Dk. Lwaitama ahoji, kama Lissu anasema hataki maridhiano, je anataka kuchukua silaha kupambana na serikali? Asisitiza umuhimu wa mazungumzo ya vyama

Lissu anataka kuigiza watu mstituni kidai Katiba...CDM kuweni makini.

Huwezi kudai katiba mpya bila kumshirikisha mkuu wa dola, mwambieni Lissu hapa siyo Somalia.
 
Wapi Lissu amesema hataki maridhiano? Lissu alichokataa ni ulaghai unaofanywa na CCM katika mazungumzo ya maridhiano. Mazungumzo yamefanyika jee nini kimebadilika? Watu wameendelea kutekwa,kuteswa na kuuliwa kikatili, wizi na uchafuzi wa mchakato wa uchaguzi ndiyo kama tulivyoona mwezi November 2024,CCM waliahidi kuwa yaliyotokea 2019 hayatajirudia tena jee wametimiza ahadi yao? Mazungumzo ya kuzungumzia amani huku CCM wameficha AK 47 kifuani huo ni upumbavu.
Mdo maana jamaa yenu anakwenda kukwama asbh tu.
 
Dk. Lwaitama, moja kati ya nguli wa zamani pale UDSM ameshangazwa na msimamo wa Lissu kwamba hataki kuzungumza au kuridhiana na yeyote. Katika moja ya makala zake, mzee wa maswali magumu Ansbert Gurumo, katika moja ya makala zake, alisema kwamba Lissu ni Mwanasiasa ambaye anaweza kutoa kauli mwenyewe, halafu akaipinga baada ya sekunde chache

Gwiji hilo la taaluma ya siasa limesema lazima vyama vya siasa vizungumze kwa kuwa hiyo ndio siasa, kwamba lazima umshawishi mwenzako akubaliane na wewe.

Dk. Lwaitama kwa mara kadhaa amekuwa mshauri wa Chadema katika mambo mbalimbali. Ni Dokta mbobevo. Lissu kwa muda mwingi amekuwa akitumia muda wake na Mdude Nyagali, Askofu Mwanamapinduzi ambaye haijulikani kama alimaliza shule ya msingi, na pia alichukuliwa fomu ya kugombea na SATIVA, ambaye hela zake anazipata kwa kubeti, na kupewa tenda ya kutukana watu mitandaoni.

View attachment 3190484
Yote sawa ila#£ mbowe must go
 
Hayo unayosema yamekubaliwa siyo maridhiano bali hayo ni haki yao ya kikatiba ni kwa vile tu yule mwendawazimu aliyaweka kibabe.
Na nani alikuwa na ubavu wa kumlazimisha Rais azingatie hizo unazoita haki yao ya kikatiba? Tupende tusipende ulikuwa ni uamuzi wa Rais peke yake na moja ya mapungufu ya Katiba yetu inampa haki ya kuikiuka bila kuzuiwa na mtu yeyote. Mbowe alijua hilo.
Maridhiano ilikuwa kuweka misingi mizuri ya mifumo ya uchaguzi na sheria ili yale yaliyotokea 2019 na 2020 yasijirudie tena lakini si wote tumeona yale ya 2019 yamejirudia tena na kuzidi kwani 2019 Magufuli alifuta uchaguzi wote lakini hakuua mtu lakini 2024 uchaguzi ulivuruguwa kwa 100% na zaidi wagombea wengi walitekwa,waliteswa na kuuwawa sasa watu kama hawa utafanya nao maridhiano kweli?
Maridhiano katika maeneo hayo hayakufikiwa. Hapa tena msimamo wa Lissu ilikuwa chama chake kisishiriki mpaka Tume Huru ipatikane. Unadhani CDM wasingeshiriki wangekosekana wapinzani wa kushiriki? Unaona Chaumma wamejipatia ushindi kwa mara ya kwanza. Kushiriki kwa CDM umeweka wazi namna mfumo uliopo hauwezi kutoa matokeo ya haki. Matokeo yale yanaipa CDM nguvu katika madai yao ya Tume Huru ya Uchaguzi. Na hata kama watagombea serikali itahakikisha kuwa angalau matokeo yawe yana uhalisia. Sidhani kama ushindi wa 99% ya vitu vya ubunge utarudiwa tena.

