Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 16,003
- Thread starter
- #21
Hakika
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sitaki kesi ya uhujumu uchumi
hata tukipewa huo uhuru wa kujieleza bado kuna changamoto zingine zitakua kikwazo kwetu, inshort maisha ya mwanadam ni changamoto mwanzo mwisho ukitatua hii inakuja nyingine...Tunahitaji uhuru wa kujieleza, ajira kwa vijana, wastaafu wasicheleweshewe malipo yao.
Kutokuwa na sera za kudumu kutumia sera za majukwaani 'uncertainty policy ' huwezi kukuza uchumi kwa sera za majukwaaniMagufuri lazima aondoke, amelirudisha Taifa miaka takribani 25 nyuma katika kila kitu kuanzia hicho unachoita diplomasia ya uchumi, na kwenye mambo mengine mengi kama utawala wa bora, mahusiano ya kimataifa, siasa safi, mapambano dhidi ya rushwa, n.k.
Diplomasia ya Uchumi.
Kwanza ujue, katika karne hii, unapoamua kuzunguzia masuala ya kiuchumi katika muktadha wa kidemocrasia maana yake unazungumzia namna uchumi wa Taifa unavyochangamana na uchumi wa kidunia.
Sasa, Kwanza sisi tuliishaamua kujichangamana na uchumi wa kidunia, na ndio maana serikali tatu zilizopita ile ya Mzee Ruksa, Mzee Mkapa, na ya Mjeda, Jakaya Kikwete zilijikita kushirikisha wananchi na makampuni ya ndani na nje kwenye kusimamia uchumi, kabla ya ujio wa magufuri, Tanzania ilikua inaongoza katika kuvutia mitaji kutoka nje katika ukanda wa africa mashariki, wananchi kwa wingi sana walikuwa wanashiriki katika shughuri za kiuchumi KWA FAIDA, na uchumi ulikua unakua kwa viwango visivyopungua 6% (1995-2005) na visivyopungua 7% (2005-2015)
Wakati Rais Mwinyi anaingia Madarakani mwaka 1985, nchi hii kila mtu alikuwa anawajibika kwenye sera za CCM na hasa maelekezo ya Azimio la Arusha, ambayo kimsingi yalikuwa yanakasmisha tena labda kwa lugha ingine, yalikuwa yanawanyang'anya wananchi fursa za kushiriki kwenye uchumi walizokuwa nazo kipindi cha mkoloni na kuzikamismisha kwa serikali, matokeo yake yakawa ni kusimika mizizi ya umasikini katika Taifa.
Mashirika ya kiserikali, yaliyopaswa kuongozwa kwa misingi ya kibiashara, basi lau kufuata misingi ya kiuchumi katika kujiendesha yote yakawa yana matawi ya chama cha mapinduzi, vyama vya ushirika badala ya kusimamisha biashara ya mazao ya kilimo kwa faida za wavujajasho wakulima, vikawa vikiendeshwa kwa matakwa ya ccm, n,k
Huku Nyerere akizunguka kila mahala nchini akisema ni lazima tujitegemee huku akiita wazungu mabeberu nyuma ya pazia alikuwa ni omba omba anayetia aibu kwa mataifa ya kijamaa, Hasa uchina na Urusi, ambao walimzawadia miradi mikubwa mikubwa kama hii ya magufuri ambayo serikali ya chama cha mapinduzi haikuwa na uewezo wa nyenzo, fedha wala ujuvi wa kuviendesha na kuviendeleza, ndio maana mpaka leo kuna maswali tu lakini majibu hakuna, viwanda vile vilivyojengwa wakati wa mwalimu vilienda wapi?
sasa, nikiruka miaka ishirini ya utawala wa Mkapa na Kikwete, ambayo ilitengenezewa mazingira mazuri kabisa ya kubadirisha ama kufuta umasikini na ushenzi wote katika Taifa letu baada ya Mzee mwinyi kulivunja azimio la Arusha na kuvunja mizizi ya u-ccm kwa kuruhusu mfumo wa vyama vingi nchini.
