Division 1 ya point saba imepoteza hadhi, Shule kama Saint Francis wanafunzi "wote" wamenyoosha, nashauri kuanzishwe division 1 ya 6 na 1 ya 5

Division 1 ya point saba imepoteza hadhi, Shule kama Saint Francis wanafunzi "wote" wamenyoosha, nashauri kuanzishwe division 1 ya 6 na 1 ya 5

Hiyo shule miaka mingi wapo vizuri kwenye matokeo ya kidato Cha nne na Cha pili na kipindi Cha nyuma walivyokuwa wanatangaza shule kumi Bora Kitaifa ,shule hiyo haijawahi kukoseka kwenye top ten .
 
Hii imekuwa too much sasa, hawa mabinti wa saint francis wanaifedhehesha Necta 😂

Division 1 ya saba kwao imekuwa kama kumpa samaka mtihani wa kuogelea, kila mwanafunzi anaibonda !!

Shule imesha master mbinu ya kuwafanya wanafunzi wote wapate division 1 ya saba.

Nashauri kuongezwe division za ziada kama 1 ya 5 na 1 ya sita maalum kwa hizi shule,

A za kawaida zilete 1 ya 7, A za kuanzia 90 zilete 1 ya 6, A za kuanzia 95 ziwe 1 ya 5

View attachment 3192124
Wanasoma vizuri
 
Hayo ndiyo maendeleo, Hongera sana kwao

Ama hakika, Mama Samia anaupiga mwingi, mitano tena kwake
 
One iliheshimika mwisho mwaka 2012.

Ukipata hata div two wewe ni mwamba, baada ya hapo tulianza kushuhudia maigizo kibao, mara div five, sijui distinction na ngonjera kibao.
Walaumiwe Waislamu na wanasiasa
 
Hiyo shule miaka mingi wapo vizuri kwenye matokeo ya kidato Cha nne na Cha pili na kipindi Cha nyuma walivyokuwa wanatangaza shule kumi Bora Kitaifa ,shule hiyo haijawahi kukoseka kwenye top ten .
Sio top ten ni top three ama top two kabisa

Wao ilikuwa ni moja au mbili wakizingua sana labda tatu
 
Kikubwa baba zao wawe na mitaji ama mabiashara makubwa maana bila hivyo hao watoto wataishia kufedheeka tu na maisha baada ya shule.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Back
Top Bottom