mkulima gwakikolo
JF-Expert Member
- Nov 22, 2014
- 1,767
- 2,855
Hivi wewe Mwandambo ni Mwandambo wa eneo la watokaoMwandambo wote ambako hawajawahi kuwa na fikra za kinafiki kabsaa. Ambao ni wasomi waliokombolewa kifikra au ni wa kutoka nchi ya kusadikika?Katika kuishi kwangu mtaani nimejifunza mambo mengi sana, dereva wa Lori akiwa barabarani hamjali dereva wa daladala, na dereva wa daladala hamjali bodaboda, na bodaboda hamjali wa baiskeli. Kuna kipindi nimepanda gari la Sumbawanga likaovateki basi lingine bila kumjali muendesha pikipiki, naye akaishia korongoni na dereva wa basi akawa anacheka.
Tatizo ni kwamba ukatiri huwa tunauona kwa wengine, inawezekana kuna majirani zako unawatendea mambo mabaya lakini kwa kuwa anayetendewa si wewe ubaya ule kwako hauonekani. Magufuli ametoka miongoni mwetu, kama utayaona mabaya kwake basi anaweza akawa kioo kwako ili wewe ubadirike. Basi jaribu kujifunza hata mema yanayotendwa na wengine. Jumapili njema.
Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app