Dini zinamilikiwa na Wazungu au Waafrika?

Dini zinamilikiwa na Wazungu au Waafrika?

Imani zetu waafrika si ziliitwa za mizimu tukazitupa acha tuongozwe Sasa.. tutapakwa majivu,tutatoa zaka,sadaka na fungu la kumi mixer kuzikana kwa kuangalia huyu alikuwa muumini au hakuwa!.
Imani za Kiafrika ziliogopwa sana kuvunjwa ila sheria za dini leo zinavunjwa bila hofu, unafiki tu!
 
Mshamaliza UE's eeh....!!?? Mnakuja kuhoji upumbavu nyambaaf

Soma hii.​

1 Wakorintho 2:10-16​

Hayo ndiyo mambo Mungu aliyotufunulia kwa njia ya Roho wake. Maana Roho huchunguza kila kitu hata mambo ya ndani kabisa ya Mungu. Nani awezaye kujua mambo ya ndani ya mtu isipokuwa roho yake mtu huyo? Hali kadhalika, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.

Sasa, sisi hatukuipokea roho ya ulimwengu, bali tumepokea Roho atokaye kwa Mungu ili atuwezeshe kujua yale tuliyojaliwa na Mungu. Basi, sisi twafundisha, si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya binadamu, bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua mambo ya kiroho kwa walio na huyo Roho.

Mtu wa kidunia hapokei mambo ya Roho wa Mungu. Kwake mtu huyo mambo hayo ni upumbavu mtupu; yanapita akili yake; maana yanaweza tu kutambuliwa kwa msaada wa Roho. Lakini mtu aliye na huyo Roho anaweza kubainisha ubora wa kila kitu, naye mwenyewe hahukumiwi na mtu mwingine. Maandiko yasema:

“Nani awezaye kuifahamu akili ya Bwana? Nani awezaye kumshauri?” Lakini sisi tunayo akili ya Kristo.

So sisi tunaotafuta maarifa kwenye uzi huu tuna Roho wa Mungu kwa kuwa siyo dhambi kutafuta maarifa, ILA WEWE UNA UKAHABA NDANI YAKO hivyo mchango wako ni uasi na ubatili mtupu.
 

Soma hii.​

1 Wakorintho 2:10-16​

Hayo ndiyo mambo Mungu aliyotufunulia kwa njia ya Roho wake. Maana Roho huchunguza kila kitu hata mambo ya ndani kabisa ya Mungu. Nani awezaye kujua mambo ya ndani ya mtu isipokuwa roho yake mtu huyo? Hali kadhalika, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu. Sasa, sisi hatukuipokea roho ya ulimwengu, bali tumepokea Roho atokaye kwa Mungu ili atuwezeshe kujua yale tuliyojaliwa na Mungu. Basi, sisi twafundisha, si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya binadamu, bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua mambo ya kiroho kwa walio na huyo Roho. Mtu wa kidunia hapokei mambo ya Roho wa Mungu. Kwake mtu huyo mambo hayo ni upumbavu mtupu; yanapita akili yake; maana yanaweza tu kutambuliwa kwa msaada wa Roho. Lakini mtu aliye na huyo Roho anaweza kubainisha ubora wa kila kitu, naye mwenyewe hahukumiwi na mtu mwingine. Maandiko yasema: “Nani awezaye kuifahamu akili ya Bwana? Nani awezaye kumshauri?” Lakini sisi tunayo akili ya Kristo.

So sisi tunaotafuta maarifa kwenye uzi huu tuna Roho wa Mungu kwa kuwa siyo dhambi kutafuta maarifa, ILA WEWE UNA UKAHABA NDANI YAKO hivyo mchango wako ni uasi na ubatili mtupu.
Kwahiyo unaikubali Biblia uliyoletewa na wazungu?
 
Upuuzi kama huo niliauacha nikiwa kidato tu,nashukuru sana elimu ya iliyoasisiwa na huyu huyu mzungu ndio imenikomboa maadam Najua kusoma na kuandika kingereza na kiswahili nikachimba sana kuhusu hizi dini
Na Imani nikaujua ukweli
Nikamkana kuanzia li Mungu lao,mavitabu Yao na upupu mwingi kuwahusu nikaamua kuwapuuza Kwa puuzo kuu mno,

Leo utaniambia Nini ewe Mathayo mweusi wa nanjilinji kuhusu Dini na Mungu wa wayahudi nikuelewe?😁

Haya wewe Mwamedi mweusi wa kilwa kivinje utaniambia Nini kuhusu Mungu wa waarabu nikakuelewa

Kiufupi hua nawadharau sana hamjui tu!
😁😁😁😁🔥🔥
 
Yesu siyo muarabu ni Myahudi. Uislamu ni agano la kale la Biblia. Uislamu ulianzishwa na mapadre watano wa kikatoliki walioasi kanisa katoliki miaka 500 baada ya Kristo.
Jamani kuna maarifa makali humu hadi raha! Yaani unachukuwa notebook na kalamu kabisa. Kumbe ukimya ni hasara, ukiwa muwazi ndiyo unapata maarifa hivi...
 