Yaani wakati mimi nairuka kwa kwenda mbele, Magufuri ameiruka miaka hiyo hiyo tena na zaidi na kulirudisha nyuma Taifa. Kwanza achana na matendo yake, matamanio yake yote kama ambavyo amekuwa akiyarudia mara kwa mara ni kulirudisha Taifa katika mfumo wa chama kimoja, more than 35 years back. Anataka kulirudisha Taifa katika mfumo ambao asilimia karibia 50 ya nguvu kazi yake hauufahamu zaidi ya kuhadithiwa namna ulivyokuwa wa kijima na wa hovyo.
Mambo yale yale, na mfumo mbovu wa uchumi ule ule alioutengeneza mwalimu baada ya uhuru, ambao baadae ulikuja kumbadirikia na kuwa kama kaa la moto mkononi hata akaikimbia Ikulu ya Magogoni ndio anaoukumbati Magufuri leo, aina ya uchumi ulioelekezwa na azimia la arusha.
Hizi ni imani mbili kati ya nyingi za TANU/CCM/AZIMIO LA ARUSHA
1. Kwamba ili kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakwenda sawa Serikali lazima iwe na mamlaka kamili juu ya njia muhimu za kuukuza uchumi; na
2.Kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe, kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ili kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani na siasa ya watu wote kuwa sawa.
Maazimio haya, na matokeo yake, nyakati hizo, yalikuwa yanapigiwa upatu na wanaccm vipofu, pamoja na watendaji wa serikali waliokuwa na njaa kali sana vichwani mwao, yalipigiwa upatu sana, hasa na wapambe feki wa mwalimu ambao walifikia hatua ya kulazimisha FIKRA ZA MWALIMU ZIDUMU kama ambavyo leo kuna kundi kubwa pia linalotaka kila mtu AUNGE JUHUDI.
Hakuna utawala uliokamilika, hata hizo tawala tatu zilizopita zilikuwa na matatizo mengi tu, lakini hazikuwahi kujiingiza kwenye kwenye makosa ambayo yanaweza kutetemesha familia zote katika Taifa kama ambavyo ilifanya Awamu ya Kwanza.
Nini kinachokupa certainty kwenye sera za uchumi za magufuri? Policy ipi ni certain?Kutokuwa na sera za kudumu kutumia sera za majukwaani 'uncertainty policy ' huwezi kukuza uchumi kwa sera za majukwaani
Kwani umeambiwa wewe. Mimi namhitajiWewe na nani mnamuhitaji huyo Magufuli wako? Usije sema Watanzania maana kuna Watanzania hatumuhitaji.
Hahaha! mlipo enda kununua korosho baba na mama lishe walikosa pesa.wenye vyumba vya kulala pia walikosa pesa vibarua na wasafirishaji walikosa pesa. Hao wanajeshi wanao okoa bilioni 2.2 tungelikupa wewe hiyo pesa ingelikuwa kwenye mzunguko kwenye ujalisilamali kuna somo linaitwa mfanya biashara na mambo yanayo mzunguka 'the entrepreneur and his environments'Nini kinachokupa certainty kwenye sera za uchumi za magufuri? Policy ipi ni certain?
- Analifufua Shirika la Ndege la Taifa, unaona certainity yoyote kwenye hii ambition? Limefufuka? Linafufuka?
- Kilimo, uliwahi kutegemea, hata kwenye ndoto zako kwamba siku moja wanajeshi watatoka makambini waende kukusanya korosho?
- Fedha, uliwahi kutegemea hata siku moja, japo kwenye ndoto zako kwamba wanajeshi watatoka makambini waingie mitaani, wavamie maduka ya fedha za kigeni, wachukue fedha za watu, kwa sababu kuna watu wamefanya nini sijui kwenye fedha za kigeni?
hii ndio unaita certainty ya magufuri?
- watafute wakurugenzi wa precision air, waulize wanaonaje soko la biashara nchini? kawaulize. these poor businessmen can not even think beyond one year in their plans. hawajui ikija ndege ingine watengenezewa uzushi gani.
- Afadhali kwenye madini sababu hata mimi najua tumekuwa tunaibiwa, lakini wadau wa sekta hiyo wako certain na mfumo utakaotumika dhidi yao wakati serikali inachukua vyetu? hemu jiweke kwenye viatu vya makampuni ya madini yaliyo huko nje? ungeweza fikiria kuja kuwekeza hapa?
- Kawaulize wasafiri wa ndege? bei zinaeleweka? ni affordable ?
