Diwani Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema afukuzwa Uanachama

Kwamba kwa sababu ni sehemu muhimu ya mageuzi basi hana mapungufu na wakiyasema mapungufu lazima wafukuzwe uanachama!

Hiki kweli ni chama cha Demokrasia na Maendeleo!
Hakuwa na sababu ya kwenda kuongea na nyombo vya habari masuala yaliyotakiwa yajadiliwe ndani ya vikao vya chama. Huyo diwani ni kiongozi tena ni mmoja wa madiwani wanoheshimika Arusha alishindwa nini kushawishi kikao cha ndani kiitishwe?
Huyu diwani alishafika bei kimyakimya sema yeye aliona aibu kuunga juhudi hadharani badala yake kapitia njia nyingine. Haiwezekani ajifanye hajui sababu za madiwani na hata wabunge wa nyama vya upinzani kuacha nafasi zao na kuhamia upande mwingine? Lazima anajua manunuzi makubwa yanayofanywa na wenyewe kufika bei.
 
Huu ni ujinga uliopitiliza. Chama kilichokomaa ni lazima kikubali kukosolewa. Kwa kumfukuza, kinathibitisha alichosema kuwa Arusha kweli kuna tatizo. Walitakiwa kumshukuru kwa kuwa muwazi na kufanyia kazi tuhuma zake. Uamuzi wa kumfukuza mtu uanachama hautakiwi kufanywa kirahisi rahisi hivi.

Amandla
 
Mbona huyo huyo Lema Kuna kipindi alimkosoa mhe. Lowassa kwa kutumia social network wakati lowassa yupo chama Cha chadema alipoenda kukutana na Magufuli ikulu mbona hakutumia vikao vya chama na Wala hakuchukuliwa hatua zozote na chama chake.Tusipende kutanguliza mahaba kwenye mambo ya msingi.
 
Utaratibu wa chama ufuatwe. Nyie akina January kuongea tu kwenye simu in person wala si hadharani wakalazimika kutembea kwa magoti. Wangeongea na vyombo vya habari ingekuwaje? Si wangeenda kuomba msahama kifudifudi?
 
WeweKILAZA TUU, MGANGA NJAA NDIO MAANA HUJAPATA UTEUZI HATA WA UDIWANI. NJAA MBAYA SANA
Wewe lazima utakuwa mfuasi mzuri wa kamanda msaliti, maana wafuasi wote ni wazuri sana kwa matusi bila hoja zozote za maana. Komaa kamanda, matusi ni mtaji mzuri kwenye siasa za upinzani 👏🏿👏🏿✌🏿🤞🏿👌
 
Angepewa hata onyo lakini sio kumfukuza,Kwa hali hii walau CCM kuna demokrasia maana kama wanachama "walimtukana" mwenyekiti na wakasamehewa ina maana kule walau kuna uvumilivu kidogo.
 
Na hapo kamchana Lema, imagine angemchana mwenye chama mwenyewe!

Halafu haohao baadae wanaibuka na ngonjera za hakuna Demokrasia nchini.

Kwa hiyo katiba yenu inataka wanachama wasifie tu na kukenulia viongozi wao?
 
Isaya Doita. Mtu mwerevu Sana. Alininoa Kiingereza nilipomaliza Darasa la Saba. Hakika namuheshimu Sana japo alisepa na daftari langu la notice Ila mbinu zake zilibaki kichwani. Nimekula Sana Hela ya wanafunzi wa Lugha ya Malkia.
Shukurani pia kwa Mwalimu Mwiga, Roho yake ipumzike kwa Amani.
 
 
Angepewa hata onyo lakini sio kumfukuza,Kwa hali hii walau CCM kuna demokrasia maana kama wanachama "walimtukana" mwenyekiti na wakasamehewa ina maana kule walau kuna uvumilivu kidogo.
Hapa upo sahihi kabisa. Ile kutoa tu mtazamo wake haikutosha kuondolewa uanachama mara moja tena ndani ya saa 24. Ilitakiwa onyo kwanza. Huyu diwani tunamfahamu vizuri, ni mtu committed na CDM pamoja na majukumu yake ya udiwani. Si mropokaji wala mkurupukaji. Kuna wakati Komu na Kubenea walileta hitilafu la kiuongozi ndani ya chama lakini chama kikamalizia mambo yao kimyakimya na wao kuomba msamaha. Kwanini haraka haraka kwa huyu diwani? Lema na wenzake ajipime, wanapwaya mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…