if cap fits
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 1,461
- 2,062
Tutafutane ukiwa na mda, huenda ukauona uwezo wangu vizuri, nimeanza huu mchezo nikiwa darasa la nne na kaka zangu wote walikuwa wanacheza michezo yote karate, judo, kick box hata taikondo, nilikuwa nawafata wananizuia ila baadae nikapendwa na mwalimu mmoja akawazuia kuwa wananifukuza. Akaanza kunifundisha kutafuta stamina na mikao mbali mbali na baada ya mda nikaaza rasimi na nilikuwa ndo mdogo peke yangu.What kind of moves u can do?
Nilikutana na vijana wa umri wangu wengi kupimana uwezo lakini mimi nilikuwa haraka zaidi yao na hakuna aliyeweza kunishinda ,hadi naachana na mwalimu huyo naenda secondary nilikuwa vizuri sana,hadi leo mtaani wananijua kuwa nilianza sanaa za mapigano tangu zamani, yani ni kama hobby tu,, mana hata nilipokuwa katoto nilikuwa sikubali kushindwa ,nakumbuka niliwahi kupigwa na mdada mmoja aliyekuwa mkubwa zaidi baada ya kutuharibia mchezo wetu na kutufukuza mimi nikabaki nikasema napigana na yeye, alinipiga mana alikuwa mkubwa sana ila sikukubali hadi wanakuja kuamua wanakuta nimeumia sana na yeye kachoka utazani anapigana na mkubwa na hali mimi nilikuwa kitoto kidogo,na hapo nilikiwa sina elimu yoyote ya mapigano.
Hao kaka zangu walikuwa na uwezo mkubwa sana, ukiwakuta wanafanya mazoezi utazani niwachina wapo pale, walikuwa wanacheza michezo yote na walikuwa na nidhamu sana mazoezi yalikuwa yanafanyika kuanzia saa kumi usiku hadi saa moja na jioni saa kumi na mbili hadi saa tatu,na walikuwa wanakimbia mbio ndefu sana hivyo pumzi walikuwa nayo sana.
Mwisho,hii kazi ni ngumu na inataka moyo wa kujitoa kweli kweli mana usipofanya mazoezi wiki moja au siku tatu au nne utagundua kuna vitu unapoteza, yani hata ukiwa safari ukifika sehemu pana utulivu lazima ufanye mazoezi, mahari popote lazima upate hata nusu saa au lisaa limoja u practice.