TANZIA Director Nisher afariki dunia

TANZIA Director Nisher afariki dunia

View attachment 2840201
Director maarufu wa video mbalimbali ikiwemo za Wasanii wa Bongofleva ambaye pia ni Mtoto wa kwanza wa Muhubiri maarufu wa Arusha wa Kanisa la Ngurumo ya Upako Dr. GeorDavie, Nic Davie maarufu Nisher amefariki saa nane na dakika tisa usiku wa kuamkia leo December 12,2023.

Familia ya Dr. GeorDavie imethibitisha kutokea kwa msiba huo wa Kijana wao Nisher na kusema msiba unafanyika katika nyumba ya matamko Kisongo Jijini Arusha na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
Mapesa yote anayogawa mtoto kafia nyumbani,iko shida
 
mzee geodevie atakuwa anajua nini shida, na pengine zilitumika nguvu badala ya hekima na saikolojia katika kumhudumia... nisher kwanza wakishua, mzee ana pesa mzee ana connection, pili yeye mwenyewe mtu mkubwa, maarufu na bila shaka mzigo anao... hizo attempt za kujiua zinaonesha kuna mambo mazito yalikuwa yanamtatiza, pengine madawa, au mambo ya kifamilia.... sasa kuna uwezekano hakupata tiba sahihi ya kimwili, kiakili na kiroho (vitu vote hivi viko ndani ya uwezo wa baba yake)... sasa kuvikosa ndio huko majaribio kadhaa mpaka kufanikiwa kujiua... kifo hakina mbabe ila kama kweli ni kwa kujiua basi mzee wake atakuwa na mengi ya kujilaumu....
swala la kupoteza mtoto ni painfull lakn angepata msaada sahihi lilikuwa ni jambo la kupita, bado ni kijana Mungu angembariki mwingine.. hizo ni assumption zangu kwa sasa until further info kuhusu chanzo cha kifo chake.
 
Back
Top Bottom