Diva: Siwezi kuingia kwenye mahusiano na mwanaume asiyejua kuongea kingereza

Diva: Siwezi kuingia kwenye mahusiano na mwanaume asiyejua kuongea kingereza

Mbona wanaokijua hawamuoni sasa au yeye hajui kama hana viwango vya tunaoongea kiinglish?
 
Kumbe wa kawaida kuliko kawaida yenyewe! Ngoja ajibaraguze. Ipo siku atasema anataka wazee vijana hawataki kwakuwa atakuwa kachemka kucompete na warimbwende wa ukweli wa jiji
 
Prof mary karoro okurut, katika kitabu chake "the official wife" alihoji, "does vargina go to school", alikuwa anawazungumzia wanaume waliokuwa wanaacha wake zao ksa kgezo cha elimu
 
Hapo ndiyo vidume mtofautishe kati ya kupenda na kutamani.kuna wimbo flan waliimba the welas unaitwa the blac sheet man.kumbe ulikua na maana kubwa sanaa kwa watu wenye rangi kama hyo ya sijui diva.siye watu weusi tuna shida sanaaaa!.
 
Kwanza ana simama na vitoto muda wote yan Diva sijui kama yuko sahihi kichwani
 
Wasalaam wana jamvi.
Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Diva The Bosslady amefunguka kwa kudai kuwa hawezi kudate na mwanaume ambaye hajui kuongea kingereza kwa kuwa yeye katika maisha yake huongea Kiingereza zaidi kuliko Kiswahili.

Akiongea na waandishi wiki hii, Diva amedai wanaume ambao amewahi kutokana nao wanazungumza lugha hiyo ambayo amedai inamvutia sana.

"Sipendi mwanaume ambaye hajui Kiingereza, napenda kudate na mwanaume ambaye anajua Kiingereza," alisema Diva.

"Yaani imetulia na inapendeza kwa sababu siyo local local, wapo ambao waliwahi kunitokea lakini baada ya kujua hawajui kingereza nikawatosa,"

Alisema wanaume wake wengi anakutana nao kwa mara ya kwanza kupitia kipindi chake cha Ala za Roho kwa kuwa ndio sehemu ambayo atakutana na watu mbalimbali.

Mtangazaji huyo ambaye pia ni muimbaji wa muziki kwa sasa anatoka kimapenzi na muimbaji 'Heri Muziki'.
Ina maana wazazi wako huo hamuongei au lugha ni kwenye mapenzi tu...
 
Baada ya yote tunaishia kwenye mahojiano....hizi mbwembwe za mjini zinazidi kuboa
 
Back
Top Bottom