Diwani Athumani Msuya atenguliwa Ikulu

Diwani Athumani Msuya atenguliwa Ikulu

Ameukataa uteuzi na sio kutenguliwa!
Niliandika hapa juzi!Iweje Mkurugenzi TISS kupelekwa Ikulu!
Diwani ni mwenye kujitambua,ameukataa uteuzi ule.
Diwani ana uzoefu na serikali zaidi ya Nne za CCM.

Diwani ni afisa aliehudumu idara mchanganyiko za nchi hii kwa kiwango cha juu!

Diwani anaijua michezo yote ya CCM na magenge yake!

Diwani sio Kabudi au Lukuvi!

Diwani ndie afisa mwenye siri nzito za kilichojiri kati ya serikali hizi mbili .....

Serikali ya Magufuli na hii ya Samia!

Pia ieleweke yeye ndie alikuwa madarakani wakati JPM anafariki Dunia.

Yote yaliyojiri katikati hapo...
Ni Diwani ndie anaeyajua!

Diwani sio wa kubezwa!
Diwani anastahili kupewa ulinzi kwa usalama wake!

Kitendo cha kuikataa safe house,ina maana amekataa ku surrender mawasiliano yake yote.
Ili kuanza kutumia mapya ya Safe House!

Na mengi bado yanakuja,maana kadri inavyonyesha,ndio matobo yanavyozidi kuonekana.

"Rais Samia atengua uteuzi wa Diwani Athumani"

By Bakari Kiango
(Mwananchinewspaper)
Alhamisi,05/01/2023.

Dar es Salaam.

Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Ikulu, Kamishna Diwani Athumani uliodumu kwa siku mbili baada ya kuteuliwa akitokea Idara ya Usalama TISS.

Kamishna Diwani aliteuliwa Januari 3, 2023 kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu, akitokea katika wadhifa wa Mkurungezi Mkuu wa TISS, nafasi aliyohudumu kwa siku 1,210 tangu alipoteuliwa na Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Januari 5, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, imeeleza kuwa nafasi ya Diwani imechukuliwa na Mululi Mahendeka aliyekuwa ofisa mwandimizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu.

Alamsikhi
10101.
*Diwani ndie afisa mwenye siri nzito za kilichojiri kati ya serikali hizi mbili .....

Serikali ya Magufuli na hii ya Samia!

Pia ieleweke yeye ndie alikuwa madarakani wakati JPM anafariki Dunia.

Yote yaliyojiri katikati hapo...
Ni Diwani ndie anaeyajua!*

KILA MTANZANIA ASOME HAYA MANENO HAPO NA AYATAFAKARI
 
Hizo hisia zako tu na uzushi hakuna mwenye ubavu wa kukata uteuzi wa rais. Mkurugenzi wa usalama wa taifa ni mtu mdogo sana hawezi kuwa hata tone ndani ya maji ya bahari. Hii nchi ni zaidi ya mtu awaye yote. Vilevile kumbuka rais ni mtu mkubwa sana nchi hii kwa mujibu wa katiba na hawezi kutishwa wala kukwamisha na limkuu wa idara moja ndani ya nchi yenye idara nyingi. Rais ni amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama, we mkuu wa idara moja tu ya usalama utatoa wapi kiburi? Hizo ni hisia zako tu rais anasimamia nchi yenye makomandoo na vyombo vingine vya siri. Sijui kama unaweza kukumbuka issue ya Imrani Kombe aliyekuwa naye mkurugenzi wa usalama wa Taifa. Alitaka kutumia uchaga wake kumsaidi mchaga mwenzake Mrema apate urais alichinjwa mchana kweupe.

Hakuna anayeweza kukataa uteuzi wa Rais, ni majuzi tu aliyekuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Venance Silvatory Mabeyo aliteuliwa baada tu ya kustaafu na hakukataa. Kwanza utaanzaje kukataa jambo la rais? Basi itakuwa hiyo nafasi aliipata isivyostahili, wale wanatakiwa wawe na utii wa hali ya juu usiotiwa shaka ya aina yoyote ndugu. Acha kumnenea uwongo.
Polee sana na jamii iliyo kuzunguka, amini we ni hasara
 
Sijui hua akipewa jina au ushauri hua anameza tu au anatafakari na kuuliza maswali?
Diwani amefanya kazi nzuri sana awamu ya tano. Leo hii unakuta mbowe na genge lake ndio wanataka atoke TISS na mama anakubali na kumshusha hadhi.
Uongo wa akina mbowe umekolea hadi kiongozi dhaifu wa ccm anaamini.
Ccm haijafanya kosa kuwashinda kabisa chadema kwenye uchaguzi mkuu 2020. Wananchi waliona kile kinachofanywa na ccm ya magufuli na kuipa ccm kura karibu zote.
Wewe ni mpumbavu na kama si mpumbavu basi ni mwehu na unatakiwa upelekwe Milembe,ule ni uchaguzi kweli kwa mtu mwenye akili timamu,ona nchi inavyopitia magumu kwa sababu ya Uchaguzi mbovu.Hata kama Rais amekufa mambo yangeenda vizuri kwa sababu viongozi wangekuwa waliochaguliwa na wananchi hivyo wangelinda heshima zao kwa kufanya yenye haki na heshima.
 
Alikuwa DG wa TISS kwa siku 1000 na ushee anajua pa kuingilia na pa kutokea... ANAJIAMINI!

Diwani ni afisa aliehudumu idara mchanganyiko za nchi hii kwa kiwango cha juu!

Diwani anaijua michezo yote ya CCM na magenge yake!

Diwani sio Kabudi au Lukuvi!

Diwani ndie afisa mwenye siri nzito za kilichojiri kati ya serikali hizi mbili .....

Serikali ya Magufuli na hii ya Samia!

Pia ieleweke yeye ndie alikuwa madarakani wakati JPM anafariki Dunia.
Hata serikali ya Kikwete anaijua vizuri sana
 
Umewahi kupata mafunzo yoyote ya vyombo vya ulinzi na usalama? Tunaojua (nimeshiriki mafunzo yaliyokuwa yakiendeshwa na NATO). WATU WOTE WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA HAWAWEZI KABISA, NA HAIWEZEKANI, UKATAE AMRI YA MKUU WAKO. NA KAMANDA MKUU KULIKO WOTE WA VYOMBO VYA ULIMZI NA USALAMA NI AMIRI JESHI MKUU. UKIAMBUWA CHOCHOTE NI AMRI.

Wanaoleta habari za sijui kukataa, waouuze tu, hawajui chochote.
Umenena Kweli !
 
Mamba anatisha akiwa ndani ya maji, nje ya maji màmba ni sawa na mjusi tu.

Saa hizi ukimkuta Diwani Athman hata ukimtemea mate anaweza kukuomba wewe msamaha.

Mtoa mada umem over estimate Diwani bila sababu, I assure you he is nobody in this country.
Wewe jamaa una Siri nyingi Sana,nje ya mfumo kiukweli mtu anakuwa kibogoyo..
 
Back
Top Bottom