Waafrika kazi yetu ni kukariri walichoandika. Dini zetu za asili tungezimiliki ila tulizika zote na kufuata za kwao. Mdharau asili yake ni mtumwa, basi tuendelee kuwatumikia na dini zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo maana Dhehebu la Ukatoliki ni dynamic, linaendana na upepo, kwa miaka ya karibuni wamekuja na kitu kinaitwa UTAMADUNISHO (Hubiri na fundisha kwa kadri ya utamaduni wa eneo ulipo ili uwalete watu wa eneo hilo kwa Kristu pasina kuvuruga tamaduni zao).

Kwa hapa Tz Padre Karugendo ni Advocate-nguli wa dhana ya Utamadunisho (Culturalization) na Useja (Celibacy). Ameandika kwa mapana, kina na marefu sana (kwa uhuru wa fikra na mawazo) kuhusu dhana hizi mbili kiasi cha kumsababishia mgogoro na Kanisa.

Hizi dynamisms zitaendelea kufanya RC kuongoza duniani kwa wafuasi wengi.
 
Dini na madhehebu yana wamiliki wake, sio mungu. RC wamiliki wako Italia, Anglican wako UK, Lutheran wako Ujerumani, SDA wako USA, Shia na Suni wako Uarabuni, Budha wako India, Shinto wako Japan, nk.

Viongozi wa hizo dini popote walipo Duniani lazima wa report ama kuchaguliwa na kua endorsed na hao viongozi wao kutoka makao makuu.

Sisi huku Afrika kazi ni kupokea tu hizi dini, kupumbaza watu na kuwafanya waendelee kua masikini kwa kuwatoza michango isiyo na kichwa wala miguu kwa jina la zaka, sadaka na michango mingine, kiasi kidogo kinabakia hapa kikubwa wanapelekewa wamiliki wa kanisa huko walipo.

Nawapongeza hawa kina Kakobe, Gwajima, Mwamposa wao kuanzisha makanisa yao na wao kua wamiliki na kula hizo hela. Watu mnachanganye hela Tanzania anapelekewa papa italia kula? Wakila kina Mwamposa maneno ila anazokula Papa hazisemwi.
Bora waafrika waanzishe madhabehu yao tuchangiane hapa hapa afrika..kuliko kuwapelekea walio tutesa na utumwa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Bora waafrika waanzishe madhabehu yao tuchangiane hapa hapa afrika..kuliko kuwapelekea walio tutesa na utumwa.

#MaendeleoHayanaChama
Great Thinker!

Imagine katika Karne ya 29 BC Kaisari Agusto aliwarubuni (brainwash) Warumi eti wakimpelekea dhahabu wanasamehewa dhambi zao, Warumi wakasambaa duniani kote hadi Afrika kuchukuwa dhahabu zetu kumpelekea Kaisari, akatunza dhahabu, akatumia marble kujenga Roma.

Hii ndiyo asili ya ule usemi "Roma ulijengwa kwa dhahabu/marble" Aliondoa majumba yote ya matofali Roma akayajenga kwa marble.
 
Great Thinker!

Imagine katika Karne ya 29 BC Kaisari Agusto aliwarubuni (brainwash) Warumi eti wakimpelekea dhahabu wanasamehewa dhambi zao, Warumi wakasambaa duniani kote hadi Afrika kuchukuwa dhahabu zetu kumpelekea Kaisari, akatunza dhahabu, akatumia marble kujenga Roma. Hii ndiyo asili ya ule usemi "Roma ulijengwa kwa dhahabu/marble" Aliondoa majumba yote ya matofali Roma akayajenga kwa marble.
Wanatunyonya sana..we need more ngwajimazi tujitajirishe sisi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Dini ya ukristo yaani ukristo ule wa awali wakina Petro na wengine ilikuwa ni dini ya mtu mweusi vile hao wote walikuwa weusi waisrael wa nyakati zile walikuwa weusi.

