Diwani Athumani Msuya atenguliwa Ikulu

Diwani Athumani Msuya atenguliwa Ikulu

Kwa ufupi tahasisi imepwaya sana....miaka ya hivi karibuni,
Imeshindwa kuimili mabadiliko ya kitamaduni, kisiasa, kiuchumi, na kitechnologia ndani ya jamii na nje ya jamii yetu.

Taifa kwa ujumla linatakiwa liwe chini ya mikono ya watu wa kudumu wasiopungua watano wakiwemo makatibu wakuu wa mambo ya ndani, mambo ya nje, ulinzi, katibu mkuu kiongozi, katibu mkuu Ikulu, na mkurugenzi wa usalama wa taifa.

Hawa wanapaswa kuwa wazalendo wa kweli, wanaowiwa na maendeleo ya nchi kwenye kila sekta na wasioyumbishwa na itikadi za kisiasa au vyama isipokuwa tu pale ambapo mambo haya yanagusa maslahi ya taifa.

Wanatakiwa kuwa watu wenye upeo mkubwa na uwezo wa kuchambua na kuchakata habari zote za kiintelijinsia kutoka ndani na nje ya nchi ili kumshauri rais katika maamuzi magumu ya kisera yanayoweza kuathiri maslahi ya taifa ya siku kwa siku na yale ya vipindi virefu.

Kimsingi hawa ni watu wenye uwezo mkubwa wa akili na kujiongeza, wasio na tamaa ya madaraka, chembechembe zozote za ufisadi au jazba za kisiasa na dini katika kufanya maamuzi.

Kwasababu ya uwezo wa kubadilika na kujiongeza kutokana na mahitaji ya nchi kwa nyakati tofauti, kunakuwa hakuna haja ya kuwabadilisha mara kwa mara hata kama kiongozi mkuu(rais) amemaliza muda wake wa kikatiba wa kuwepo madarakani au anapoingia rais mwingine.

Kwa uchache.

Mifano ya tawala zenye mafanikio makubwa kwa mataifa husika ipo. Tunatakiwa kuzisoma kwa undani na kuziasilisha kwenye mifumo yetu ili tuweze kusonga mbele.

Kumteua mtu kwenye nafasi nyeti ya kitaifa na kisha kutengua uteuzi chini ya masaa kadhaa ni kuendesha nchi kama marefa na makocha wa michezo ya dakika tisini badala ya taifa linalotegemewa kudumu mpaka jua litakapoishia miaka milioni tano kutoka sasa!

Pia nchi hii itabakia ya kijima sana kwenye kila kitu isipoanza mara moja kuasilisha utawala wa kisasa unaozingatia ukweli na uwazi.
 
Diwani Athumani hawezi kuchinjiwa mbali kama baadhi ya watu wanavyofikiri fikiri kwanza kuhusu CV yake maeneo aliyowahi kupita???
 
Hivi mkuu kutoka DGIS mpaka Chief of staff ni demotion kweli?🤔
I think there must be something wrong au mama alipanga amshushe kiaina bila kelele.
Ni demotion ndg chief of staff wa ikulu sio tz.. wana jF walishaur apelekwe ubaloz akapumzike mama naona kasikia.. haikua sawa.. nadhan Mh rais angepta shida kubwa kumtumatuma hapo ikulu.. that y wamemtengua
 
Eti kakataa unajua mfumo ww.si bado anahitaji kuhema kama ww tu.
Kuweni wapole msiwe na mihemko sw.anapatiwa nafasi nyingine.
 
Kuwa makini na maneno yako
Yana shida gani?

Kukosea kwenye teuzi sensitive sio swala la mzaha, inaonesha kutokuwa makini huko Ikulu.

Soma kitabu cha John Bolton “The Room, Where it Happened’ na upate picha kwa nini raisi marekani anachukua muda sana kuteua. Lakini baada ya kuteua kwanini inakuwa rahisi kwake kupata replacement teuzi wake wake mmoja akimzingua.

Kukusaidia anatumia muda mwingi sana kufanya vetting za nafasi sensitive za Ikulu ambazo zinatakiwa kushikwa na watu wa usalama kupata misimamo yao kwanza. Akishateua anabaki na majina spares ya kumwaga ya watu alio wafanyia interview na kuelewa misimamo yao.

John Bolton mwenyewe alikuwa interviewed na Trump aliposhinda for NSA post lakini akuteulia admin ilipoanza.

Uwezi kuteua leo nafasi ya katibu wa Ikulu halafu keshokutwa yake ukaifuta, mbele ya dunia ni kielelezo tosha Ikulu hawapo makini; chawa awawezi kuona tatizo kwa jicho la dunia sababu wamezoea kusifia tu.
 
Back
Top Bottom