Dini zimefanywa biashara, michango imekuwa mingi

Sasa si bora wewe Mkatoliki uliambiwa utoe hiyo 25,000/=

Mimi Mlutheri (KKKT), niliambiwa mwanangu atoe 70,000/= ili aweze kupata kipaimara mwaka Jana, nilishangaa Sana!!!

Nikahoji hiyo elfu sabini yanini?! Kwani kupata kipaimara ni biashara?! Wakajibu atapewa biblia Kama zawadi?!

Sawa hatukatai kupewa biblia, lakini hiyo ndio bei ya biblia?! Na Kama mzazi hana hiyo hela?! Ndio kusema mtoto hapewi kipaimara?! Kiukweli haya madhehebu yetu hakika yamegeuka sehemu ya kuchuma hela Sana Tena kwa lazima, huna hela hupati huduma ya kiroho,

NB:

Watu hawakatai kutoa sadaka, michango n.k. lakini isiwe too much, au upigaji kiasi hicho ,Tena kwa masharti na lazima , hutoi hupatiwi huduma ya kiroho!!

Inasikitisha Sana kiukweli!!

Tunakoelekea huko, sijui,,,!!!

Mungu tu atusaidie!!
 
Siri kubwa ya maarifa imejificha hapa.
Kutokana na uelewa mdogo wanawapuuza wenye uhitaji kama mayatima,walemavu/maskini wanampelekea mtu mwenye maisha mazuri anayetembelea gari ya kifahari wakati huo wao wanatembea kwa miguu

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
muhimu sana, maana unaweza mpa jambazi kama hakuna umuhimu kwenye utoaji
Yes ukitoa sehemu isiyo sahihi inakuwa useless,ukitoa kwa watu wenye uhitaji kama mayatima,walemavu/maskini na mafukara wasiojiweza hapo inakuwa umepatia sehemu sahihi na Mungu anakubariki.
Ila ukienda kutoa kwa mtu anayetembelea gari ya milioni 60 na anamiliki nyumba ya milioni 200 au 300 akala yeye binafsi au na familia yake hapo ni sawasawa umeitupa tu.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Inategemea umempa nani

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
Safi kabisa,

Siku hizi nimeona heri hata nitoe kwa yatima, wagonjwa mahospitalini, masikini wenye uhitaji mbalimbali, wajane maskini na hata wafungwa magerezani,,,!!

Kuliko hawa wanaotoza hela nyingi sana huku wao wanaenda kujenga majumba ya kifahari na kununua magari ya gharama kubwaaaa!!

Bora tuwape masikini na wenye uhitaji akya Mungu!!
 
Haswa hivi ndivyo inavyotakiwa ila watu wanafanya kinyume kutokana na uelewa mdogo

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
lakini mtu kumiliki nyumba na kuendesha gari la samani sio tatizo.. je ? anachokusanya kinaenda wapi ... Tujue pia wahitaji wengine hukimbilia huko.. ni muhimu kuongozwa na mtu wako wa ndani ujue unapotoa ni sahihi au chenga chenga
 
Ni dokta wa moyo ama
 
Ukisikia sadaka ndio hii sasa
Kila leo tunawaambia watu badala ya kuwapa masikini walio jirani yeye mbio anapeleka kwa jamaa ambae anamlazimisha atoe kila mwezi, sasa sijui kwa mwaka mnatoa ngapi na marejesho ni nini?

Masikini akiomba anapitwa kama hawamuoni huku wakiwa wamependeza wanazipeleka wanakojua
 
lakini mtu kumiliki nyumba na kuendesha gari la samani sio tatizo.. je ? anachokusanya kinaenda wapi ... Tujue pia wahitaji wengine hukimbilia huko.. ni muhimu kuongozwa na mtu wako wa ndani ujue unapotoa ni sahihi au chenga chenga
Huo uwezo wa kuhoji au uwezo wa kudadisi walio wengi ndio hawana.
Mimi nikienda sehemu ya ibada ukiitishwa mchango lazima nisikilize kwa makini na nidadisi huo mchango ni kwa ajili ya shughuli gani?kwa mfano kama ukiniambia ni kwa ajili ya ujenzi basi ni lazima nicheki je kuna ukuta umebomoka?Au kuna paa limeezuliwa?Au kuna finishing inatakiwa kufanyika na ili nishawishike zaidi inabidi niwaone mafundi wako saiti tayari

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Sema haya mambo ya kutoa yana mambo mengi sana
 
Ukiwa na ufahamu na maandiko katika kitabu unakuwa huru kwasababu utakuwa unajua halali na batili hautayumbishwa haya makando kando yapo hata ktk baadhi ya Mashekh japo si kwa wingi

Lakini ukweli unabaki kama waumini tukiwa na elimu hatuibiwi tunajua huyu katuchota huyu anasema kweli
 
Uzuri sadaka sio Kodi kwamba ni lazima utoe. Kazi kwako na Iman yako. Jamn watanzania tujaribu kuwa serious na Mambo ya msingi. Hv jambo la hiyari ni jambo la kuja kulalamikia huku. Kutoa sadaka na michango ni hiyari Yako huna haja ya kuja kulalamikia huku coz sio sheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…