Leo ukristo umeibwa na wazungu wakaugeuza ni mali yao. Ndiyo maana wanapambana sana kuchora Yesu mzungu yaani majarida yao yote wamejichora wao kama mitume na mamovies wamejiweka wao ili kufuta uchafu wote.
 
Tribute to Marhum Sh. Abdullah Seif ( Linganaweka)


The Changing Faces of Racism - Maulana Syed Muhammad Rizvi
Jaffari Community Centre920 views25 Sept 2020

- Racism and its different forms throughout time and space - Islam's view on racism, and the examples of the Prophet and Ahlul Bayt - Recognizing and remmbering an African Shi‘a scholar, Shaykh ‘Abdullah Seif who passed away in Lindi, Tanzania, on 12th of September at the age of 81 - Marhum Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi was the pioneer of tabligh among the local African community, despite opposition by the Khoja community of the time -
View attachment 1983472
Sheikh Abdallah Seif Linganaweka

He started gradually, and among his first converts and students was Marhum Shaykh Seif - They were sent for further studies to complete their hawza training - They then returned and served the cause of Shi'ism admirably, especially in southern Tanzania - Recounting a story of when this group was first leaving to study, and the racial prejudice they faced locally in Tanzania -

Discussing the contrast to today, where there is more widespread support and unity, however there is still more work to be done on this front - Tying the concept of unity beyond race, to Karbala and the martyrs who stood together Friday Message Recited By: Maulana Syed Muhammad Rizvi Date: September 18th, 2020

Source : Jaffari Community Centre
 
Koffi Anan, from Ghana.
Na Boutros Boutros Ghali pia.

Ila kuthibitisha ugumu wa Mwaftika kuongoza Dini duniani ni kama mfano huu:

Prof. Kabudi amewahi kuwa Mwenyekiti taifa wa Baraza la Wadhamini la Kanisa Anglikana Tanzania, pia AG, Jaji, Brig. Gen. Rev. Agustino Ramadhani wa Anglikana wote wawili kwa nyakati tofauti wasingeweza kuchaguliwa kuwa Mkuu wa Kanisa Anglikana Duniani wakam-replace Malkia wa Uingereza.

Wapo Waafrika wamefanya makubwa sana (ukiwemo kuondoa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini) na kuwa na hata Nishani ya Nobel na CV kubwa kwa Kanisa kama Askofu Desmond Tutu lakini bado hasingeweza kuwa Kiongozi wa Anglikan duniani.

Labda kwa amri ya Yesu mwenyewe hilo lingewezekana ila kibinadamu siyo rahisi hata kusogelea geti la mtaguso wa kumpata kiongozi wa dini duniani.
 
Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania

(NZIMA)-SIMULIZI YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF (1939 -2020) - HISTORIA YETU part 1









KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)



Sheikh Abdallah Seif Linganaweka anatujuza kuwa Wenyeji wa Lindi jina Lao la asili ni Wakudewe kwa sasa almaaruf wanafahamika kama waMachinga wa pwani ya Lindi.



Babu yake Babu Abdallah Seif alikuwa mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga mwenye watumwa baada ya kuwazidi wanyonge majirani kuja kuwatumikisha kujaza vyakula. Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi. Baada ya kuja mkoloni Muingereza nchini Tanganyika, aliua ufalme na kubakiza uchifu. Sehemu za pwani ziliathirika kwanza kwa kupoteza ufalme mapema kabla ya watu wa bara.. Pwani wakabakia na usheikh na uchifu... usiokuwa na nguvu kama falme za asili za maeneo yao Lindi / Kilwa kabla ya kuja ukoloni...



Sheikh MbogaBure mjuzi wa lugha ya Kiarabu, dini pia mmoja wa waanzilishi wa madhehebu ya Shia Tanzania amuunganisha Mzee Abdallah Seif kupata scholarship kwenda Baghdad, Iraq mwaka 1968 kusoma zaidi dini...



Kijana Abdallah Seif mwaka 1968 alipokwenda Kijijini ashutumiwa kupotea kwa kuukumbatia u-Shia mojawapo ya madhehebu ya dini ya KiIslamu, wakati wengine wote ni Sunni. Lakini babu yake msomi wa dini madhehebu wa Sunni anayetambulika Lindi na Kilwa hakuwa anatoa shutma zozote alikuwa msikivu na kumtia moyo Abdallah Seif asome zaidi na ili kuifahamu dini vizuri zaidi.



