Uchaguzi 2020 Diplomasia ya Uchumi kumbeba Magufuli Uchaguzi wa Urais Oktoba 2020

Uchaguzi 2020 Diplomasia ya Uchumi kumbeba Magufuli Uchaguzi wa Urais Oktoba 2020

Ndugu zangu,

Ukiacha jinsi alivyosimamia rasilimali kwa maslahi ya Watanzania namna alivyolikabili janga la COVID-19 hususani dhidi ya sera dhidi ya WHO na baadhi ya mataifa mengine.

Tukija visa na mikasa ya majirani hususani Kenya, JPM ameonesha msimamo usioyumba, hakika ramani ya Tanzania imeng'aa. Hata wafuasi wa CHADEMA waliopo kwenye Jukwaa la Kenya wamebaki midomo wazi wasipate la kubwabwaja.

Itoshe tu kusema Tanzania inahitaji Amiri jeshi Mkuu mwenye hulka ya JPM ili kutuvusha kwenye diplomasia ya uchumi.

Tunamuhitaji Magufuli tena!
Twende na Lissu
 
Lissu ndiye kipenzi cha mamilioni ya watanzania
Ndugu zangu,

Ukiacha jinsi alivyosimamia rasilimali kwa maslahi ya Watanzania namna alivyolikabili janga la COVID-19 hususani dhidi ya sera dhidi ya WHO na baadhi ya mataifa mengine.

Tukija visa na mikasa ya majirani hususani Kenya, JPM ameonesha msimamo usioyumba, hakika ramani ya Tanzania imeng'aa. Hata wafuasi wa CHADEMA waliopo kwenye Jukwaa la Kenya wamebaki midomo wazi wasipate la kubwabwaja.

Itoshe tu kusema Tanzania inahitaji Amiri jeshi Mkuu mwenye hulka ya JPM ili kutuvusha kwenye diplomasia ya uchumi.

Tunamuhitaji Magufuli tena!
 
Usema “diplomasia ya uchumi” halafu ukaitaja Kenya kama jirani. Ingefaa utuambia diplomasia hiyo ya uchumi kwa mifano ya nchi kama Japan, Brazil na SA.

Sidhani unajua hata hiyo “diplomasia ya uchumi” ni moja ya propaganda za hovyo huku mkisema pia tuko kwenye “vita ya kiuchumi”!!!

Hata hivo. Una haki ya kumpenda JPM kama mtu mwingine alivyo na haki ya kutompenda. Wengine hawaoni barabara, ndege, umeme kama ni gharama ya kulipia haki, upendo, furaha, usawa nk!!

Wananchi wasilazike kuacha kimoja ili kupata kingine. Wanastahili kupata vyote viwili!!
Kupata vyote kwa wakati mmoja haiwezekani
 
Magufuri lazima aondoke, amelirudisha Taifa miaka takribani 25 nyuma katika kila kitu kuanzia hicho unachoita diplomasia ya uchumi, na kwenye mambo mengine mengi kama utawala wa bora, mahusiano ya kimataifa, siasa safi, mapambano dhidi ya rushwa, n.k.

Diplomasia ya Uchumi.
Kwanza ujue, katika karne hii, unapoamua kuzunguzia masuala ya kiuchumi katika muktadha wa kidemocrasia maana yake unazungumzia namna uchumi wa Taifa unavyochangamana na uchumi wa kidunia.

Sasa, Kwanza sisi tuliishaamua kujichangamana na uchumi wa kidunia, na ndio maana serikali tatu zilizopita ile ya Mzee Ruksa, Mzee Mkapa, na ya Mjeda, Jakaya Kikwete zilijikita kushirikisha wananchi na makampuni ya ndani na nje kwenye kusimamia uchumi, kabla ya ujio wa magufuri, Tanzania ilikua inaongoza katika kuvutia mitaji kutoka nje katika ukanda wa africa mashariki, wananchi kwa wingi sana walikuwa wanashiriki katika shughuri za kiuchumi KWA FAIDA, na uchumi ulikua unakua kwa viwango visivyopungua 6% (1995-2005) na visivyopungua 7% (2005-2015)

Wakati Rais Mwinyi anaingia Madarakani mwaka 1985, nchi hii kila mtu alikuwa anawajibika kwenye sera za CCM na hasa maelekezo ya Azimio la Arusha, ambayo kimsingi yalikuwa yanakasmisha tena labda kwa lugha ingine, yalikuwa yanawanyang'anya wananchi fursa za kushiriki kwenye uchumi walizokuwa nazo kipindi cha mkoloni na kuzikamismisha kwa serikali, matokeo yake yakawa ni kusimika mizizi ya umasikini katika Taifa.

