Diwani Athumani Msuya atenguliwa Ikulu

Diwani Athumani Msuya atenguliwa Ikulu

Sema nyie watu ni wakatili sana asee hivi nyie ni binadamu kama sisi kweli? Mtu akitofautiana na wewe kimtazamo unamuona adui unampa zawadi ya mateso na kifo?
Tatizo nyinyi mmejiaminisha matatizo ya watu kutekwa na kupotea yameanzia kwenye utawala wa Magufuli na Diwani, mambo ya Watu kupotea au kufa yapo tokea enzi za Nyerere tena enzi za nyerere hata mitandao vyombo vya habari,hakukuwepo kama Sasahivi, hivyo walifanya walivyotaka enzi hizo tunasikiliza redio Tanzania (tbc)hata mtu wako akipotezwa hauwezi fungua mdomo kusema, Hata Sasahivi bado watu wanapotea tu sema bado mna mahaba na mama, kwenye utawala kuko hivyo kuna watu lazima waminywe ndipo unaweza kuendesha mchi maana wengine wako kwa ajili ya vurugu tu.
 
Acha kutumia herufi "x" kwenye maneno utakuwa shoga wewe.
Naweza sema akili yako inashida fulani!
Anaetumia "X" anatumia kama mbadala "S" sio "Z", Hivo basi ulichoshindwa kuelewa ni kiwa hiyo ni typing error, na kwa kuthibitisha ilo angalia herufi hizo mbili ukaribu wake katika keyboard ya simu yako.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Kawaida serikalini ukikataa uteuz wao wanasema wamekutengua.

Ni kama wakati wa Kangi lugola Ninja alipomuaibisha hadharani mkuu wa magerza. Jamaa aliamua kuachia ngazi kwa hiari na roho safi siku hiyo hiyo jioni. Lakini Kesho yake Jiwe akasema kamfukuza
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Daaah
 
Labda kama ametoka kabisa nje ya mstari mwekundu. ila kama ametoka nje ya mistari mingine 'laaah' hakuna yeyote wa kumfanya kitu chochote unless aya ya kwanza..
 
Suala la peter wa royal tour, halihusiki kweli?
Kutenguliwa balozi wa USA, na yeye kuondolewa kwake madarakani, huenda walishindwa kumpa mama siri na malengo halisi ya peter!
Nchi ngumu sana hii.
Maswali ni mengi kuliko majibu
Malengo ya peter ni yepii
 
Kukataa uteuzi wa Rais anajiweka ktk hatari kubwa sana, nakwakatiba hii ilivyompa Rais mamlaka wanaweza mchomekea kesi nzito akafie gereza la ukonga
Anakundi lake la kumtii na hatujui madhara ya kundi lake kwa maaana ya wanaomuunga mkono hatuwajui na hatujui uwezo wao

Kikubwa Mungu asimame na taifa
 
Siku hizi CDF mkuu mkuu wa majeshi ya Ulinzi na usalama ndiyo mwenyekiti wa jopo la ujasusi na yeye hupata taarifa nyingi na ukumbuke yeye ana ndege za kivita vifaru makombora usimweke level ya IGP na hao wengine
Wabongo bana,ehe

Ova
 
Sema nyie watu ni wakatili sana asee hivi nyie ni binadamu kama sisi kweli? Mtu akitofautiana na wewe kimtazamo unamuona adui unampa zawadi ya mateso na kifo?
Ndiyo mifumo yote iko hivyo duniani
Kutekana,kuua nk
Dunia ni uwanja wa fujo

Ova
 
That is rare...there is only one way and the way is clear. Awekewe ulinzi wa kutosha. Kama alifanya mambo ya maajabu, hii ni payback time
Nani amuwekee Ulinzi sasa ?
 
Ameukataa uteuzi na siyo kutenguliwa, niliandika hapa juzi! Iweje Mkurugenzi TISS kupelekwa Ikulu?

Diwani ni mwenye kujitambua, ameukataa uteuzi ule. Diwani ana uzoefu na serikali zaidi ya nne za CCM.

Diwani ni afisa aliehudumu idara mchanganyiko za nchi hii kwa kiwango cha juu. Diwani anaijua michezo yote ya CCM na magenge yake. Diwani sio Kabudi au Lukuvi!

Diwani ndiye afisa mwenye siri nzito za kilichojiri kati ya serikali hizi mbili. Serikali ya Magufuli na hii ya Samia!

Pia ieleweke yeye ndiye alikuwa madarakani wakati JPM anafariki Dunia. Yote yaliyojiri katikati hapo, ni Diwani ndiye anaeyajua!

