TANZIA Diwani wa CCM na Mwenyekiti Halmashauri Wilaya ya Nzega afariki kwa ajali

TANZIA Diwani wa CCM na Mwenyekiti Halmashauri Wilaya ya Nzega afariki kwa ajali

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Itilo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nzega Mji, Wilayani Nzega kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Paschal Kigaru amefariki Dunia kufuatia ajali ya barabarani ambayo imehusisha gari alilokua amepanda kugongana na gari jingine usiku wa kuamkia Februari 17, 2026 Wilayani humo

Akitoa taarifa ya kifo hicho kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na Mkuu wa mkoa wa Tabora ,Paulo Chacha amesema wakati ajali hiyo ikitokea marehemu alikuwa kwenye mizunguko yake binafsi

RC Chacha ameeleza kuwa mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa siku ya Alhamis, February 19 ,2026 Wilayani Nzega huku chanzo cha ajali kikiendelea kuchunguzwa kwa ukaribu zaidi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai, kwa njia ya simu amesema kuwa kama wana Nzega wamesikitishwa sana na tukio hilo, akimwelezea Marehemu alikua kiongozi bora na mwenye utu, hivyo kama Wilaya imepoteza mtu muhimu.

Wakuu kama heading inavyojileza

Screenshot 2026-02-17 185050.png
Picha za hali ya gari
FB_IMG_1771349733732.jpg

FB_IMG_1771349730482.jpg
 
Back
Top Bottom