Kilichomsukuma Sheikh Abdallah Seif kuvutiwa na u-Shia ni namna masheikh wa ki-Shia walivyokuwa wazi (tabligh) kukaribisha maswali tofauti na madhehebu mengine ya KiIslam ambapo kijana hakuruhusiwa kuhoji na pia kuuliza maswali ilikuwa inachukuliwa ni utovu wa nidhamu kwa waalimu au masheikh wake.



Safari ya Sheikh Abdallah Seif wenzie vijana wakiwemo kina Sheikh Isihaka Pingili kwenda Iraq kwa meli iliwachukua mwezi mzima kupitia bandari mbalimbali za Zanzibar, Tanga, Mogadishu, Bahrain na kuishia Basra nchini Iraq na kutua katika chuo cha Hawza mji wa Najaf Iraq



Ujio wao Basra, Iraq ulileta tafrani kwa mwenyeji wao Mpakistani mfanyabiashara mkubwa nchini Iraq enzi hizo na kupelekea Saadam Hussein kumshutumu mfanyabiashara huyo tajwa kuleta majasusi wa kiAfrika ikumbukwe ndiyo kwanza Saddam Hussein na chama chake cha Baath walikuwa wanajaribu kushika hatamu za kuongoza nchi baada ya mapinduzi nchini Iraq. Mpakistani huyo alinyongwa mwaka 1969 pamoja na wafadhili wengine kama kuna Bakri Sadr waliowezesha ujio wa vijana wa kiAfrika
kuingia Iraq kwa dhumuni la kusoma dini.



Kutokana na hilo ikabidi Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine wa kiAfrika waondoke Iraq mwaka 1970 kwenda Lebanon kwenda kuendelea na azma yao ya kusoma dini.



Sheikh Abdallah Seif wakakaa Lebanon kuanzia mwaka 1970 mpaka 1978 ambapo mara nyingine masomo ya dini yakaingia changamoto baada ya vita baina ya Wapaletina waliokuwa kambi za ukimbizi Lebanon na waLebanon wenye nchi na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe.



Mwaka 1978 Ikabidi Sheikh Abdallah Seif na wenzie wahamie nchi ya jirani ya Iran kwenda katika mji wa Qom city kuendelea na masomo yao ya dini. Iran ilikuwa imetulia nchi ya amani chini ya utawala wa mfalme (Shah) Mohammed Reza Pahlavi Historic Personalities of Iran: Mohammad Reza Shah Pahlavi miaka 7 waliakaa Iran wakiendelea kusomeshwa.



Wakati wa likizo Iran wengine wenda Ufaransa kuchuma zabibu mashambani au kufanya kazi sehemu za utalii wa ndani wa Iran au kuchukua mabusati ya kushona ya Iran yanayosifika Uarabuni kote kwenda kuyauza ktk nchi mbalimbali za Arabuni ndivyo mwanafunzi kama Sheikh Abdallah Seif na wenzie vijana walivyojiongezea fedha za kujikimu na kupeleka kiasi cha pesa nyumbani Tanzania.



Hatimaye mwaka 1980 baada ya ukisoma kwa miaka 11 nje ya Tanzania ,walitunikiwa shahada ya baccalauréat ya masomo ya dini na kurejea Tanzania. Kwa miaka hiyo 11 ughaibuni pia waliweza kusoma elimu ya secular kiwango cha sekondari kwa njia ya posta masomo ya nchi ya Uingereza kwa msaada mkubwa wa swahiba wa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria Jenerali Yakubu Gowon. Swahiba huyo alikuwa mfanyabishara wa vituo vya mafuta na makazi yake Uingereza.



Mahojiano haya yanakuja kwa hisani kubwa ya Ammar Dachi yaliyemshawishi Mzee Abdallah Seif kufunguka historia ya mapito yake, ukoo , ilmu na utafiti wa mafuta 1955 na pia ujio wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania


HISTORIA YA ABDALLAH SEIF (1939 -2020) Part - 2







Sheikh Alhaj Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mnan’gole sehemu za Dimba mkoa Lindi Tanzania anaendelea kusimulia kazi kubwa aliyofanya ya kujitolea ya kueneza dini.



Sheikh Abdallah Seif anasisitiza umuhimu wa ilmu na elimu kwa wanazuoni wote wa KiIslamu.



Anasema ili sheikh awe mwanazuoni aliyekamilika kufundisha chuoni lazima kusoma ilmu ya dini kwa angalau miaka 15.