Diwani sio wa kubezwa! Diwani anastahili kupewa ulinzi kwa usalama wake! Kitendo cha kuikataa safe house, ina maana amekataa ku surrender mawasiliano yake yote ili kuanza kutumia mapya ya Safe House!

Na mengi bado yanakuja, maana kadri inavyonyesha ndio matobo yanavyozidi kuonekana.

"Rais Samia atengua uteuzi wa Diwani Athumani"

Mwananchinewspaper
Alhamisi, 05/01/2023.

Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Ikulu, Kamishna Diwani Athumani uliodumu kwa siku mbili baada ya kuteuliwa akitokea Idara ya Usalama TISS.

Kamishna Diwani aliteuliwa Januari 3, 2023 kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu, akitokea katika wadhifa wa Mkurungezi Mkuu wa TISS, nafasi aliyohudumu kwa siku 1,210 tangu alipoteuliwa na Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Januari 5, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, imeeleza kuwa nafasi ya Diwani imechukuliwa na Mululi Mahendeka aliyekuwa ofisa mwandimizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu.

Alamsikhi
10101.
Hana ubavu wa kuukataa uteuzi wa Raisi hata Mara Moja.
Akishakula ma Viapo mengi ya Kumtii Raisi
 
Kiuhalisia kuna kundi liko TISS linalomuingiza chaka mteuzi.

Kwanza kiutaratibu,alipaswa kumstaafisha kisha ndio ampatie uteuzi.

Halafu kiuhalisia hawa maafisa wa ngazi hiyo,huwa wanaishia kupelekwa ubalozini.

Hii maana yake ni kuwa Disconnect na mfumo.

Na kwa wale ambao huwa wamestaafu kisheria,huwa bado wanakuwa karibu na kitengovkama washauri.

Hata wateuzi mara nyingi hiwatumia pale wanapotaka kufanya verification ya jambo fulani nyeti.

Sasa mama yeye anatengua kwa nia fulani,halafu anakupeleka Ikulu ili utazamwe 24×7.

Huyu amelitambua hilo,na hii itamsumbua sana kichwa mteuzi.
Nyerere alitengua Gama kutoka DGIS na kuwa RC Dodoma
 
Sijui hua akipewa jina au ushauri hua anameza tu au anatafakari na kuuliza maswali?
Diwani amefanya kazi nzuri sana awamu ya tano. Leo hii unakuta mbowe na genge lake ndio wanataka atoke TISS na mama anakubali na kumshusha hadhi.
Uongo wa akina mbowe umekolea hadi kiongozi dhaifu wa ccm anaamini.
Ccm haijafanya kosa kuwashinda kabisa chadema kwenye uchaguzi mkuu 2020. Wananchi waliona kile kinachofanywa na ccm ya magufuli na kuipa ccm kura karibu zote.
Okay nimekusoma vyema kumbe hofu yako mkuu
 
Hizo hisia zako tu na uzushi hakuna mwenye ubavu wa kukata uteuzi wa rais. Mkurugenzi wa usalama wa taifa ni mtu mdogo sana hawezi kuwa hata tone ndani ya maji ya bahari. Hii nchi ni zaidi ya mtu awaye yote. Vilevile kumbuka rais ni mtu mkubwa sana nchi hii kwa mujibu wa katiba na hawezi kutishwa wala kukwamisha na limkuu wa idara moja ndani ya nchi yenye idara nyingi. Rais ni amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama, we mkuu wa idara moja tu ya usalama utatoa wapi kiburi? Hizo ni hisia zako tu rais anasimamia nchi yenye makomandoo na vyombo vingine vya siri. Sijui kama unaweza kukumbuka issue ya Imrani Kombe aliyekuwa naye mkurugenzi wa usalama wa Taifa. Alitaka kutumia uchaga wake kumsaidi mchaga mwenzake Mrema apate urais alichinjwa mchana kweupe.

Hakuna anayeweza kukataa uteuzi wa Rais, ni majuzi tu aliyekuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Venance Silvatory Mabeyo aliteuliwa baada tu ya kustaafu na hakukataa. Kwanza utaanzaje kukataa jambo la rais? Basi itakuwa hiyo nafasi aliipata isivyostahili, wale wanatakiwa wawe na utii wa hali ya juu usiotiwa shaka ya aina yoyote ndugu. Acha kumnenea uwongo.

Mkurugenzi wa TISS ni mtu mdogo sana??? Pole sana aisee! Ulisoma shule ya Kata ya wapi?
 
Back
Top Bottom