Nowonmai
JF-Expert Member
- Jan 15, 2019
- 1,050
- 1,126
Kwa ufupi tahasisi imepwaya sana....miaka ya hivi karibuni,
Imeshindwa kuimili mabadiliko ya kitamaduni, kisiasa, kiuchumi, na kitechnologia ndani ya jamii na nje ya jamii yetu.
Taifa kwa ujumla linatakiwa liwe chini ya mikono ya watu wa kudumu wasiopungua watano wakiwemo makatibu wakuu wa mambo ya ndani, mambo ya nje, ulinzi, katibu mkuu kiongozi, katibu mkuu Ikulu, na mkurugenzi wa usalama wa taifa.
Hawa wanapaswa kuwa wazalendo wa kweli, wanaowiwa na maendeleo ya nchi kwenye kila sekta na wasioyumbishwa na itikadi za kisiasa au vyama isipokuwa tu pale ambapo mambo haya yanagusa maslahi ya taifa.
Wanatakiwa kuwa watu wenye upeo mkubwa na uwezo wa kuchambua na kuchakata habari zote za kiintelijinsia kutoka ndani na nje ya nchi ili kumshauri rais katika maamuzi magumu ya kisera yanayoweza kuathiri maslahi ya taifa ya siku kwa siku na yale ya vipindi virefu.
Kimsingi hawa ni watu wenye uwezo mkubwa wa akili na kujiongeza, wasio na tamaa ya madaraka, chembechembe zozote za ufisadi au jazba za kisiasa na dini katika kufanya maamuzi.
Kwasababu ya uwezo wa kubadilika na kujiongeza kutokana na mahitaji ya nchi kwa nyakati tofauti, kunakuwa hakuna haja ya kuwabadilisha mara kwa mara hata kama kiongozi mkuu(rais) amemaliza muda wake wa kikatiba wa kuwepo madarakani au anapoingia rais mwingine.
Kwa uchache.
Mifano ya tawala zenye mafanikio makubwa kwa mataifa husika ipo. Tunatakiwa kuzisoma kwa undani na kuziasilisha kwenye mifumo yetu ili tuweze kusonga mbele.
Kumteua mtu kwenye nafasi nyeti ya kitaifa na kisha kutengua uteuzi chini ya masaa kadhaa ni kuendesha nchi kama marefa na makocha wa michezo ya dakika tisini badala ya taifa linalotegemewa kudumu mpaka jua litakapoishia miaka milioni tano kutoka sasa!
Pia nchi hii itabakia ya kijima sana kwenye kila kitu isipoanza mara moja kuasilisha utawala wa kisasa unaozingatia ukweli na uwazi.