Diwani ashindwa jaribio la kumchafua kwa makusudi Waziri Mstaafu Kawambwa huko Bagamoyo


Dr. Kawambwa ni mtu mpole sana na mwangalifu. Pale FOE alikuwa kitengo cha IPI enzi hizo. Hana makuu na nilishituka sana niliposikia amekuwa dalali. Huyo diwani amekosa adabu kabisa.
 
Mawazo yako yamejaa u-dola. Mimi sijui mgogoro wao ni nani mwenye kosa, lakini nadhani kumdhalilisha mtu yeyote siyo vizuri (bila kujali cheo au alikuwa nani). DSO wa Bagamoyo kasikilia bango kwa sababu aliyedhalilishwa ni DSO, ingekuwa ni mtu wa kawaida je, ingekuwaje?
 
Kwahiyo rais mstaafu unamlinganisha na DSO?
 
Ukweli, migogoro mingi ya ardhi inasababiswa na wastaafu njiti, kule magu kuna dc mstaafu kaenda kujambazia shamba la kikongwe, katengeneza na hati kapelekwa hadi kwa waziri slaa kakomaa tu, tunamsubiri site tumalizane nae, huyu diwani na beki wa mlandege nae tunamsubiri atoke jela atueleze vizuri kisa cha kumfunga prof wigi mikononi,
 
dah, inasikitisha sana. huyo kijana hajakamatwa hadi sasa? hivi ana power gani ya kukamata mtu kwa namna anavyotaka kufanya? hao ndio vijana mnawapa udiwani kumbe wahuni tu. afundishwe iwe shule kwa wengine hata kwao hana wakubwa? kwanini asingeongea kwa ustaarabu kwa hoja walau. serikali ichukue hatua.
 
Yuko ndani na kesho nampelekea chai kuhakikisha hatoki hadi j3 atakapopandishwa kizimbani
 
Yuko ndani na kesho nampelekea chai kuhakikisha hatoki hadi j3 atakapopandishwa kizimbani
unajua hiyo ni common assault kabisa, pamoja na kosa lingine wamtafutie afundishwe naona wazazi wake hawakufanikiwa kumfundisha. hivi kweli unamdhalilisha mtu mzima vile? hata kama asingekuwa waziri.
 
Waziri mstaafu Huwa hapewi bodyguard?

Huyo kijana angeweza kumwiba kawambwa na kutokomea nae kusikojulikana!!

Anyway,

Igizo Hilo limefanikiwa, naamini lengo ni kupeleka taarifa juu Ili Kawambwa naye aje mezani " kula", maana amesahaulika.
 
Uvccm ni genge la wahuni na wengine ndiyo hawa usiku wanageuka kuwa panyaroad
 
Dunia Ina Mambo
Nilipoona ile clip nilijiuliza maswali sana kwani wengine tunmebahatika kumfahamu mh Kawambwa akiwa waziri na Mbunge. Nimeshawahi kukutana naye ni mzee hekima na busara sana.Mtaratibu msikivu na hana mabishano. Huyu dogo alichofanya ni upuuzi wa hali ya juu kwa kitendo cha kumdhalilisha Kiongozi. Kwani kulikuwa na haja gani ya kurekodi swali la kwanza? Pili kuita kama anamuita mwanae eti wewe Kawambwa. Tatu kumtishia sijui pingu kwani ni jambazi au mzee alimtishia nini mpaka kutaka mfunga? Pingu unamfunga mtu mkorofi aliyekaidi sasa mzee mwenyewe ni mpole na hakuwa na mabishano yoyote. Nadhani iwe fundisho kwa vijana wenzetu wasiojielewa na kuheshimu wazee wetu hasa hawa waliotumikia nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…