Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Wewe unaposikia nabii Issa unadhani ni nani?Kwa hiyo unataka kusema YESU kwa kiarabu anaitwaje?
Raha ya dini uzijue zote usiishie kwenye ukafir.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe unaposikia nabii Issa unadhani ni nani?Kwa hiyo unataka kusema YESU kwa kiarabu anaitwaje?
Sema alikuwa wa wapi, lazima ana kwao ukiacha mbinguni.Yesu hakuwa typically mzungu ila hakuwa pia muarabu. Mbona ipo wazi ukifungua Bible agano jipya unaoneshwa ukoo wake ulivyoanza hadi kufikia kwake "mfalme wa uyahudi"
Yesu siyo muarabu ni Myahudi. Uislamu ni agano la kale la Biblia. Uislamu ulianzishwa na mapadre watano wa kikatoliki walioasi kanisa katoliki miaka 500 baada ya Kristo.Kwanza ukiristu haukuanza ulaya, Yesu hakuwa mzungu alikuwa mwarabu yaani alitoka mashariki ya kati na maeneo yake ya kujidai yalikuwa uarabuni yaani Misri, Irani, Iraki, Jordani, Palestina na Israeli.
Uisilamu ulianzia mashariki ya kati hukohuko ulikoanzia ukirisitu, kinacho tuchanganya sisi ni majina bila kuyachambua vizuri, majina ya dini zote mbili ni ya kiarabu ila yametafsiriwa kwenye lugha nyingine, majina watumiayo wakiristu wa nchi zilizotawaliwa na mwingereza yanatamkwa tifauti kwenye nchi zilizitawaliwa na mfaransa au mspaniola,
Sasa haya majina tunayoyatumia ndiyo yanatufanya tudhani kuwa ukirisitu ulianzia Landani au Parisi, hapana, hakuna dini iliyoanzia ulaya au marekani, tusichanganye na madhehebu tukadhani ni dini.
Nabii Issa na Yesu Kristo ni watu wawili tofauti kabisa kwa ushahidi wa Quran tukufu na Biblia takatifuWewe unaposikia nabii Issa unadhani ni nani?
Raha ya dini uzijue zote usiishie kwenye ukafir.
Na ndio wanaongoza kwa majanga ya asili na umasikini
Na huo ukweli mchungu ukiusema unatengwa kundini. Wao wakisemana wenyewe kwa wenyewe unasikia wanameguka EAGT na TAG, mara Kanisa la Kiinjili la Moravian Tanzania KKMT na Kanisa la Moravian Tanzania KMT.Ukweli mchungu mkuu.. dini zina ubaguzi sana ndani yake za wenyewe kwa wenyewe mkuu.. hili nimelitoa katika uvungu wa moyo wangu.. ila bado linaniuma sana
Papa wa 266 na Makaisari walikuwa 12.Hizi dini nahisi hazitufai. Haiwezekani leo tuna papa sijui wa ngapi harafu asiwemo mwafrika hata mumoja
Hasa kwenye sadaka.Dini tumeletewa zote
Lakini kwenye masuala ya dini tunaishia kutoana
Ngeo wafrika
Ova
Dini na madhehebu yana wamiliki wake, sio mungu. RC wamiliki wako Italia, Anglican wako UK, Lutheran wako Ujerumani, SDA wako USA, Shia na Suni wako Uarabuni, Budha wako India, Shinto wako Japan, nk.
Viongozi wa hizo dini popote walipo Duniani lazima wa report ama kuchaguliwa na kua endorsed na hao viongozi wao kutoka makao makuu.
Sisi huku Afrika kazi ni kupokea tu hizi dini, kupumbaza watu na kuwafanya waendelee kua masikini kwa kuwatoza michango isiyo na kichwa wala miguu kwa jina la zaka, sadaka na michango mingine, kiasi kidogo kinabakia hapa kikubwa wanapelekewa wamiliki wa kanisa huko walipo.
Nawapongeza hawa kina Kakobe, Gwajima, Mwamposa wao kuanzisha makanisa yao na wao kua wamiliki na kula hizo hela. Watu mnachanganye hela Tanzania anapelekewa papa italia kula? Wakila kina Mwamposa maneno ila anazokula Papa hazisemwi.
Very nice piece, worth publishing in a journal.Dini ya muafrika iliyowekwa kwenye records vizuri ni voodoo ya Haiti….
Quoting the link “
For many in the West, Voodoo invokes images of animal sacrifices, magical dolls and chanted spells.
But Voodoo – as practiced in Haiti and by the black diaspora in the United States, South America and Africa – is a religion based on ancestral spirits and patron saints.
Known as “Vodou” in Haiti, the religion has also served as a form of resistance against the French colonial empire.
And unlike many mainstream representations around magic and rituals, scholars have shown how Voodoo serves as a form of health care system by providing religious healing.
A religion born out of struggle
Haitian Vodou was born from the blending of Catholicism, Western and Central African spirituality.
In addition, scholars assert that the religion was influenced by escaped slaveswho wanted to inspire rebellions under a common spiritual identity.
