Dirisha la Usajili CAF na TFF limefungwa RASMI niliyoshauri yafanyiwe kazi Simba HAYAJAFANYIKA, Wanasimba mjiandae kisaikolojia

Dirisha la Usajili CAF na TFF limefungwa RASMI niliyoshauri yafanyiwe kazi Simba HAYAJAFANYIKA, Wanasimba mjiandae kisaikolojia

Ndio umeandika nini hapa?
HUJUI KITU,
KAA KIMYA.
CHAMA NI WINGA?[emoji23][emoji23][emoji23]

dully jr
Usiwe unaropoka sana Mimi najua mpira ndio maana nilifanya kazi simba ya mafanikio nikiwa Kijana mdogo kabisa.

Michezo yote ya simba Tangu amekuja Robertinho na Benchika.
Chama anacheza No 11
Saido anacheza No 10.

Chama aliomba awe anachezeshwa winga mika mingi tangu enzi za patric Ausem ( Uchebe) akiwatumia washambuliaji wawili kagere na Boko.
Winga Okwi winga Chama.

JIFUNZE MPIRA NA SIO USHABIKI MAANDAZI.
 
Che Malone amechoka,Ngoma ndio hata mzuka hana,Saido hoi mwili unataka akili imechoka wkt watu wengine wapo wakuanza,in nutshell Simba iombe ipate nafasi ya 2 ili iende champions league then wasuke kikosi otherwise nawaona shirikisho.
Kocha anatakiwa kuwapa vijana wengine nafasi wenye uchu km KażI,Chasambi yule mzanzibar wanaotakiwa kuanza ni Chama,Hussein,Kibu and Che Malone wengine wote waanze bench
 
Hatima ya Simba kwenda champs au shirikisho iko Kwa Ihefu/Black Stars kesho kutwa.
 
Tatizo quality...Simba wamekosa namna au wapi pa kutafuta quality za maana aidha Kwa kuwa na watu wasiofahamu wanafanya Nini au makusudi au tamaa za kupiga, kwenye football hakuna kubahatisha linapokuja suala la kutafuta quality players maana inahitaji timu ya watu wabobevu kuweza kujua Hilo, Bara la afrika ni Bara lenye vipaji lukuki vya soka tena Kwa bei rahisi kweli kweli.

Ni jukumu la mgt kuweza kufanya kazi Yao lakini nashangaa hili hawalifanyi, wachezaji wa kigeni Simba inaoleta mbona hata hapa bongo tunao wengi tu!, tunahitaji exceptional siyo magarasa ya kukimbia kimbia tu. Na kitu kibaya kinachoipoteza Simba ni kucheza biti la Yanga, badala ya kufocus na mambo Yao kama Simba eti tunafocus na trend za Yanga ambazo hazina faida, mtani akifeli ss ndo furaha yetu huu ni upuuzi. Lazima tufocus na ya kwetu kwanza.

Mambo ya kujifananisha na Yanga tuyaache, tucheze na biti ya kwetu kwann tuwe kwenye presha ya mtani wetu?, hata timu kubwa ulaya hazifanyi ujinga huu...huwezi Kuta Real Madrid anajifananisha FC Barca, Kila mmoja anajiangalia yy namna gani ya kuweza kutoboa na kushinda vikombe, Simba imekubali kirahisi kuwa ndani ya circle ya Yanga.
 
Back
Top Bottom