Uchaguzi 2020 Diplomasia ya Uchumi kumbeba Magufuli Uchaguzi wa Urais Oktoba 2020

Uchaguzi 2020 Diplomasia ya Uchumi kumbeba Magufuli Uchaguzi wa Urais Oktoba 2020

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,506
Reaction score
16,003
Ndugu zangu,

Ukiacha jinsi alivyosimamia rasilimali kwa maslahi ya Watanzania namna alivyolikabili janga la COVID-19 hususani dhidi ya sera dhidi ya WHO na baadhi ya mataifa mengine.

Tukija visa na mikasa ya majirani hususani Kenya, JPM ameonesha msimamo usioyumba, hakika ramani ya Tanzania imeng'aa. Hata wafuasi wa CHADEMA waliopo kwenye Jukwaa la Kenya wamebaki midomo wazi wasipate la kubwabwaja.

Itoshe tu kusema Tanzania inahitaji Amiri jeshi Mkuu mwenye hulka ya JPM ili kutuvusha kwenye diplomasia ya uchumi.

Tunamuhitaji Magufuli tena!
 
Kafanya nini na kimeifaidisha nini Tanzania kwenye hiyo Diplomasia ya uchumi?

Yaani saivi marafiki zetu wamekuwa wafu Zimbabwe na Burundi ndo unasema amefanikiwa kwenye diplomasia ya uchumi???? Burundi na Zimbabwe wanaongeza nini kwenye Uchumi wa Tanzania kilaza wewe?

Ungeniambia amehamasisha uwekezaji wa Bandari ya Bagamoyo ambapo Tanzania ndo tungekuwa Gateway kiuchumi kwa Central and East Africa hapo ningekuelewa.

Mchina kashindwana nae kaamua kwenda Lamu na anatengeneza Bandari na economic Zone kule nyie mnaendelea tu na propaganda zenu hapa

Kiufupi Magufuli kaua diplomasia ya uchumi na hakuna lolote alilofanya zaidi ya kujiweka karibu na wafu Zimbabwe na Burundi
 
Capture.JPG


hatuna maneno mengi bana
 
Hivi wewe dada, huwezi kuandika kitu bila kuitaja Chadema?
Hivi unajua kuna kifo na siku ukifa utazikwa mwenyewe huku Chadema na Ccm vikisalia duniani?
Hovyo kabisa
 
Simpigii kura Magufuli, ni mbinafsi, mbabe, mbishi na mtu asiyeheshimu haki za wengine.

Katika kuishi kwangu mtaani nimejifunza mambo mengi sana, dereva wa Lori akiwa barabarani hamjali dereva wa daladala, na dereva wa daladala hamjali bodaboda, na bodaboda hamjali wa baiskeli. Kuna kipindi nimepanda gari la Sumbawanga likaovateki basi lingine bila kumjali muendesha pikipiki, naye akaishia korongoni na dereva wa basi akawa anacheka.

Tatizo ni kwamba ukatiri huwa tunauona kwa wengine, inawezekana kuna majirani zako unawatendea mambo mabaya lakini kwa kuwa anayetendewa si wewe ubaya ule kwako hauonekani. Magufuli ametoka miongoni mwetu, kama utayaona mabaya kwake basi anaweza akawa kioo kwako ili wewe ubadirike. Basi jaribu kujifunza hata mema yanayotendwa na wengine. Jumapili njema.
 
Back
Top Bottom