Historian C.L.R. James described Voodoo as a “medium of the conspiracy,” meaning Voodoo was at the center of inciting the 1791 revolution in Haiti against slavery and colonialism.
In later years – from 1835 to 1987 – the Haitian government banned Voodoo under laws that prohibited ritualistic practices. However, as historian Kate Ramsey points out, the laws were almost impossible for the Haitian government to implement. As early as the 19th century, Voodoo had already become a dominant belief system even influencing elite culture – even if secretly.”
What is Haitian Voodoo?
Ni kweli mkuu.Kwanza ukiristu haukuanza ulaya, Yesu hakuwa mzungu alikuwa mwarabu yaani alitoka mashariki ya kati na maeneo yake ya kujidai yalikuwa uarabuni yaani Misri, Irani, Iraki, Jordani, Palestina na Israeli.
Uisilamu ulianzia mashariki ya kati hukohuko ulikoanzia ukirisitu, kinacho tuchanganya sisi ni majina bila kuyachambua vizuri, majina ya dini zote mbili ni ya kiarabu ila yametafsiriwa kwenye lugha nyingine, majina watumiayo wakiristu wa nchi zilizotawaliwa na mwingereza yanatamkwa tifauti kwenye nchi zilizitawaliwa na mfaransa au mspaniola,
Sasa haya majina tunayoyatumia ndiyo yanatufanya tudhani kuwa ukirisitu ulianzia Landani au Parisi, hapana, hakuna dini iliyoanzia ulaya au marekani, tusichanganye na madhehebu tukadhani ni dini.
Mimi ninaamini Mungu kwa upeo wangu, sio kwa kupitia dini yeyote..Tunaweza tukawa tofauti kwa rangi zetu na asili zetu.
Ila Mungu wetu ni Mmoja
nadhani sisi waafrika ndo tuna ubaguzi sisi wote ni binadamu hatutakiwi kubaguana
Je, wajuwa kuwa huo mfumo ulioaminishwa wa kuabudu umetoka kwao? Kila wakibadilicho huko kwao kinaakisiwa Afrika hadi kwy dhehebu lako na unafuata hivyo hivyo (Kumbuka The Doctrine of Papal Infallibility).Tangu nilipoelewa kuwa dini yangu hainishikii bango, fimbo, mjeledi, panga, mshale, kisu, bunduki, bomu wala sheria yoyote kuwa kumwabudu Mungu(Yawe, Yesu na Roho Mtakatifu) yani siyo lazima bali ni hiyari na nilianza kuona matokeo baada ya hapo, kamwe sitaki kuelewa dini ililetwa na nani, kwa faida ya nani, wala nani ana ulazima wa kuwa Mkuu Kiongozi Mkuu katika hiyo dini na dhehebu ninaloabudu.
Jinsi ilivyo kidunia yani kuzaliwa karibu na bahari, mto, ziwa siyo sababu ya kujua kupiga mbizi, ndivyo jinsi ufalme wa Mungu utavyomilikiwa na watakatifu wake.
JINSI UFALME WA MBINGUNI UNAVYOFANANA:
MATHAYO 13:44-50.
"[44]Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.
[45]Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri;
[46]naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua.
[47]Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna;
[48]hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa.
[49]Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki,
[50]na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno."
Basi kupanga ni kuchagua, ikiwa unataka kumwabudu Mungu mpaka Kiongozi wa hiyo dini awe Mwafrika kazi kwako, ila ukiwa unataka nuru halisi ya wokovu kuhusu Mungu muumba mbingu na nchi, hayo mengine hayahusiani kabisa.
Ndiyomaana wawezaona Israel iliyotangulia kupata nuru ya kumjua Mungu halisi, bado wapo wasiotaka kumsikia hata huyo Mungu na wanampinga kwa nguvu zote sababu ya utukutu wao tu, ni sawa na jinsi sheria za kidunia zinavyokataza watu wasiue, wasiibe lakini kila siku watu huendelea kujihusisha na huo uhalifu, halikadhalika ndivyo ilvyo katika kumcha Mungu imekuwa tatizo kwa baadhi yetu sisi Binadamu.
Yesu yupo, tumeshuhudia kazi zake na tunazidi kuzishuhudia anavyojitangaza utukufu wake, na lazima injili ienee duniani kote na kila goti litapigwa mbele zake Mungu kukiri na kuamini hakika Mungu anastahili kuabudiwa duniani na mbinguni kote.
Hahahaaa.... Nimeipenda hiyo. Ina ukweli mchungu unaomezeka kwa sukari au asali.Nawapongeza hawa kina Kakobe, Gwajima, Mwamposa wao kuanzisha makanisa yao na wao kua wamiliki na kula hizo hela. Watu mnachanganye hela Tanzania anapelekewa papa italia kula? Wakila kina Mwamposa maneno ila anazokula Papa hazisemwi.
G5 yupi huyo aliyetoka Afrika, naomba kumjuwa pia mkuu.Kuhusu kuwa viongozi, shida Africa ni uwezo mdogo…. ila inawezekana sio kwa zamu wala huruma.
Mfano UN tumewahi kutoa GS mmoja, ni dalili njema…. kuna Bara halijawahi kushika nafasi hiyo.