Mashirika ya kiserikali, yaliyopaswa kuongozwa kwa misingi ya kibiashara, basi lau kufuata misingi ya kiuchumi katika kujiendesha yote yakawa yana matawi ya chama cha mapinduzi, vyama vya ushirika badala ya kusimamisha biashara ya mazao ya kilimo kwa faida za wavujajasho wakulima, vikawa vikiendeshwa kwa matakwa ya ccm, n,k

Huku Nyerere akizunguka kila mahala nchini akisema ni lazima tujitegemee huku akiita wazungu mabeberu nyuma ya pazia alikuwa ni omba omba anayetia aibu kwa mataifa ya kijamaa, Hasa uchina na Urusi, ambao walimzawadia miradi mikubwa mikubwa kama hii ya magufuri ambayo serikali ya chama cha mapinduzi haikuwa na uewezo wa nyenzo, fedha wala ujuvi wa kuviendesha na kuviendeleza, ndio maana mpaka leo kuna maswali tu lakini majibu hakuna, viwanda vile vilivyojengwa wakati wa mwalimu vilienda wapi?

sasa, nikiruka miaka ishirini ya utawala wa Mkapa na Kikwete, ambayo ilitengenezewa mazingira mazuri kabisa ya kubadirisha ama kufuta umasikini na ushenzi wote katika Taifa letu baada ya Mzee mwinyi kulivunja azimio la Arusha na kuvunja mizizi ya u-ccm kwa kuruhusu mfumo wa vyama vingi nchini.

Yaani wakati mimi nairuka kwa kwenda mbele, Magufuri ameiruka miaka hiyo hiyo tena na zaidi na kulirudisha nyuma Taifa. Kwanza achana na matendo yake, matamanio yake yote kama ambavyo amekuwa akiyarudia mara kwa mara ni kulirudisha Taifa katika mfumo wa chama kimoja, more than 35 years back. Anataka kulirudisha Taifa katika mfumo ambao asilimia karibia 50 ya nguvu kazi yake hauufahamu zaidi ya kuhadithiwa namna ulivyokuwa wa kijima na wa hovyo.

Mambo yale yale, na mfumo mbovu wa uchumi ule ule alioutengeneza mwalimu baada ya uhuru, ambao baadae ulikuja kumbadirikia na kuwa kama kaa la moto mkononi hata akaikimbia Ikulu ya Magogoni ndio anaoukumbati Magufuri leo, aina ya uchumi ulioelekezwa na azimia la arusha.

Hizi ni imani mbili kati ya nyingi za TANU/CCM/AZIMIO LA ARUSHA
1. Kwamba ili kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakwenda sawa Serikali lazima iwe na mamlaka kamili juu ya njia muhimu za kuukuza uchumi; na

2.Kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe, kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ili kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani na siasa ya watu wote kuwa sawa.

Maazimio haya, na matokeo yake, nyakati hizo, yalikuwa yanapigiwa upatu na wanaccm vipofu, pamoja na watendaji wa serikali waliokuwa na njaa kali sana vichwani mwao, yalipigiwa upatu sana, hasa na wapambe feki wa mwalimu ambao walifikia hatua ya kulazimisha FIKRA ZA MWALIMU ZIDUMU kama ambavyo leo kuna kundi kubwa pia linalotaka kila mtu AUNGE JUHUDI.

Hakuna utawala uliokamilika, hata hizo tawala tatu zilizopita zilikuwa na matatizo mengi tu, lakini hazikuwahi kujiingiza kwenye kwenye makosa ambayo yanaweza kutetemesha familia zote katika Taifa kama ambavyo ilifanya Awamu ya Kwanza.
Magufuli kuondoka ni ndoto ya mchana ukiwa macho
 
Ndugu zangu,

Ukiacha jinsi alivyosimamia rasilimali kwa maslahi ya Watanzania namna alivyolikabili janga la COVID-19 hususani dhidi ya sera dhidi ya WHO na baadhi ya mataifa mengine.

Tukija visa na mikasa ya majirani hususani Kenya, JPM ameonesha msimamo usioyumba, hakika ramani ya Tanzania imeng'aa. Hata wafuasi wa CHADEMA waliopo kwenye Jukwaa la Kenya wamebaki midomo wazi wasipate la kubwabwaja.

Itoshe tu kusema Tanzania inahitaji Amiri jeshi Mkuu mwenye hulka ya JPM ili kutuvusha kwenye diplomasia ya uchumi.

Tunamuhitaji Magufuli tena!
Sina uhakika kama unajua nini maana Diplomasia ya uchumi na namna inavyotekelezwa!.
 
Ameua EAC iliyoasisiwa na Mwalimu na kufufuliwa na Mkapa na Kikwete hafai kabisa.
 
Sina uhakika kama unajua nini maana Diplomasia ya uchumi na namna inavyotekelezwa!.
nimekatisha maelezo yangu, sababu najua Jamii forums ya sasa imejaa watu wenye tabia ya tweeter. kama wewe hapo ndo umeishamaliza.
 
Magufuli kuondoka ni ndoto ya mchana ukiwa macho
kwa mabavu, lakini kwamba wananchi wanataka nini. kiongozi wa namna gani, kwa maana ya kwamba anayebeba vision ambayo wananchi tuko tayari kushirikiana nae, sio magufuri.
 
Ameua EAC iliyoasisiwa na Mwalimu na kufufuliwa na Mkapa na Kikwete hafai kabisa.
Hana uwezo wa kuhimili ideologies za hata marafiki zake anawezaje kuhimili hoja za washirika au wapinzani wake.
 
Back
Top Bottom