CDM ingefuata msimamo wa Lissu ( ambae hakujisumbua kujiandikisha kupiga kura. Kama nakumbuka vizuri hakufanya hata kampeni ya maana) wangekosa huo ushahidi na CCM wangesema kuwa wangeshindana wangeweza kushinda. Kama Chaumma wameshinda itakuwa CDM? Aidha, CDM na wapinzani wengine wana nafasi ya kujipanga vizuri kwa sababu wanajua hamna lililobadilika. CDM hawezi kubeba lawama ya watu wake kutotendewa haki.

Amandla...
 
Na nani alikuwa na ubavu wa kumlazimisha Rais azingatie hizo unazoita haki yao ya kikatiba? Tupende tusipende ulikuwa ni uamuzi wa Rais peke yake na moja ya mapungufu ya Katiba yetu inampa haki ya kuikiuka bila kuzuiwa na mtu yeyote. Mbowe alijua hilo.

Maridhiano katika maeneo hayo hayakufikiwa. Hapa tena msimamo wa Lissu ilikuwa chama chake kisishiriki mpaka Tume Huru ipatikane. Unadhani CDM wasingeshiriki wangekosekana wapinzani wa kushiriki? Unaona Chaumma wamejipatia ushindi kwa mara ya kwanza. Kushiriki kwa CDM umeweka wazi namna mfumo uliopo hauwezi kutoa matokeo ya haki. Matokeo yale yanaipa CDM nguvu katika madai yao ya Tume Huru ya Uchaguzi. Na hata kama watagombea serikali itahakikisha kuwa angalau matokeo yawe yana uhalisia. Sidhani kama ushindi wa 99% ya vitu vya ubunge utarudiwa tena.

CDM ingefuata msimamo wa Lissu ( ambae hakujisumbua kujiandikisha kupiga kura. Kama nakumbuka vizuri hakufanya hata kampeni ya maana) wangekosa huo ushahidi na CCM wangesema kuwa wangeshindana wangeweza kushinda. Kama Chaumma wameshinda itakuwa CDM? Aidha, CDM na wapinzani wengine wana nafasi ya kujipanga vizuri kwa sababu wanajua hamna lililobadilika. CDM hawezi kubeba lawama ya watu wake kutotendewa haki.

Amandla...

..Tundu Lissu aliunga mkono maridhiano mpaka pale alipojiridhisha kwamba CCM hawana nia njema ndipo alipoyapinga.

..Kuachiwa kwa Mbowe, kufutwa kwa kesi za kubambikiwa, mahabusu 400+ kufunguliwa, wakimbizi kuhakikishiwa ulinzi, zilikuwa PRE-CONDITIONS za kuanza mazungumzo, na sio madai au dondoo za maridhiano.

..According to Lissu, maridhiano yalikuwa yanahusisha kufumuliwa na kuundwa upya kwa mifumo na taratibu zetu za uchaguzi, na kuendeleza mchakato wa Katiba mpya.

..Mwenyekiti Mbowe alikuwa mgumu kidogo kubaini na kujitokeza kueleza kwamba maridhiano yamefeli, lakini na yeye baadae alijitokeza na kuungana na kauli kwamba maridhiano yalifeli.
 
Mbona sasa katiba mpya haipatikani na ni haki ?

Unadhani katiba,mpya ni sawa na kwenda haja kubwa chooni?

Key boards warriors mnashangaza sana.

Sijui umeelewa kilichoandikwa.
Kimsingi hakuna mahala niliposema nataka katiba mpya, bali nimeshangaa kuona watu wanataka maridhiano kwa masuala ambayo yapo kikatiba na sio favour.

Uwe na siku njema, lakini Mwenyezi akubariki pia nakukupa hekima na busara za kutosha pamoja na kuibariki familia yako ndugu yangu.
 