Well, Nakubaliana na wewe, sera za majukwaani nyingi kwanza kimsingi hazihitaji technical explanations, wao hata ukiimba imba tu wanakuchagua, lakini niambie, Kati ya Mpaka, Kikwete na Magufuri ni na nani amezidisha kwa kuongoza nchi kwa sera za majukwaani? au labda kwa usahihi zaidi, ni nani anaongoza nchi majukwaani?
Usema “diplomasia ya uchumi” halafu ukaitaja Kenya kama jirani. Ingefaa utuambia diplomasia hiyo ya uchumi kwa mifano ya nchi kama Japan, Brazil na SA.
Sidhani unajua hata hiyo “diplomasia ya uchumi” ni moja ya propaganda za hovyo huku mkisema pia tuko kwenye “vita ya kiuchumi”!!!
Hata hivo. Una haki ya kumpenda JPM kama mtu mwingine alivyo na haki ya kutompenda. Wengine hawaoni barabara, ndege, umeme kama ni gharama ya kulipia haki, upendo, furaha, usawa nk!!
Wananchi wasilazike kuacha kimoja ili kupata kingine. Wanastahili kupata vyote viwili!!
usirukeruke, jibu swali langu.Hahaha! mlipo enda kununua korosho baba na mama lishe walikosa pesa.wenye vyumba vya kulala pia walikosa pesa vibarua na wasafirishaji walikosa pesa. Hao wanajeshi wanao okoa bilioni 2.2 tungelikupa wewe hiyo pesa ingelikuwa kwenye mzunguko
Magufuri lazima aondoke, amelirudisha Taifa miaka takribani 25 nyuma katika kila kitu kuanzia hicho unachoita diplomasia ya uchumi, na kwenye mambo mengine mengi kama utawala wa bora, mahusiano ya kimataifa, siasa safi, mapambano dhidi ya rushwa, n.k.
Diplomasia ya Uchumi.
Kwanza ujue, katika karne hii, unapoamua kuzunguzia masuala ya kiuchumi katika muktadha wa kidemocrasia maana yake unazungumzia namna uchumi wa Taifa unavyochangamana na uchumi wa kidunia.
Sasa, Kwanza sisi tuliishaamua kujichangamana na uchumi wa kidunia, na ndio maana serikali tatu zilizopita ile ya Mzee Ruksa, Mzee Mkapa, na ya Mjeda, Jakaya Kikwete zilijikita kushirikisha wananchi na makampuni ya ndani na nje kwenye kusimamia uchumi, kabla ya ujio wa magufuri, Tanzania ilikua inaongoza katika kuvutia mitaji kutoka nje katika ukanda wa africa mashariki, wananchi kwa wingi sana walikuwa wanashiriki katika shughuri za kiuchumi KWA FAIDA, na uchumi ulikua unakua kwa viwango visivyopungua 6% (1995-2005) na visivyopungua 7% (2005-2015)
Wakati Rais Mwinyi anaingia Madarakani mwaka 1985, nchi hii kila mtu alikuwa anawajibika kwenye sera za CCM na hasa maelekezo ya Azimio la Arusha, ambayo kimsingi yalikuwa yanakasmisha tena labda kwa lugha ingine, yalikuwa yanawanyang'anya wananchi fursa za kushiriki kwenye uchumi walizokuwa nazo kipindi cha mkoloni na kuzikamismisha kwa serikali, matokeo yake yakawa ni kusimika mizizi ya umasikini katika Taifa.
Mashirika ya kiserikali, yaliyopaswa kuongozwa kwa misingi ya kibiashara, basi lau kufuata misingi ya kiuchumi katika kujiendesha yote yakawa yana matawi ya chama cha mapinduzi, vyama vya ushirika badala ya kusimamisha biashara ya mazao ya kilimo kwa faida za wavujajasho wakulima, vikawa vikiendeshwa kwa matakwa ya ccm, n,k
Huku Nyerere akizunguka kila mahala nchini akisema ni lazima tujitegemee huku akiita wazungu mabeberu nyuma ya pazia alikuwa ni omba omba anayetia aibu kwa mataifa ya kijamaa, Hasa uchina na Urusi, ambao walimzawadia miradi mikubwa mikubwa kama hii ya magufuri ambayo serikali ya chama cha mapinduzi haikuwa na uewezo wa nyenzo, fedha wala ujuvi wa kuviendesha na kuviendeleza, ndio maana mpaka leo kuna maswali tu lakini majibu hakuna, viwanda vile vilivyojengwa wakati wa mwalimu vilienda wapi?
sasa, nikiruka miaka ishirini ya utawala wa Mkapa na Kikwete, ambayo ilitengenezewa mazingira mazuri kabisa ya kubadirisha ama kufuta umasikini na ushenzi wote katika Taifa letu baada ya Mzee mwinyi kulivunja azimio la Arusha na kuvunja mizizi ya u-ccm kwa kuruhusu mfumo wa vyama vingi nchini.
