Director wa RayVanny atuhumiwa ‘kumuiba’ mtoto wake na kutokomea naye, mzazi mwenzake abaki analia

Director wa RayVanny atuhumiwa ‘kumuiba’ mtoto wake na kutokomea naye, mzazi mwenzake abaki analia

Mpigapicha na Muongozaji Video (Director) wa Msanii Rayvanny anayefahamika kwa jina la Eric Mzava anatuhumiwa kuiba mtoto wake na kutokomea naye huku akimuacha mzazi wenzake akihaha kumtafuta.

Akisimulia stori hiyo, mama wa mtoto ambaye ndiye mzazi mwenza wa Mzava anasema:

“Mzava ni mzazi mwenzangu lakini hatuishi pamoja, ugomvi wetu mimi na yeye ni katika matunzo yam toto, kila nikimwambia kuhusu matunzo amekuwa hajali hilo wakati mimi nina hali ngumu.

“Jumapili iliyopita (Agosti 13, 2023) nilienda ofisini kwake nikiwa na mtoto ambaye ana umri wa mwaka mmoja, akaomba akae na mtoto hadi jioni nikamkubalia.

“Ilipofika jioni wakati namtafuta akawa hapokeo simu na baadaye aka ni block kabisa, nikaanza kumtafuta bila mafanikio, sikumpata yeye wala Mtoto.

“Mtoto wangu bado ana Nyonya, leo ni siku yabtatu sijui alipo na sijui ana hali gani.

“Nimeenda Ustawi wa Jamii, nimezungushwa lakini sijapata msaada wowote, nikaenda Polisi Kituo cha Kati, wakamtafuta kwenye simu wakampata akadai eti mimi nimeende kumtelekeza mtoto kwake, akaaambiwa afike kituoni, hakufika.
“Nimefanikiwa kuongeza na Waziri Gwajima nikamuelezea suala langu, akanipatia maofisa wake wanisikilize, wameahidi kunisaidia, nipo naendelela kusubiri msaada wao lakimi mpaka sasa napo naona kimya.

“Nimeambiwa Mzava amesafiri kwenda Congo, ameenda na Rayvanny, sijui nini kinampa jeuri mpaka sasa anadharau hata Vyombo vya Usalama kama Polisi ambao walimtafuta lakini akawapotezea (anaanza kulia).

“Naomba Serikali na mamlaka zinazohusika zinisaidie kumoata Mtoto wangu, sijui huko alipo ana hali gani.

“Nimejaribu kutafuta watu wake wa karibu hata ndugu zake hakuna anayejua chochote kuhusu alipo mtoto.”

==============

UPDATES...

MAJIBU YA MZAVA

Alipotafutwa Eric Mzava kuhusu taarifa hiyo ya mtoto akajibu: "Nani amekwambia kuwa mimi nimemchukua mtoto? Mimi sijui chochote."
Duuh asee
 
Back
Top Bottom