TANZIA DJ Steve B afariki dunia

TANZIA DJ Steve B afariki dunia

kuna wakati fulani staff wa clouds media waliingiza siasa kuhusu maradhi ya steve B wakimlaumu DJ JD kwa kwenda kumtembelea na kupiganae picha. sasa sijui huu msiba wataubeba wao au familia ya marehemu?.
Hawa viumbe wakipata umaarufu kidogo wa ndani ya mipaka ya nchi huwa wanajidai ni watu special sana maradhi ya mmoja Kati yao huwa wanafanya ni Jambo la aibu pindi wanaposhindwa kumudu gharama za matibabu wakat inatakiwa Jambo liwe wazi tu ili mwenye moyo wa kutoa atoe msaada, japo haiepushi kifo lakini itasaidie kupunguza sehem flan ya tatizo
 
Hawa viumbe wakipata umaarufu kidogo wa ndani ya mipaka ya nchi huwa wanajidai ni watu special sana maradhi ya mmoja Kati yao huwa wanafanya ni Jambo la aibu pindi wanaposhindwa kumudu gharama za matibabu wakat inatakiwa Jambo liwe wazi tu ili mwenye moyo wa kutoa atoe msaada, japo haiepushi kifo lakini itasaidie kupunguza sehem flan ya tatizo
Kwa Luge walificha mwisho wa siku yalipowashinda wakaanza kutembeza bakuli.

Clouds ni watu wa hovyo sana
 
Bora hizi pombe za ngano kuliko spirits, spirits zinachoma kabisa.

Visungura na Double Kick vitaleta balaa kwa vijana wengi sana miaka 10 inayokuja

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Hivi wale wazee kule vijijini wanakunywa gongo toka walivyokuwa vijana hadi uzee sikuwahi kusikia hayo tofauti ni nini? Au hawa vijana wa mjini hawali vzr na kunywa maji, maziwa kwa wingi?
 
Kama namuona vile kavaa kaptula ya grey ya Tambaza, tunakwenda kwao wakati wako hapa Mikocheni karibu na Morocco.

Nakumbuka back in the days.Tunakwenda studio East Africa FM kumpokea kipindi chake huku tunamsikiliza kwenye redio...

So many good memories maan.
Regent estate, muanzilishi wa regent party
 
R.
Dj Steve B aliyejipatia umaarufu miaka ya mwanzoni mwa 2000 amefariki dunia leo. Dj Steve B maarufu pia kama Dj Skills alikuwa maarufu kiasi cha kutajwa sana katika nyimbo nyingi za bongofleva za miaka ya 2000.

Nyakati ngumu hazipiti ila watu wagumu wanapita, pumzika kwa amani Steve BView attachment 2704085
R.I.P
Jamaa kwa kumuona kwenye picha tu,anaonekana alikua mpole sana.
 
Ndio mwisho wako wa maarifa? umeshasoma causes za kidney failure zipo ngapi? common ni zipi? unadhani kila mtu anayeumwa figo ni mnywa pombe? nenda pale muhimbili dialysis alafu uulize walevi ni wangapi na wasiokunywa ni wangapi, utagundua huna akili.
Achana na kilaza huyo, mm ninafahamu watu zaidi ya watano walifariki kwa tatizo la figo na hawajawahi kugusa pombe
 
Nakumbuka kuna jingle moja aliimba marehemu Mr Ebbo "Dj Steve wewe ndiyo unafanya watu wasilale"

Hiyo ni safari yetu sote, tangulia nasi tupo nyuma yako.

Pumzika kwa amani mwamba 😭😭

"Sitivibii wewe unamfanya muji unatishingika , asandee" - Abel Motika(Mr Ebbo).

Poleni Ndugu , Jamaa na Marafiki.
 
Back
Top Bottom