..Tundu Lissu aliunga mkono maridhiano mpaka pale alipojiridhisha kwamba CCM hawana nia njema ndipo alipoyapinga.
Lakini hii sio narrative ambayo inasambaa. Kinachosambaa ni kuwa aliistukia toka Mbowe alipoipendekeza kwa mara ya kwanza. Kuwa yeye na wenzake wanne walimkatalia na ndio maana Mbowe amewashughulikia kutokana msimamo wao( Aliyepona ni Wenje peke yake kwa sababu zilizo wazi). Ndio maana watu wanadai kuwa mazungumzo yale hayakuwa na faida yeyote. Kitu ambacho ni uongo. Na Lissu anajua hilo.
..Kuachiwa kwa Mbowe, kufutwa kwa kesi za kubambikiwa, mahabusu 400+ kufunguliwa, wakimbizi kuhakikishiwa ulinzi, zilikuwa PRE-CONDITIONS za kuanza mazungumzo, na sio madai au dondoo za maridhiano.
Kwa hiyo mazungumzo yalianza kabla Mbowe hajaachiwa? Wakati huo Boss si alikuwa Lissu? Sasa mbona watu wanadai yalianza baada ya Mbowe kulambishwa asali alipoenda Ikulu mara baada ya kutoka gerezani? Na kama yalikuwa ni pre-condition tu kwa nini Mbowe abebeshwe shutma za usaliti?
..According to Lissu, maridhiano yalikuwa yanahusisha kufumuliwa na kuundwa upya kwa mifumo na taratibu zetu za uchaguzi, na kuendeleza mchakato wa Katiba mpya.
Nae ni lazima alijua ugumu wa CCM kukubali hilo. Kuna wakati zilikuwa zinatoka taarifa zisizo rasmi zikielezea jinsi Kinana anavyokuwa na wakati mgumu kushawishi wengine.
..Mwenyekiti Mbowe alikuwa mgumu kidogo kubaini na kujitokeza kueleza kwamba maridhiano yamefeli, lakini na yeye baadae alijitokeza na kuungana na kauli kwamba maridhiano yalifeli.
Ni kweli unalosema. Lakini yeye kuendelea na mazungumzo kulionyesha kuwa walishiriki in good faith kuliko wenzao. Kinachonishangaza ni watu kuongea kama vile mazungumzo hayo bado yana endelea. Na Lissu haisahihishi hiyo imani.

Amandla...
 
Lakini hii sio narrative ambayo inasambaa. Kinachosambaa ni kuwa aliistukia toka Mbowe alipoipendekeza kwa mara ya kwanza. Kuwa yeye na wenzake wanne walimkatalia na ndio maana Mbowe amewashughulikia kutokana msimamo wao( Aliyepona ni Wenje peke yake kwa sababu zilizo wazi). Ndio maana watu wanadai kuwa mazungumzo yale hayakuwa na faida yeyote. Kitu ambacho ni uongo. Na Lissu anajua hilo.

Kwa hiyo mazungumzo yalianza kabla Mbowe hajaachiwa? Wakati huo Boss si alikuwa Lissu? Sasa mbona watu wanadai yalianza baada ya Mbowe kulambishwa asali alipoenda Ikulu mara baada ya kutoka gerezani? Na kama yalikuwa ni pre-condition tu kwa nini Mbowe abebeshwe shutma za usaliti?

Nae ni lazima alijua ugumu wa CCM kukubali hilo. Kuna wakati zilikuwa zinatoka taarifa zisizo rasmi zikielezea jinsi Kinana anavyokuwa na wakati mgumu kushawishi wengine.

Ni kweli unalosema. Lakini yeye kuendelea na mazungumzo kulionyesha kuwa walishiriki in good faith kuliko wenzao. Kinachonishangaza ni watu kuongea kama vile mazungumzo hayo bado yana endelea. Na Lissu haisahihishi hiyo imani.

Amandla...
Kinachokera wengi ni Mbowe kusifia maridhiano, na hata kuonyesha maridhiano yalikua na manufaa makubwa, haliyakua watu wazima wote tunaona.
 
Sijui umeelewa kilichoandikwa.
Kimsingi hakuna mahala niliposema nataka katiba mpya, bali nimeshangaa kuona watu wanataka maridhiano kwa masuala ambayo yapo kikatiba na sio favour.

Uwe na siku njema, lakini Mwenyezi akubariki pia nakukupa hekima na busara za kutosha pamoja na kuibariki familia yako ndugu yangu.
Mikutano ya hadhara ilizuiwa wakati ipo kikatiba na kisheria mbona Lissu hakufanya wakati ilipozuiwa?
 
Maridhiano yamepelekea ccm kushinda 99% uchaguzi serikali za mitaa
 
Back
Top Bottom