Yaani wakati mimi nairuka kwa kwenda mbele, Magufuri ameiruka miaka hiyo hiyo tena na zaidi na kulirudisha nyuma Taifa. Kwanza achana na matendo yake, matamanio yake yote kama ambavyo amekuwa akiyarudia mara kwa mara ni kulirudisha Taifa katika mfumo wa chama kimoja, more than 35 years back. Anataka kulirudisha Taifa katika mfumo ambao asilimia karibia 50 ya nguvu kazi yake hauufahamu zaidi ya kuhadithiwa namna ulivyokuwa wa kijima na wa hovyo.
Mambo yale yale, na mfumo mbovu wa uchumi ule ule alioutengeneza mwalimu baada ya uhuru, ambao baadae ulikuja kumbadirikia na kuwa kama kaa la moto mkononi hata akaikimbia Ikulu ya Magogoni ndio anaoukumbati Magufuri leo, aina ya uchumi ulioelekezwa na azimia la arusha.
Hizi ni imani mbili kati ya nyingi za TANU/CCM/AZIMIO LA ARUSHA
1. Kwamba ili kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakwenda sawa Serikali lazima iwe na mamlaka kamili juu ya njia muhimu za kuukuza uchumi; na
2.Kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe, kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ili kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani na siasa ya watu wote kuwa sawa.
Maazimio haya, na matokeo yake, nyakati hizo, yalikuwa yanapigiwa upatu na wanaccm vipofu, pamoja na watendaji wa serikali waliokuwa na njaa kali sana vichwani mwao, yalipigiwa upatu sana, hasa na wapambe feki wa mwalimu ambao walifikia hatua ya kulazimisha FIKRA ZA MWALIMU ZIDUMU kama ambavyo leo kuna kundi kubwa pia linalotaka kila mtu AUNGE JUHUDI.
Hakuna utawala uliokamilika, hata hizo tawala tatu zilizopita zilikuwa na matatizo mengi tu, lakini hazikuwahi kujiingiza kwenye kwenye makosa ambayo yanaweza kutetemesha familia zote katika Taifa kama ambavyo ilifanya Awamu ya Kwanza.
Soma nilicho andika nakuelewausirukeruke, jibu swali langu.
Matendo ya namna hiyo yanakupa uhakika wa kesho itakuwa vipi?
Magufuri katurudisha kwenye sera za kisiasa na kiuchumi za miaka ya 1961-1990. hatufai.Kamanda fupisha andiko lako na ujikite kwenye hoja
kipi? ushaana na hoja za "Policy certainty"Soma nilicho andika nakuelewa
uncertainty policy not certainty policykipi? ushaana na hoja za "Policy certainty"
either way, umeiacha?uncertainty policy not certainty policy
Mtu kashindwa kuajiri kwa miaka 5, haijawahi kutokea tangia tupate uhuru. Mtaani kajaza jobless hakuna mfano.
Kashindwa kuongezea wafanyakazi mshahara pamoja na stahiki zao mbalimbali.
Kaua uchumi wa watu kwa kodi za kinyonyaji, na kwa ajili ya maamuzi ya kibabe kapelekea kufukuza wawekezaji na kufunga biashara zao hapa nchini hali iliyopelekea wananchi wengi kupoteza ajira
Kaua soko la bidhaa za mazao kama ufuta, korosho, pamba etc kwa ajili ya maamuzi ya kibabe.
Kaua demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari, kafungia vyombo vya habari na kupelekea vijana wengi kupoteza ajira zao.
Kaleta sheria kandamizi katika kila kona, hakuna mwananchi ambaye hajaguswa. October 28 ni lazima apishe magogoni.