Dioniz Kipanya alipotea aliporekodi video ya msafara mrefu ziara ya Rukwa. Leo mnamsikiliza baada ya kumchinja?

unaambiwa hata sisimizi akiitishia serikali huangamizwa! Serikali hainaga mdogo wala mkubwa, ikihisi tu inatishiwa huondoa tishio hilo
 
unaambiwa hata sisimizi akiitishia serikali huangamizwa! Serikali hainaga mdogo wala mkubwa, ikihisi tu inatishiwa huondoa tishio hilo
Sawa. Nimekuelewa.

Kwa hiyo ile katiba ni uongo ? Serikali inatudanganya kwamba tunaruhusiwq kuichallenge kwa nia ya kuiondoa ? Ni uongo mtupu ???

Tukiifuatisha tutaumia.

Kwamba oooh, jamani mimi nafaa yule hafai kwa saab anafuja mafuta ya serikali na misafara ya magari ya kifahari na ukarabati. Ni kosa. Utaumia.

Katiba ile ni uongo wa serikali ?
 
Ogopa sana serikali, ni dola na ina mkono mrefu
 
Halafu leo kuna mtu anasifia kabisa eti msafara umepungua qmmk sijui nani ametuloga
 
Waliomuua nao watauawa
 
Maana yake hakua threat so kulikua hakuna haja ya kumuua. Maana influence yake ilikua ni eneo dogo tu la Rukwa/Katavi.
Issue sio kuwa threat. Hata akiwa threat hapaswi kuuwawa kama kweli walimuua.

MAgufuli alicheza kete moja nzuri sana. Katika kipindi chake aliacha kutekeleza ilani ya ccm akaamua kutekeleza ilani iliyojaa maoni ya wapinzani.

The likes of stable electric power kupitia bwawa la nyerere, relief ya mwendo Kasi, kuhuisha usafiri wa ndege nk, hayo yalikuwa ni maoni ya upinzani. Japo naye aliferi kwenye kuwapoteza watu na kubinya upinzani. Ila still was a patriotic leaders ever than hata nyerere
 
Fuatilia SOMO LA 2 MAZISHI YA CARDINAL PENGO
 
Mshikaji wangu wa enzi za shule Dioniz Kipanya, roho waga inaniuma sana juu ya Dioniz. Wamemkatili sana Dioniz.

Nimesoma shule tofauti na yeye alikuwa ni mshikaji wangu, tukikutana kwenye tuition na michezo, miaka mingi iliyopita 2003 kushuka chini.
Aise pole sana

Mambo madogo lakini mtu unapotezwa

Ova
 
Maana yake hakua threat so kulikua hakuna haja ya kumuua. Maana influence yake ilikua ni eneo dogo tu la Rukwa/Katavi.

Hawana threat yeyote.

Yupo mmoja aliuliwa Bukombe, Geita, Agosti 2025.

Alirusha mwimbo unasema Wajinga Ndio Watatiki.

Akapigiwa simu aende mjini kuchukua helaake. Akarudi kwanza kijiweni, akawaambia wenzake, halafu akaomba buku la nauli aende huko mjini. Aliyemwomba nae akawa hana buku. Na ndio aliyeelezea hili tukio.

Wakati bado kaganda pale kijiweni, kijana mmoja aliyejitambulisha kama anahitaji nyimbo za flashi akawa anaongea na simu. Ghafla ikaja Land Cruiser, ikamchukua yule kijana wa flashi ( alikuwa kumbe wa kwao) na huyu mhanga, kinguvu. Hajaonekana mpaka leo.

Wamechinja mtu ambae hana hata buku mfukoni la kusema anunue lile bisu la Wamachinga wa Kimasai akapindue nchi. Na hata akiambiwa nchi tumeshachukua, mchango wako mkubwa, njoo mjini uapishwe uwaziri - hana nauli!

Anaitwa Mchungaji Elisha Juma.

Roho inaniuma vibaya mno yani !
 
Duh hii story imeniumiza sana, hili taifa linaelekea wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…