Anakumbuka alivyokuwa mjini Qom Iran akisoma chuoni alionana na wazee wa miaka 70 wakijiendeleza na kuwaambia wao vijana kuwa inahitajika miaka 35 ili kuielewa dini nje ndani kwa ufasaha. Wazee hao walicheka waliposikia vijana Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine toka Afrika wakisema wanataka kusoma dini kwa miaka 5 mpaka 10 tu ilihali wametoka Afrika na kuwaambia bila kupepesa macho kuwa ili wawe wabobevu wafikirie miaka angalau 15 ya ilmu ya dini ngazi ya chuo.



Hivyo akiwa amepikika kwa elimu tosha ya kidini baada ya kufanya kazi kwa takriban miaka 11 nchini Tanzania, mwaka 1990 sheikh Abdallah Seifu alikwenda Nampula jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique kufanya kazi ya dini.



Kisha sheikh Abdallah Seif alishuka mpaka mji mkuu wa Maputo Mozambique na alisaidia kufungua taasisi rasmi inayotambulika na serikali na kupewa leseni iliyosajiliwa Maputo Mozambique kwa ajili ya taasisi ya Shia Ithna-Asheri Muzdalifah . Sheikh Abdallah Seif anazungumza lugha za Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na Kireno.

Source : Asadiqmedia
 
Dini ya ukristo yaani ukristo ule wa awali wakina Petro na wengine ilikuwa ni dini ya mtu mweusi vile hao wote walikuwa weusi waisrael wa nyakati zile walikuwa weusi. Leo ukristo umeibwa na wazungu wakaugeuza ni mali yao. Ndiyo maana wanapambana sana kuchora Yesu mzungu yaani majarida yao yote wamejichora wao kama mitume na mamovies wamejiweka wao ili kufuta uchafu wote.
Golden Mind!

Wametumia Religious propaganda ya gharama kubwa kubadili mindset za waumini wa Kiafrika kuwaamini.

Ila inapokuja USHOGA na NDOA ZA JINSIA MOJA wanalazimisha kuwa makao makuu ya dini hizo ni kwao hivyo kila kitokacho kwao kiheshimiwe na kutekelezwa, kinyume na hapo hakuna msaada.

Je, kiu ya akina Mch. Masanja Mkandamizaji kuleta mapinduzi ya kiimani Afrika itafanikiwa?
 
Waafrika waswahili tunahangaika sana kusaka elimu / Ilmu ya dini za kuja kwa majahazi au manowari toka Ulaya na Mashariki ya Kati huku tukizitupa imani asilia zetu tukidhani tutakubalika kuongoza imani hizo za wenzetu.

Mbaya zaidi tuna jivisha imani hizo za kuja na kuzigawa familia, koo, kabila, wilaya, mikoa na hata Taifa kwa kutumia dini hizo za kuja .


Tunapoteza nguvu, akili na rasilimali muda kutetea imani za kuja kiasi hatuwezi tena kufikiri kwa akili huru na kubaki wafuasi wa dini za kuja na hivyo kukesha kuwaza, kutukuza, kujenga majengo ya ibada kwa nguvu kubwa huku hatuwezi kujitolea kwa nguvu ile ile kuchimba mifereji ya maji kutoka vyanzo vya maji ili kuendeleza kilimo chetu n.k

Wenzetu wamesoma dini zao na kufanikiwa kuitumia katika masuala 'mtambuka' mfano engineering shuleni n.k zaidi ya yale ya kiroho.

Simulizi za Noah / Nuhu ktk imani zao kujenga safina kubwa leo imetimilika huko ulaya/ mashariki ya kati wameweza kujenga meli kubwa za kisasa oil tankers, cruises na majahazi makubwa. Sisi huku hatuwezi meli hata merikebu yetu, tunaweza kukata gogo na kulichimba kutengeneza ka mtumbwi.
Surah Nuh(نوح) 71:1 Indeed, We sent Noah to his people ˹saying to him˺, “Warn your people before a painful punishment comes to them
The story of Noah, the ark, and the Flood in Genesis 6-9 ....... God told Noah to build a big boat, called an ark, and He told Noah exactly how to do it. The ark was to be 450 ft. (137 m) long, 75 ft. (23 m) wide and 45 ft.
 
Tunaweza tukawa tofauti kwa rangi zetu na asili zetu.

Ila Mungu wetu ni Mmoja

nadhani sisi waafrika ndo tuna ubaguzi sisi wote ni binadamu hatutakiwi kubaguana
Hakuna Mungu mmoja. Dini ziko nyingi sana ambazo maagizi zilizo nayo kutoka kwa huyo Mungu yanaachana kabisa
 
Back
Top Bottom