Dini zinamilikiwa na Wazungu au Waafrika?

Yesu hakuwa typically mzungu ila hakuwa pia muarabu. Mbona ipo wazi ukifungua Bible agano jipya unaoneshwa ukoo wake ulivyoanza hadi kufikia kwake "mfalme wa uyahudi"
Sema alikuwa wa wapi, lazima ana kwao ukiacha mbinguni.
 
Yesu siyo muarabu ni Myahudi. Uislamu ni agano la kale la Biblia. Uislamu ulianzishwa na mapadre watano wa kikatoliki walioasi kanisa katoliki miaka 500 baada ya Kristo.
 
Ukweli mchungu mkuu.. dini zina ubaguzi sana ndani yake za wenyewe kwa wenyewe mkuu.. hili nimelitoa katika uvungu wa moyo wangu.. ila bado linaniuma sana
Na huo ukweli mchungu ukiusema unatengwa kundini. Wao wakisemana wenyewe kwa wenyewe unasikia wanameguka EAGT na TAG, mara Kanisa la Kiinjili la Moravian Tanzania KKMT na Kanisa la Moravian Tanzania KMT.
 

Word.
 
Very nice piece, worth publishing in a journal.

Wengi wanakimbilia voodoo kwa sababu zinawapa majibu ya papo kwa hapo. Mfano, wakati wa uchaguzi mkuu wagombea wanaomuabudu Mungu kwenye nyumba za ibada huwa wanasema Mungu subiri kwanza niende kwa Profesa Ndevumbili alafu nitarudi kutubu baada ya kushinda uchaguzi.

Afrika Kusini sheria imeruhusu mitala na hivi karibuni imeruhusu mwanamke kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja, hii sheria inatekelezwa na wenye dini zote zilizoko humo na bahati mbaya sana kwamba SHERIA HII ILIPITA BILA PINGAMIZI.
 
Ni kweli mkuu.

Dini zilianzia Mashariki ya Kati (Ukristo, Uislamu, Bahai, Aramean, Armenia, Kurd, Druze, Judaism, Jewish, zingine zimeanzia Uhindini na Uchina).

Madhehebu yameletwa na Mzungu, so utata ni kuwa hakuna dini bila dhehebu.

Bara Arabia inafyatua dini, Ulaya na Amerika wanafyatua madhehebu. AFRIKA INAPOKEA NA KUMEZA TU. Zikiishabuniwa nje ya Afrika, haraka haraka zinakimbizwa kuletwa Afrika.
 
To answer your question HAIWEZEKANI.

Kimsingi Dini ni tamaduni za hao waliozileta kama zilivyo tamaduni za wanyakyusa, wakyura nk. Mfano leo mizungu au miarabu iabudu miungu ya kikinga unadhani wanaweza kumpa mgeni awe chifu wao?

Leo Afrika wafuasi wa hizo dini wanafanya kila jitihada kujivua tamaduni zao na kuwa kama mabwana zao waliowaletea hizo dini kuanzia muonekano, majina, lugha nk.
 
Tunaweza tukawa tofauti kwa rangi zetu na asili zetu.

Ila Mungu wetu ni Mmoja

nadhani sisi waafrika ndo tuna ubaguzi sisi wote ni binadamu hatutakiwi kubaguana
Mimi ninaamini Mungu kwa upeo wangu, sio kwa kupitia dini yeyote..
Na hapa hatumzungumzii Mungu, tunazizungumzia dini ambazo zimewafanya waafrika kuwa wajinga.....
 
Je, wajuwa kuwa huo mfumo ulioaminishwa wa kuabudu umetoka kwao? Kila wakibadilicho huko kwao kinaakisiwa Afrika hadi kwy dhehebu lako na unafuata hivyo hivyo (Kumbuka The Doctrine of Papal Infallibility).

Aidha, Israel ambako ndiyo chimbuko la dini ya Ukristo (siyo Ukristo) Wakristo wako 2% tu, dini ya Uyahudi 75%, Uislamu 19%, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shalom Goldman [ISLAMIC Commentary] yenye kichwa ‘Surveys of religious affiliation in the US and Israel 2015 Washington Post”
 
Nawapongeza hawa kina Kakobe, Gwajima, Mwamposa wao kuanzisha makanisa yao na wao kua wamiliki na kula hizo hela. Watu mnachanganye hela Tanzania anapelekewa papa italia kula? Wakila kina Mwamposa maneno ila anazokula Papa hazisemwi.
Hahahaaa.... Nimeipenda hiyo. Ina ukweli mchungu unaomezeka kwa sukari au asali.
 
Kuhusu kuwa viongozi, shida Africa ni uwezo mdogo…. ila inawezekana sio kwa zamu wala huruma.

Mfano UN tumewahi kutoa GS mmoja, ni dalili njema…. kuna Bara halijawahi kushika nafasi hiyo.
G5 yupi huyo aliyetoka Afrika, naomba kumjuwa pia mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…