Tetesi: Diwani Athumani au Wambura Camilius mmoja anaweza kuwa IGP, Selemani Mombo kwenda TISS?

Status
Not open for further replies.
Tukitaka polisi jeshi lile linyooke rais afanye maamuzi kama ya mtangulizi wake alivyompeleka maj general mzee magereza basi mm nashauri kuna brig general anaitwa mkande huyo jeshi la polisi atalinyoosha na kuliweka kwenye mstari nmewahi kufanya nae kazi mahali jamaa ni mtu na nusu hata wenzake wanamjua
 
Wewe bwana achana na watoto wa humu,huyu jamaa akiwa polisi ni moja ya maofisa askari wadogo walikiwa wanamuogopa maana hapendi kupindisha mambo,tofauti ya huyu jamaa na hamduni ni rangi tu.
Sometime huwa naamini hawa jamaa dini inawashape kiasi pia.
 
Huu ujinga siku akiufanya raisi yeyote hakuna rangi ataacha kuona.

Upolisi ni taaluma inayojitegemea,halafu kuna uaskari.
Kila polisi ni askari ila sio kila askari ni polisi,hata waliousomea huko ccp wengi bado upolisi hawana(rejea kangi lugola) ije kuwa mwanajeshi asiyejua hata jukumu la msingi la mkuu wa kituo!!!
Tofauti ya ukuu wa polisi na ukuu wa taasisi nyingine,ili uwe mkuu bora wa taasisi hiyo lazima uwe umeotumikia kwa vyeo mbali mbali.unamweka mjeshi ambaye hajui kutoa maamuzi katika vurugu za uchaguzi,ataagiza watu wapigwe risasi za moto.

Kwanza atapata upinzani tokea ndani ya taasisi,maana sio pure.
Pili kazi yenyewe itamshinda maana haifahamu vyema.
 

Naungana na wewe. Kiongozi bora ni Yule aliyekulia ndani ya mfumo na Sio nje ya mfumo. Tumeona hata DAM( Diwani Athuman Msuya) Upinzani ambao amekumbana nao chini kwa chini uliokuwa na lengo la kumuonesha hawezi. Ni muhimu kumchukua Kiongozi aliyekulia ndani ya mifumo; hao wa nje huwa inawachukua Muda kujifunza na adaptation ya culture organisation. Kwa mfano huyo DG wa MSD ambae ni Mjeshi ,hakuwahi kufanya kazi hata siku moja kwenye mfumo wa ugavi,akaenda kupewa MSD akiwa na dhana ya utii, je amefanikiwa chochote kwa kulinganisha na watangulizi wake ? Mwisho wa siku tumeona Rais alivyoonesha MSD now ni worst enough as compared na miaka ya nyuma. Swali la msingi ,Ngosha alikosa mfamasia mwenye uwezo palepale wizarani au MSD kuifanya kazi kama DG ? Naamini wapo
Taasisi sio za majaribio ,tuangalie namna bora ya kupata hawa watu
Halafu Hii mambo ya kutumia jeshi kusimamia taasisi ilianza na mwendazake na ni ilikuwa ni uporaji wa kazi za raia
 
Mmepewa lini ndugu [emoji23][emoji23][emoji23] wakati mwezi jana na mwezi huu mpaka leo hamjalipwa, na utaratibu unapoelekea ni kuwanywa kichwa kabisa [emoji38][emoji38][emoji38] mama anawapigia mwingi sana!!
Poleni
Mama kagundua anahujumiwa na hao jamaa Labda!!why KWENYE Report ya CAG wakuu wote wa ulinzi wa pande hizo hawajahudhuria hafla!!?wameanza vugu vugu Nini!!!
 
Binafsi natamani IGP mpya awe Suzan Kaganda maana ana uwezo na uthubutu wa kukemea maovu hata ndani ya Police bila kujali mambo ya jinsia pia ni msomi na muumini wa utawala bora sheria.
Mama Samia tupia jicho lako kwenye faili yake please.
 
Binafsi natamani IGP mpya awe Suzan Kaganda maana ana uwezo na uthubutu wa kukemea maovu hata ndani ya Police bila kujali mambo ya jinsia pia ni msomi na muumini wa utawala bora sheria.
Mama Samia tupia jicho lako kwenye faili yake please.
Level of Education yake ikoje?
 
Kila taaluma waongozane wao, kutuletea bwana afya kuwa headticha hatuwezi kukataa lakn tutampng kimya kmya
 
Kwa Mimi sioni tatizo kuwatumia hao jwtz iwapo wana taaluma husika. Ingekuwa mtu anapelekwa kuongoza hospital ya Muhimbili halafu sio Dr hapo sawa. Lakini maadam taaluma anayo anafanya tu, hata awe ni Ofisa wa Wanyama pori, Magereza au Zimamoto anaweza kuongoza MSD. Kuhusu Diwani Athumani kukumbana na upinzani wa chini kwa chini ni sababu ya watu WENYE MENTALITY kama yako kuishi kwa MAZOEA , so far huyohuyo Diwani ameonyesha uwezo mkubwa hata kuzidi baadhi ya watangulizi wake.

Hata hapo MSD huyo jwtz ni kati ya wakurugenzi waliofanya vizuri kushinda watangulizi wake hasa suala la vifaa vya DIALYSIS na kuzuia wizi. Pia tangu MSD inaanzishwa kila Mkurugenzi amekuwa akilaumiwa na kutumbuliwa, je hao wote walitokea jwtz au Polisi

Nchi yetu wengi wanaishi kwa mazoea sana. Tunatakiwa kuangalia nje ya Box. Nendeni huko duniani ndipo mtafunguliwa macho, unakuta mtu ni Afisa wa Police (engineer) lakini ni Meneja katika kiwanda cha chuma.

Mtu apimwe kwa weledi na uaminifu lakini sio alipotokea.
 
Ni kweli MI iko vizuri.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…