Hivi kwanini baadhi ya watu wanapenda kufikia hitimisho haraka haraka? Kwanini tumejenga mazoea ya kwamba tunayoyajua sisi, basi lazima na wengine wayajue kama sisi!!?? Kama wewe unajua kuimba wimbo wa Taifa, so what?!! Ni wewe! Tangu lini kwa mtu asiyejua wimbo wa Taifa (Tanzania) kwamba amekuwa hajitambui? Tena amekuwa mkweli kabisa kwamba haujui na haupendi! amesema wazi, nilidhani kwamba kwa kusema hayo ndio anajitambua, maana anajua asichojua na asichopenda. Labda kama kuna mengine, lakini kwa hili la Wimbo wa Taifa, hapana si haki kuhukumu. Mleta mada una mangapi huyajui maishani mwako ambayo wengine wanayajua, je na wewe kutuite hujitambui!! Hapana