambiwa mwanangu atoe 70,000/= ili aweze kupata kipaimara mwaka Jana, nilishangaa Sana!!!
Nikahoji hiyo elfu sabini yanini?! Kwani kupata kipaimara ni biashara?! Wakajibu atapewa biblia Kama zawadi?!
Sawa hatukatai kupewa biblia, lakini hiyo ndio bei ya biblia?! Na Kama mzazi hana hiyo hela?! Ndio kusema mtoto hapewi kipaimara?! Kiukweli haya madhehebu yetu hakika yamegeuka sehemu ya kuchuma hela Sana Tena kwa lazima, huna hela hupati huduma ya kiroho,
NB:
Watu hawakatai kutoa sadaka, michango n.k. lakini isiwe too much, au upigaji kiasi hicho ,Tena kwa masharti na lazima , hutoi hupatiwi huduma ya kiroho!!
Inasikitisha Sana kiukweli!!
Tunakoelekea huko, sijui,,,!!!
Mungu tu atusaidie!!