Dj Choka hana busara hata kidogo. Maradhi yake isiwe sababu ya kuwahukumu watu

Daah , Kidney injury ndio inakuwaje mkuu? Kama hutojali
AKI ni ajali ya muda mfupi inayoipata figo. Kuna kiwango maalum kinachotenganisha aina hizo mbili kutokana na uwezo wake wa kuchuja damu.

Lakini, usipowahi kuitibu Acute Kidney Injury huwa inapelekea ugonjwa wa figo wa muda mrefu (CKD)
 
hilo jina la choka nako sio. Unajiitaje choka? maneno huumba
 
DJ Choka - DJ Hugo kipindi ana Blog yake alisaidia sana wasananii wa Bongo Flavor kupush miziki yao ,wamsaidie bana ,Dayamondi kama ana zaidi ya 20B kwenye account ,kumsaidia DJ Choka hata fedha ya kwenda kumfanyia implantation ya Kidney india hashindwi.
 
Serikali ifikirie inshu ya dialysis iwe Bure kama zenji Kuna kijana mdogo nae anateseka Arusha Hadi huruma serikali ifanye jambo

Kwa hali iliyopo ipunguze gharama, lakini pia ikague upya pombe kali , nyingi zinaua vijana. Hadi mamlaka za rwanda zimeshtukia
 
Hapo Dar , vijana wanaoznza kujipata hasa hawa wasanii , waigizaji na comedians., wana ratiba za kwenda kwenye bars kutwa ili kuweka heshima..Wengine wanadai hizo sehemu watafuta connections , mwishoe wanaishi kutumia pesa nyingi kwenye starehe za kishamba .

Wakipata matatizo , hayo makundi wanayoenda nayo bar hayapo tena .
 
AKI ni ajali ya muda mfupi inayoipata figo. Kuna kiwango maalum kinachotenganisha aina hizo mbili kutokana na uwezo wake wa kuchuja damu.

Lakini, usipowahi kuitibu Acute Kidney Injury huwa inapelekea ugonjwa wa figo wa muda mrefu (CKD)
Asante mkuu
 
Ni kweli kabisa wanakuja kushtuliwa na maradhi na ile fame haipo tena.
 
Mke wake yuko wapi? Ndugu zake? marafiki zake ni kina nani? kanisani/msikitini kwake ni wapi? Katika maisha yake aliwekeza kwa nani?

Ana uhusiano gani na Diamond platinum mpaka amtupie lawama?

Ukiwa mzima tafakari haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…