t blj
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 7,035
- 16,705
Umenifanya nimkumbuke mzaramo wangu pia!Usicheke nishawai kukutana nae mmoja. Aliniteka kweli kweli.
Nilikuwa napata pata hela kizembe kazini nikawa napenda sana kununua viwanja vya bei nafuu.
Sasa yeye mzaramo mwenyej wa dar ndie akawa ananishtua akiona kiwanja cha bei nafuu kama dalali vile,,, maana huko chamazi, mbande, chanika, kitunda , kivule kote ana ndugu zake.
Kama utani nikajikuta nimemnunulia na yeye kimoja.
Waswahili wa kike sio kabisa katika mahaba.. kwanza wana heshima vibaya mnoo hawaoni ishu kukupa shikamoo bwana wake kisa umemzidi 2 yrs tu
Usiombe ukutane na hawa mabinti waliocheza unyagoo.. binti mdogoo ila jitu zima na ndevu zako unadekezwaa kama mtoto. Akija geto sasa akapikaa hata chai tu unatamani isiishe jinsi ilivyo tamuu na viungoo kibao. Hanunui chakula chochote hata mkate. Yeye lazima apike mwenyewe. Mko wawili tu ila ataamka mapema apike chapati ili aandae chai. Wakati nje zinauzwa kibao
Halafu sasa mizinga yake midogoo.. nikimpa laki ananiona wa maana kwelii.. kumbe hiyo laki ukitoka na sister duu kwenda kiwanja tu inakatika masaa tu
Wekend vijana wenzangu jobs wanaenda viwanja samak samak ama elements . Muhuni najifungua na mzaramo wangu mpaka j2
Hawa watu wana mapenzi ya kudekeza na full heshima , na hawana makuu linapokuja swala la matumizi ya pesa , kama ulitokea kwenye mahusiano yenye heka heka , unaweza ukatua nanga kirahisi sana , Sishangai yaliyotokea kwa muheshimiwa diwani ,